Dhamira ipi aliyonayo mzee nkoswe? Tamani kumfahamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhamira ipi aliyonayo mzee nkoswe? Tamani kumfahamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kasent, Jun 1, 2012.

 1. K

  Kasent Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DHAMIRA IPI * ALIYONAYO
  ?
  “MZEE NKOSWE”
  *
  *
  *
  TAMANI KUMFAHAMU
  MZEE NKOSWE……….
  *
  *
  1. SUMBAWANGA NA HARAKATI ZA SIASA
  -Sumbawanga ni miongoni mwa wilaya Kongwe ndani ya Taifa hili lenye utulivu,amani na mshikamano.Ni wilaya maarufu miongoni mwa wilaya nyingine katika nyanda za juu kusini, ambayo ni maaarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.
  * * Kwa yeyote aliyeifahamu sumbawanga kabla ya mwaka 2010 ni lazima akubaliane nami kuwa huu ni mji ambao umekuwa kwa kasi na umepata maendeleo ya kasi ya ajabu hasa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.Katika Nyanja nyingine mji huu pia umepata mabadiliko makubwa kama ifuatavyo:- *
  * * * Kisiasa- Sumbawanga ni mji uliokuwa kisiasa kwa hali ya pekee hasa kuanzia mwaka 2010 wakati wa kampeni.SIASA ILIYOAMBATANA na *Udini ,Chuki ,fitna, iliota mizizi kwa kasi ndani ya mji huu hali iliyopelekea *baadhi ya waumini wa * dini ya RC (Rhoman Catholic)kutengwa *katika shughuli za ibaada na baadhi ya watu waliokumbwa *na adha hii ya udini *na kutengwa majina yao tunayo.Siasa za namna hii hazifai kuigwa wala kurudiwa hata kidogo kwani hata waasisi wa Taifa hili walizipinga vikali na kulaani siasa za namna hii.
  * * *Mwalimu J.K Nyerere aliwahi kusema (Machi 3,1999) kabla ya kifo chake kua ……..”ukimuona sheikh au padre au mchungaji yeyote Yule anahubiri juu ya siasa ndani ya nyumba za ibada basi mjue mtu huyo amechanganyikiwa…..”
  Kwa maneno haya ya baba wa taifa ni wajibu wa kila mmoja hasa viongozi wa dini zote Tanzania kutafakari kwa *kina walifanya nini au walishiriki vipi katika masuala ya siasa ndani ya nyumba za ibaada na kisha wajiulize falsafa ya mwalimu J.K.Nyerere *inawabatiza wao kwa jina lipi na mfumo upi?
  Si rahisi *kukataa na ni vigumu kupinga kwamba ni wazi kabisa vuguvugu la siasa za chuki na udini ziliasisiwa na baadhi ya watu kwa sababu zao na si sababu zenye maslahi ya kitaifa .
  1.1 UPEKEE WA SIASA YA SUMBAWANGA MWAKA 2010
  Sumbawanga ni mji ambao ulishuhudia kutokea kwa siasa ya aina yake ambayo kama haitachunguzwa kwa umakini itaishia kujenga jamii yenye ubaguzi ,chuki ,fitna *na zaidi yenye kuigawa *jamii katika misingi ya dini,na hii ni dhambi *kubwa isoweza kufutika .Wengi watajiuliza ni mambo gani yanayofanya jamii iamini kua Sumbawanga iligubikwa na siasa ya kipekee ,Yako mambo mengi lakini *Baadhi ya mambo mazito yaliyojitokeza ni haya yafuatayo:-
   .Kwaya za kanisa kutunga nyimbo kwa ajili ya kumnadi mgombea :hili ni jambo la *kusikitisha ambapo kwaya ya kanisa iliamua kutunga nyimbo na kumnadi mgombea (X) hii ni ishara tosha kuwa kanisa hilo lilidhamiria kufanya siasa.
   .Matumizi ya vifaa vya utangazaji kutoka kanisa maarufu :na kwa yote haya, kila mja anaemgopa mungu atakubaliana na hoja kwamba siasa na nyumba za ibaada ilishamiri.
  *
  * * -Ni mengi ya kuorodhesha lakini hayo yanatosha ukiachilia mbali mahubiri na harakati nyingine nyingi ,Haitakuwa ajabu sana kuona kuwa watu watayapinga haya na kusema hayakuwapo lakini mioyo yao na Mungu wanayemuamini atawasuta ,imefika wakati ambapo wananchi tuamke na tupige vita mfumo huu wa siasa usio na tija na unaotuondolea umoja wetu ,na tukiuvunja umoja huu tujue kuwa historia itatuhukumu.
  Swali la Msingi
  * * * * * *Ni nani Muasisi na ni wepi waasisi wa aina hii ya siasa ndani ya mji wa sumbawanga ?
  Jibu
  Siku zote wapo watu ambao wana asili na *mienendo ya namna hii na wanaopenda * * * *kuwafanya watu wakakosa utu kwa mwamvuli wa Harakati.
  2.WANAHARAKATI NA HARAKATI ZAO SUMBAWANGA
  -Kipindi cha hivi karibuni wamezuka watu wajiitao wana harakati *bila kufasiri zaidi dhamira ya dhati ya harakati zao .Neno au jina *mwanaharakati ni pana sana na kila harakati ina malengo yake .”Kwa maana ya siasa Mwanaharakati “-ni mtu alie na dhamira ya dhati ya kufanya mabadiliko chanya ndani ya jamii lakini akiwa amepambwa na Sifa safi za wanaharakati miongoni mwa sifa hizo ni:-
   Dhamira ya dhati ya mabadiliko
   Utamaduni wa Harakati Chanya katika maisha yake.
  Ukichukua sifa hizo za mwanaharakati *na ukaanza kumvisha mwanaharakati mmoja mmoja ndani ya jimbo la Sumbawanga au Taifa utakuta walio wengi wamevaa viatu vikubwa kuliko miguu yao (oversize) na pia wanajivisha ngozi ya kondoo wakati miili yao na ngozi zao ni simba tena Hatari.
