Dhamira njema ya Katiba Mpya ni kuwa na jopo jipya lisilohusisha Wabunge waliopo

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,057
Salaaam!

Kuhusu kuundwa katiba mpya serikali haina budi kutenda haki juu ya muundo wa jopo au kamati au bunge ambalo halitahusisha mbunge yeyote na wa chama chochote, katiba iundwe na wasiofungamana na siasa za uwakilishi wa kibunge na Baraza la wawakilishi.

Ni matumaini yetu ya kwamba bashasha hizi ziendane na uhalisia wa sheria, haki na weledi, nia njema na utashi wa vitendo.

Sijaona bado jambo la kufurahusha kufurahia aliyoysema Rais Hassan leo, kila alichokisema kiko ndani ya wajibu wake, na mengine ni sehemu ya Utamaduni wa kuchutama walipokosea, hana jipya lolote amejisahihisha kama mhimili.

Watanzania ni muhimu muanze na nia njema na yenye utashi wa kweli, ogopeni utashi usio na nia njema ndani yake.

Kimbunga alichokiwasha Rais Hassan leo ni kinyago atakachokiogopa yeye mwenyewe kwa maana kifua hicho hana.

Vyama vya upinzani nawasihi chukueni tahadhari huu ni wakati ambao vyama vya siasa na waandishi wataonja chungu ya vyombo vya Dola.

CCM ni waoga miaka yote. Level and fair political playing field hawaiwezi, msisahau kuhusu marekebisho ya kikatiba kwa haraka kuhusu muundo wa tume huru ya uchaguzi.

Wasalaam .

Wadiz ndani ya viunga vya siasa.
 
Back
Top Bottom