Dhamiri yamlazimisha Rais Magufuli kukiri uharibifu katika uchaguzi wa Oktoba 2020

Same Blah blah blah since genesis of multipartism in Tz, common phrases now. You're wasting your time.
Lakini wewe huo upumbavu wako utaisha lini? Kiingereza chenyewe hakieleweki. Vile unajihesabu katika wajuzi wa hiyo lugha. Ondoa hapa huo upumbavu wenu wa .....i cannot reach you!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Anasema madiwani wa Dar es Salaam hawakuchaguliwa na watu. Walichaguliwa na nani?

Nilichoelewa: Madiwani wa city council hawana direct electorate. Ukitaka kujenga hoja vizuri jiepushe na hila katika hoja yako. Yaani jiepushe na spinning. Hapo ndipo naona BAK/Mwamakula amejikwaa.
 
Kongole kwa ufafanuzi mzuri
Tatizo la mleta mada na Mwamakula wana uelewa mdogo mno wa alichosema Raisi .Raisi alichosema kifupi ni kuwa meya wa Jiji la Dar es salaam ni meya hewa na hakuna diwani hata mmoja anayechaguliwa udiwani chini ya jiji la Dar es salaam hayupo!! wote huchaguliwa udiwani kwenye manispaa ya Ilala ,Temeke, kinondoni,Ubungo sasa hao wanaoenda kumchagua meya wa jiji ni madiwani ambao hawakuchaguliwa na wananchi kuwa madiwani wa jiji sababu hakuna uchaguzi wa madiwani wa jiji upo wa madiwani wa manispaa.

Kwa muktadha huo ina maana hakuna diwani wa jiji wala meya wa jiji hao hawakuchaguliwa na wananchi na wala tume ya uchaguzi haijawahi simamia uchaguzi wa diwani yeyote wa jiji sababu hakuna diwani wa aina hiyo

Ndio maana Raisi akasema atavunja hicho kinachoitwa jiji la Dar sababu meya na madiwani wake hawakupigiwa kura na wananchi kuwa madiwani wa jiji ni kakikundi ka kihuni tu pale hakapo kisheria hata tume hawawajui madiwani wanaoitwa madiwani wa jiji na hawajawahi simamia uchaguzi wao

Alichoongea Raisi kwa upeo mdogo wa Mwamakula sio rahisi kuelewa
 
Uko sahihi kabisa!
With due respect kwa Askofu Mwamakula, nafikiri ame mis conceive alichosema Rais. Pengine ni kweli hakukuwa na uchaguzi mwaka 2020 bali uchafuzi lakini Rais hakuwa na maana hii.

Halmashauri ya Jiji la Dar (ambayo imevunjwa), haikuwa na eneo la kijiographia. Na kisheria, utaratibu wa kupata madiwani ulikuwa tofauti na hizo halmashauri zingine. Hawachaguliwi moja kwa moja na wananchi (kisheria). Madiwani wa Jiji, wanatokana na halmashauri za manispaa 5 zinazounda Jiji.
 
Nilichokigundua, jamaa sio kigeugeu. Kuna baadhi ya vitu anafanya bila hiari yake, yani anajikuta tu vimeshamtoka.

Kuna kitu hakipo sawa kuhusu huyu jamaa yetu, japo sijui ni kitu gani.
Unataka uniambie kwamba kichwa chake kinachanganya mafile
 
yaani hapo mmepata neno lakuongea wapinzani uchwara yaani katika aliyoongea yoote ya muhimu hamjayaona mmeona hilo tu yaani mtu ukikosa akili unakuwa na shida sana mwacheni apige kazi hata hiyo stand hamtoi hata asante jpm mtakalia majungu tu
Ficha mbali huu ujinga, huenda utakufaa huko mbeleni!
 
Inabidi kuopiga kelel kumwambia Jiwe kuwa yeye si Rais maana hakuchaguliwa na watu, yeye hana tofauti na Idd Amin aliyepindua serikali halali ya Obote au huyu wa Myanmar
Min Aung Hlaing

View attachment 1711398

The Tatmadaw proclaimed a year-long state of emergency and declared power had been vested in Commander-in-Chief of Defence Services Min Aung Hlaing. It declared the results of the November 2020 general election invalid and stated its intent to hold a new election at the end of the state of emergency.
hizo ni dharau kwa watz!!! kwa hiyo Kama sio watu ni ,ni viumbe gani walimchagua!!
 