  Miongoni mwa wanaharakati wasio na dhamira ya dhati na waliotumia Ngozi ya Kondoo kujificha asili yao ni mzee *maaarufu “Mzee Nkoswe”.
  2.1. YA MZEE NKOSWE NA HARAKATI ZAKE
  Mzee Nkoswe ni mzee maarufu na ni miongoni mwa wanaharakati waliojitokeza *na kuongoza kundi la watu wengine wanaojiita wanaharakati pasipo *kutambua dhamira ya dhati ya harakati zao. Uanaharakati wa mzee huyu “MZEE NKOSWE” Unaleta mashaka na wasiwasi *na anasababisha maswali mengi miongoni mwa wanaotafakari kwa kina *na kujiuliza ni ipi dhamira yake .
  Nkoswe ni miongoni mwa wahubiri wanaohubiri juu ya yale wasiyoyatenda ,kukemea yale wanayoyatenda na kusahau ni wapi wametokea .Ukiitazama safari ya maisha ya mzee *huyu *utagundua *kua uanaharakati alionao sasa kupitia *CHADEMA ni uzushi ,uzandiki *na usaliti wa nafsi yake mwenyewena amesahau mengi anayoyaamini na kuyatenda.
  UZANDIKI wa Mzee Nkoswe unathibitishwa na haya aliyoyayatenda na anayoendelea kuyatenda .Uozo na uzandiki wa Mzee Nkoswe ni pamoja na haya yafuatayo:-
  *
  *
   KUTAIFISHA NG’OMBE ZILIZOCHANGWA KWAAJILIYA WAPIGANAJI WA VITA YA KAERA
  Mzee huyu akiwa na nafasi serikalini (Mkuu wa wilaya) alihamasisha wananchi kuchanga ng’ombe ili ziwasilishwe kwa wapignaji wa vita ya Kagera ili kuwapa nguvu lakini alichokifanya Ng’ombe zote alizichukua na kufungua zizi lake binafsi. Sasa tunachojiuliza uanaharakati upi alionao kwa hujuma hii kwa jamii na Taifa zima alioufanya? Ni imani kuwa anakumbuka haya na historia inamhukumu.
   KUJILIMBIKIZIA VIWANJA
  Wakati wa uongozi wake alihujumu jamii kwa kujilimbikizia viwanja vingi sana na kwaachia wananchi wakiwa na miliki ya viwanja vidogo vidogo *mithili ya vichochoro ,Hatimaye viwanja hivyo akaanza kuviuza na hadi sasa kipoa nachowauzia wazee wawili maarufu (majina yanahifadhiwa) ,Je ni dhamira ipi ya dhati aliyonayo?
   UONGOZI WAKE NI WA KIDIKITETA USIO NA MISINGI YA DEMOKRASIA
  Moja ya falsafa yake kubwa ni *matumizi ya nguvu badala ya demokrasia na atakumbukwa sana kwa ukatili wake alioufanya wakati wa uhujumu uchumi kwa kuwakamata watu wasio na hatia kupitia ushawishi wake ndani ya kamati ya ulinzi na usalama .Sasa basi kwa uongozi wa namna hii ni Demokrasia gani anayoihubiri katika majukwaa ya Chadema ? Huu ni uzandiki na usaliti wa Nafsi yake.
   KUNG’ANG’ANIA MADARAKA
  Siku zote popote alipo katika maisha yake Mzee Nkoswe ni mtu anaetaka Uongozi kila kukicha *bila uongozi hajaona ladha *ya maisha na pasipo na uongozi kwake ni sumu.Kwa kuthibitisha hili akiwa ndani ya CHADEMA tayari ameanza kuzunguka kwa ajili ya Kufungua Matawi,Swali la kujiuliza ni:
  • Je Nkoswe anafungua Matawi kama nani?
  • Na katiba ya chama *husika * inasemaje?
  • -Je ni wazi kuwa CHADEMA haina mfumo sahihi hadi kila anaekurupuka anakua ni kiongozi na kufanya shughuli za chama kama kiongozi?
  Kwa dalili hii Dhamira ya dhati ya Nkoswe ni uongozi ndani ya Chama na si dhamira ya dhati ya mabadiliko.
   KUFANYA MAAMUZI SEHEMU ZA POMBE (BAR)
  Katika uongozi wake alitumia sana mfumo wa matumizi ya sehemu za bar kutolea fikra au maamuzi ,Mzee huyu alikuwa akitumia bar iliyokua ikiitwa LANCASTER BAR huku akijistarehesha na mifumo kama hii si picha ya dhamira ya msingi ya mabadiliko bali ni uzandiki.
   .NI CHANZO CHA MIGOGORO NDANI YA CHAMA NA JAMII NZIMA
  Mzandiki Huyu ni muasisi wa migogoro na uhasama katika mfumo wa siasa ,ikumbukwe kwamba yeye alikua chanzo cha migogogro kwa chama alichokua na ni muasisi wa majungu kwa kifupi ni kiongozi asiyethamini amani katika harakati zake ,na ni muasisi mkubwa wa siasa za husuda ,chuki ,uhasama *katika uchaguzi wa mwaka 2010.Ni imani yetu kubwa falsafa isemayo “Jasiri Haachi Asili”itatimia na atakuwa mwenye kuendeleza mifarakano na huko alikoenda CHADEMA ijiandae kwa migogoro ,chuki na ung’ang’anizi wa madaraka.
  * *Kwa sifa hizi alizonazo mtu huyu ,ni wazi kuwa dhamira yake na misimamo yake ni ya kuipotosha jamii na analenga kutumia mwamvuli wa uanaharakati kuyaficha mengi aliyonayo .
  3. MWISHO
  -Ni wajibu wa kila mwanajamii kuasisi umoja na mshikamano tulioachiwa na waasisi waTaifa hili lakini pia suala la uanahrakati liendane na sifa anuai zinazolenga kuleta mabadiliko ndani ya jamii bila kuharibu umoja wetu na mshikamano lakini pia Dhamira ya dhati ya Nafsi Zetu.Kwa *haya na mengi juu ya uzandiki wa Mzee Nkoswe Tunajiuliza *Ni Dhamira ipi Aliyonayo Mzee Nkoswe Sumbawanga?
  *
   
