Serikali imepiga marufuku Halmashauri kuingia makubaliano na NGO’S bila kuishirikisha

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
NGOS.jpg

Serikali imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’S) bila kupitia na kuihidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayaendani na vipaumbule vya Serikali ambayo inakusudia kuwasaidia wananchi. Hayo yamesemwa mkoani Tabora na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora , Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na Urambo.

Amesema kuwa kabla ya kuanza utekelezaji wa shughuli za NGO’s ni vema Halmashauri zikapeleka maombi ya mashirika ambayo yameomba kufanyakazi katika maeneo yao ili Serikali ione kama kweli inaendana na vipaumbele ambavyo imepanga katika kuboresha maisha ya watanzana ambao maisha yao yako chini.

Aidha, amesema mashirika hayo yamekuwa yakidai pesa ya kusaidia Watanzania kutoka kwa wafadhili lakini matokeo yake fedha hizo zimekuwa zikiishia kuwanufaisha watu wachache na wanapoandika taarifa kwa watu waliowapa fedha wadai kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli imeshia mifukoni kwa wachache. Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa jami husika , kwa Serikali na wafadhili husika.
 
Hebu serikali inihakikishie kodi ninayotoa inaenda sehemu husika kwanza.
 
Leta huo uamuzi kamili, kuweka link wakati watu hatujui kutumia twitter hakutakupa majibu mazuri
 
Hakuna NGO inaweza kutoa fedha zake ili zifujwe. Hii dalili tosha kuzuia maendeleo kwenye halmashauri na manispaa zinazoendeshwa na vyama vya upinzani. Kwanini serikali ifikie hatua hiyo kwani tayari vyanzo vya mapato za halmashauri hizo serikali kuu imechukua halafu wanaleta masharti haya mapya..
Inabidii tuishi kama North Korea
 
Sijaona mantiki wala uhusiano wowote kati ya marufuku hii na tuhuma kuwa mashirika hayafikishi fedha wanazopata kwa walengwa waliotumika kupata hizo. Aidha ufumbuzi wa tatizo siyo hii marufuku. Kwa hali hii nini maana ya Mamlaka za Serikali za Mitaa? Hata kushirikiana na NGO mpaka kibali cha serikali kuu! Incredible! Iko wapi tena dhana ya 'hands off, eyes on'? Methinks serikali za mitaa ndizo zilizopo katika nafasi nzuri zaidi kuyasimamia hayo mashirika na siyo serikali kuu. Jukumu la serikali kuu ni kufuatilia huo ushirikiano na inapodhihiri kuwa kuna tatizo basi inachukua hatua. It is primitive thinking kudhani serikali kuu inaweza kufanya kila kitu. Kinachotakiwa hapa ni mfumo bora wa kitaasisi wa ufuatiliaji, usimamizi na uwazi.
 
kila kitu kinapitia "ofisi ya raisi" bla bla bla, raisi hajiamini na hawaamini wasaidizi wake pia
 
Wacha we! Jamaa kwa kujinasibu hawa kwamba wanasaidia watu wao, waseme kwanza kodi za watu hawa maskini zinatumikaje kuwaondelea umaskini.

Serikali ina uchungu kweli kweli ndio maana inawanunulia bombadier wapande watz na kuwajengea flyovers.
 
Kwani sheria zinasemaje? Sababu ya kwanza haimake sense, kwa sababu NGO haipo kwa ajili ya kusaidia vipaumbele vya serikali bali kwa ajili ya mambo ambayo yapo kwenye mipango yao na mahitaji ya jamii kwa jinsi wanavyoona wao. Ukizingatia pesa hazitoki serikalini, hiyo sababu haina mashiko kabisa.

Sababu ya pili ni suala la ufuatiliaji. Kwa nini chombo kinachohusika na kuzisajili kisiwe na auditing mechanism ya kuangalia fundraising zao na jinsi wanavyotumia hizo funds?

Yaani hapo utoke kupitia mlolongo wa kusajiliwa na baada ya hapo uende kuomba idhini ofisi tatu tofauti, tena kwa jambo hilo hilo, ukiachilia mbali mamlaka zingie wanazohitaji kupitia. Huu ni woga tu hakuna jingine.
 
Back
Top Bottom