Ukiona magufuli ana act kama kukiri kosa basi huo ni muda wa kuwa makin kuliko maelezo.. sio muda atawapiga kanzu.sawa wapinzan? Anawatia chenga kuja kushtuka mmepigwa tobo goli la 3 chaliii...msisema sikusema
hawawezi kukuelewa mkuu hawa.huwa wanaelewa baada ya kuona matokeo siku zote.
 
Na unafiki pia wa kujiona yeye mporaji alichaguliwa lakini madiwani hawakuchaguliwa katika uchaguzi ule ule uliosimamiwa na Tume FAKE.
Kama ni utawala wa mabavu, Basi mbowe ni phd, na kale ka utaratibu ka tiaraei ka 10% posho za wabunge,na kale ka mfumo ka kiti Cha u chairman ni ka ukoo wake,n.k

Na Kama ni unafiki ,Basi tundu lisu ni PhD holder tena with honor.( 1.).rais aliyepita alimzonga Mara dhaifu,Mara fisadi,Mara hakusanyi mapato,awamu hii ka change gia tena,Bora rais aliye pita.( 2.).utawala ule tundu alipga kelele madini yanazolewa hovyo na wazungu,umekuja utawala wa Sasa, likawekwa azimio la kubadilisha sheria za mikataba ya madini,tundu aka chenji gia,ooh tukibadilisha sheria za mikataba ,tutashitakiwa. watu Kama Hawa akina lisu,na mbowe ,ndo mnapiga miluzi humu wapewe nchi!!!???
 
DHAMIRI YAMLAZIMISHA RAIS MAGUFULI KUKIRI UHARIBIFU KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA 2020!

Nilipokuwa nahojiwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, nililazimika kumueleza mmoja wa maofisa waliokuwa wananihoji nikasema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 haukuwa Huru na wala haukuwa wa Haki. Aliponiuliza kama nilikuwa na ushahidi nilimjibu kuwa ndio ninao ushahidi!

Kama Madiwani waliopatikana katika Uchaguzi ule wamekataliwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama chao kwa kuwaambia hadharani na ametamka kwa ujasiri kuwa hawakuchaguliwa na watu, je walichaguuliwa na nani? Jibu hapa rahisi na la wazi nalo ni kuwa walichaguliwa na Tume ya Uchaguzi!

Tunaweza kusema kuwa kwa maneno na kauli ya Rais Magufuli, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haikutenda Haki na haijawa Huru machoni pa Watanzania na hata machoni pake yeye mwenyewe. Kama Madiwani wale hawakuchaguliwa na watu, sahihi kabisa pia kuwa Wabunge, na Rais nao hawakuchaguliwa na watu kwa kuwa wote walipatikana katika Uchaguzi mmoja uliosimamiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ndiyo inayolalamikiwa!

Tunawaalika Watanzania wote kujitokeza na kushiriki kwa kikamilifu katika kampeni za kuhamasisha umma wa Watanzania kuhusu umuhimu na uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Nitakuwa nikingoza kampeni hizo katika nchi nzima nikiwa nimevalia majoho ya Kiaskofu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Tumfuate
 
Tatizo huyu bwana ni kigeugeu yaani mbele za camera huwa anaropoka kuwaumiza waliojitoa kufuata alichokitaka/maagizo yake alafu kwenye audience anawaanika. NYUMA YA PAZIA HUWA NI YEYE AMBAE ANAAGIZA VYOTE HIVYO
Ngumu Sana kuishi na mtu wa aina hii
 
Nilichoelewa: Madiwani wa city council hawana direct electorate. Ukitaka kujenga hoja vizuri jiepushe na hila katika hoja yako. Yaani jiepushe na spinning. Hapo ndipo naona BAK/Mwamakula amejikwaa.
Wewe jibu swali. Kama hawakuchaguliwa na watu wamechaguliwa na nani? kama hukumsikia akisema hivyo nyamaza wajibu wenye akili
 
Back
Top Bottom