 2. U

  UKUMUZI New Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KASENTI, Kasenti! KaSenti!
  Mbona Umekosa Mantiki katika thread yako?
  Unaonekana una jambo kichwani lakini bado haujafahamu namna ya kuliwakilisha katika Chombo kikubwa cha Umma kama hiki.
  SIKU NYINGINE FIKIRIA kabla HAUJAAMUA KUANDIKA. Na endapo una matatizo yako binafsi yamalize kwanza ndo Uje katika Mtandao mkubwa wa Kijamii kama huu.

  NIKUJIBU JAPO KWA UFUPI:
  Mimi nimezaliwa Sumbawanga, si ajabu wewe ukiwa mdogo sana, maana Mwaka 1972 nilikuwa darasa la nane Middle School Mwazye, huko nilipewa cheo cha Umonita darasani; cheo hiki kilinifurahisha na kunipa heshima sana. Siku moja nikiwa natoka darasani, nilitereza mlangoni nikadondoka: Wenzangu (wana darasa wenzangu) walinicheka kwa kile kilichonitokea: Kwa hasira ukijulisha na Cheo nilichokuwa nacho, na Heshima niliyokuwa ninaitegemea kupewa na wanadarasa wale, niliamua kupitisha fimbo kwa wote, jambo lililoleta kizaa kikubwa pale darasani, mwisho Mwalimu wa darasa aliitwa akaelezwa yaliyojiri, na akatoa Uamuzi pale pale, MIMI KUVULIWA CHEO CHANGU.

  Hayo machache, yanaweza kukusaidia KASENTI, pengine ni bora kunyamaza ukajinusuru na Karandinga la wenye ubongo mkubwa; mawazo yako ni mepesi mno yaliyojaa hisia za hasira, unyong'onyevu, Uoga na Umimi. Ungepata bahati ya kulinganisha UPEVU, fikra na Uhalisia wa mambo nachelea kusema pengine usingediriki kujitokea katika mtandao huu wa Great Thinkers! (Brain Tankers)
  KUHUSU SIASA ZA SUMBAWANGA:
  Tumeona siasa za kimapinduzi zikiendeshwa popote katika nchi hii Arumeru, Arusha, Mbeya, Sumbawanga na mahali pengine, siasa hizi zimekuja katika katika wakati ambapo, mangamuzi na ukomavu wa Wananchi unaongozwa na nguvu ya Utashi wa kimawazo na fikra. Kila mtu anahoji nalipa kodi hii itanisadia nini? napiga makofi kwa kiongozi huyu ili iwe nini? wachache wa namna yako wanaweza wasijihoji KWA NINI? "wachache si wengi" wachache wasioweza kujiuliza je nipige kura yangu kwa mtu asiye na sifa za kuniwakilisha katika chombo kikubwa cha kudai haki na kutunga sheria? wachache wasioweza kujiuliza je, huyu anaweza kutafsiri ninachofikiri na kukielezea kikaeleweka?
  Sumbawanga, mtu haambiwi tazama. Harakati za kimapinduzi, zenye lengo, dhamira na Nguvu ya kimshikamano, haipingiki. Leo Umma wote "kasoro wewe Kasenti" umeungana na kudai kwa dhati KILE KINACHOHITAJIKA KWA UMMA kwa njia zote. Kwa MAPINDUZI yanayohitaji kujimwagia mafuta ya moto, kuvua ngozi nyeusi na kuvaa ngozi nyeupe nk. Kaseti" shuleni watoto wa Sumbawanga wanaimba katika mchakamchaka wakiamasisha mapinduzi, makusanyiko mbalimbali ya vijana, misiba, na sherehe zote, utayakuta mazungumzo ya kuhamasisha mabadiliko.
  Kasenti" Kamanda haendi vitani bila kutumwa! hamasa zote hizo hazipo bila makamanda wakuu? Wanaharakati uliowataja, ndiyo sababu ya matokeo angavu, yaliyotukuka na yatakayoenziwa katika mji wa Sumbawanga. Historia isiyofutika IMEANDIKWA. Nimefurahi thread yako imemtaja moja kati ya Makamanda wa mstari wa mbele katika Mapinduzi haya ndugu Mheshimiwa sana Kepteni, Muhasisi, Honorable ZENO NKOSWE, Mzee wa siku nyingi, Hekima iliyotukuka, Staa isiyoisha! Baba kipenzi cha wengi Sumbawanga!!!!! peta peta Baba ZENO NKOSWE waumie wenyewe.
  "Kasenti" unajua kwa nini nimempamba sana huyu mzee ni kwa sababu ya fide el fidius motz kilatini: jembe halitakiwi kuukataa mpini endapo unataka kupata muhindi.
  Huwezi kuyakubali mapinduzi ukamkataa mwenye kuleta mapinduzi, "Amanda Aweitu" Ndivyo Mandela alivyoongoza mapinduzi huko kusini, mapinduzi na mandela ni kitu kimoja, "filde flelimo" ni wito wa Samora Masheli Msumbiji, ni sawa na MTU KWANZA .............ya Zeno Nkoswe!
  Natamani kukueleza mengi ndugu yangu "KASENTI" tusiwachoshe wasomaji kwa ubishi wa bure, na kutumia mtandao wa umma bila faida.
  LA MWISHO: Waswahihili husema WAKIKUSHINDA, Ungana nao! Utapasuka bure endapo utaendelea kupambana na Upepo, na Asiye kinyume chetu YU upande wetu, kama ukiona U kinyume usijitambulishe, gugumia kitandani mwako, maana wakikutambua watakumaliza. Na UPEPO HUVUMA UTAKAKO, "rafiki yangu Kasenti" ZUIA HUO UPEPO UONE.
   
 3. U

  UKUMUZI New Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Kasenti" SEMA PEOPLES!!!!!!! POWER!!!!!!!
  Najua huwezi kusema kwa sababu umejaa magamba! wenye magwanda tu ndo wanaweza kusema Peoples!!!! Power!!!!
  Mwito wa CHADEMA sasa hivi ni kila mtu alipo, aanze kufungua Matawi HATUSUBIRI TARATIBU hizo taratibu zitafuatwa baadaye!!! Au nikupe Namba ya simu ya Kiongozi mkuu wa Chadema anayeorodhesha Matawi? najua wewe ni Gamba utaitumia vibaya!!!
  Yeyote, Sio mzee Zeno Nkoswe tu, hata mimi ninapita vijijini kwetu Kapozwa na Kaluko kufungua matawi!!! tuite majina yoyote utakayo, lakini kazi ya the Peoples!!!!! inatisha, Magamba kwen'g sh'ria mbali!!!!

  Ungepata Fursa ya kusikiliza Mkutano mkubwa Uliofanyika Jangwani Dar Es salaam, ungesikia wito, huu. JAMANI SOTE POPOTE, tufungue MATAWI, kila mmoja afungue 10, 100, 1000, mpaka magamba yapasuke!!! Na Sumbawanga, MZEE Nkoswe kaza Uzi, mimi nikifungua matano wewe 5000, nikifungua 10, wewe 10,000 mpaka MAGAMBA yakupigie magoti, yakikuhitaji tena YAKATAE, yaambie YA KALE YAMEPITA Yamekuwa MAPYA. "wakati mwingine inafaa ukikasirika sana utafakari usije ukajinyonga, Kasenti, usijinyonge maana the PEOPLESSSSSS POWER mwendo mdundo mpaka IKULU 2015 bila UBISHIIIIIIIIII! Pole ""Kasenti wa Magamba""""
   
 4. F

  FUPITAM Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mnajuana ninyi,.......msitusumbue...
   
 5. P

  Ptz JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Mtoa mada kajawa na majungu, ubinafsi na fitina za uke wenza! Umetumwa na Aishi nini? Njaa mbaya sana, ulikuwa wapi Mzee Nkoswe alipokuwa ccm mbona hukusema? Leo kajivua gamba unawashwa washwa! Peoplezii, ccm ishakufa Sumbawanga na siku ya alhamis tar 7 mwezi huu June makamanda wa CDM wakiongozwa na kamanda wa anga sauti la zeze kamanda Mbowe!fuatavyo:- *
  * * * Kisiasa- Sumbawanga ni mji uliokuwa kisiasa kwa hali ya pekee hasa kuanzia mwaka 2010 wakati wa kampeni.SIASA ILIYOAMBATANA na *Udini ,Chuki ,fitna, iliota mizizi kwa kasi ndani ya mji huu hali iliyopelekea *baadhi ya waumini wa * dini ya RC (Rhoman Catholic)kutengwa *katika shughuli za ibaada na baadhi ya watu waliokumbwa *na adha hii ya udini *na kutengwa majina yao tunayo.Siasa za namna hii hazifai kuigwa wala kurudiwa hata kidogo kwani hata waasisi wa Taifa hili walizipinga vikali na kulaani siasa za namna hii.
  * * *Mwalimu J.K Nyerere aliwahi kusema (Machi 3,1999) kabla ya kifo chake kua ........"ukimuona sheikh au padre au mchungaji yeyote Yule anahubiri juu ya siasa ndani ya nyumba za ibada basi mjue mtu huyo amechanganyikiwa....."
  Kwa maneno haya ya baba wa taifa ni wajibu wa kila mmoja hasa viongozi wa dini zote Tanzania kutafakari kwa *kina walifanya nini au walishiriki vipi katika masuala ya siasa ndani ya nyumba za ibaada na kisha wajiulize falsafa ya mwalimu J.K.Nyerere *inawabatiza wao kwa jina lipi na mfumo upi?
  Si rahisi *kukataa na ni vigumu kupinga kwamba ni wazi kabisa vuguvugu la siasa za chuki na udini ziliasisiwa na baadhi ya watu kwa sababu zao na si sababu zenye maslahi ya kitaifa .
  1.1 UPEKEE WA SIASA YA SUMBAWANGA MWAKA 2010
  Sumbawanga ni mji ambao ulishuhudia kutokea kwa siasa ya aina yake ambayo kama haitachunguzwa kwa umakini itaishia kujenga jamii yenye ubaguzi ,chuki ,fitna *na zaidi yenye kuigawa *jamii katika misingi ya dini,na hii ni dhambi *kubwa isoweza kufutika .Wengi watajiuliza ni mambo gani yanayofanya jamii iamini kua Sumbawanga iligubikwa na siasa ya kipekee ,Yako mambo mengi lakini *Baadhi ya mambo mazito yaliyojitokeza ni haya yafuatayo:-
  ? .Kwaya za kanisa kutunga nyimbo kwa ajili ya kumnadi mgombea :hili ni jambo la *kusikitisha ambapo kwaya ya kanisa iliamua kutunga nyimbo na kumnadi mgombea (X) hii ni ishara tosha kuwa kanisa hilo lilidhamiria kufanya siasa.
  ? .Matumizi ya vifaa vya utangazaji kutoka kanisa maarufu :na kwa yote haya, kila mja anaemgopa mungu atakubaliana na hoja kwamba siasa na nyumba za ibaada ilishamiri.
  *
  * * -Ni mengi ya kuorodhesha lakini hayo yanatosha ukiachilia mbali mahubiri na harakati nyingine nyingi ,Haitakuwa ajabu sana kuona kuwa watu watayapinga haya na kusema hayakuwapo lakini mioyo yao na Mungu wanayemuamini atawasuta ,imefika wakati ambapo wananchi tuamke na tupige vita mfumo huu wa siasa usio na tija na unaotuondolea umoja wetu ,na tukiuvunja umoja huu tujue kuwa historia itatuhukumu.
  Swali la Msingi
  * * * * * *Ni nani Muasisi na ni wepi waasisi wa aina hii ya siasa ndani ya mji wa sumbawanga ?
  Jibu
  Siku zote wapo watu ambao wana asili na *mienendo ya namna hii na wanaopenda * * * *kuwafanya watu wakakosa utu kwa mwamvuli wa Harakati.
  2.WANAHARAKATI NA HARAKATI ZAO SUMBAWANGA
  -Kipindi cha hivi karibuni wamezuka watu wajiitao wana harakati *bila kufasiri zaidi dhamira ya dhati ya harakati zao .Neno au jina *mwanaharakati ni pana sana na kila harakati ina malengo yake ."Kwa maana ya siasa Mwanaharakati "-ni mtu alie na dhamira ya dhati ya kufanya mabadiliko chanya ndani ya jamii lakini akiwa amepambwa na Sifa safi za wanaharakati miongoni mwa sifa hizo ni:-
  ? Dhamira ya dhati ya mabadiliko
  ? Utamaduni wa Harakati Chanya katika maisha yake.
  Ukichukua sifa hizo za mwanaharakati *na ukaanza kumvisha mwanaharakati mmoja mmoja ndani ya jimbo la Sumbawanga au Taifa utakuta walio wengi wamevaa viatu vikubwa kuliko miguu yao (oversize) na pia wanajivisha ngozi ya kondoo wakati miili yao na ngozi zao ni simba tena Hatari.
  Miongoni mwa wanaharakati wasio na dhamira ya dhati na waliotumia Ngozi ya Kondoo kujificha asili yao ni mzee *maaarufu "Mzee Nkoswe".
  2.1. YA MZEE NKOSWE NA HARAKATI ZAKE
  Mzee Nkoswe ni mzee maarufu na ni miongoni mwa wanaharakati waliojitokeza *na kuongoza kundi la watu wengine wanaojiita wanaharakati pasipo *kutambua dhamira ya dhati ya harakati zao. Uanaharakati wa mzee huyu "MZEE NKOSWE" Unaleta mashaka na wasiwasi *na anasababisha maswali mengi miongoni mwa wanaotafakari kwa kina *na kujiuliza ni ipi dhamira yake .
  Nkoswe ni miongoni mwa wahubiri wanaohubiri juu ya yale wasiyoyatenda ,kukemea yale wanayoyatenda na kusahau ni wapi wametokea .Ukiitazama safari ya maisha ya mzee *huyu *utagundua *kua uanaharakati alionao sasa kup
   
 6. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ptz

  Nimekuona hapa, na kwa kuwa location yako ni huko Sumbawanga utalimaliza jambo hili kwa umahiri mkubwa. Aidha ukishindwa kumteketeza tuwasiliane nifungulie B-52 ili kelele ziishe.
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Aeshi kakutuma?
   
Loading...