DHAMIRA HURU: CCM wanaweza kulazimisha sheria; Hawawezi kulazimisha Katiba bila kupingwa!

Pasco,
Kwa kuelewa kwangu mimi Chadema hawakuingia uwanjani kucheza isipokuwa walihudhuria mkusanyiko tayari kucheza ikiwa sheria kadhaa zitarekebishwa. Hotuba ya Lissu ilikuwa ni kueleza kwanza sababu ya wao kutshiriki wakijua fika kwamba CCM atapewa mpini na wao washike kwenye makali.. Tatizo limekuja ya kwamba CCM hawataki kubadilishwa kwa sheria, ama kushika upande wa makali wala kupokonywa mpini. Na Chadema wakasema kama mchezo wenyewe ndio huu sisi hatutaweza kushiriki - Kabla kabisa ya kipenga kupigwa..

Kwa hiyo kutumia kanuni ya 86 bado utarudi kesho kufikia kuitoa hiyo hotuba na kueleza kinachokufanya usitake kushiriki siku mtakapo rudi bungeni na yatakayo fuata ni sawa na yaliyotokea jana. Kwa hiyo badala ya kutokea haya bunge lijalo imetokea leo..Sijui kama umenielewa ama naomba msaada wako ktk hili maanake sielewi Chadema wangeweza vipi kubadilisha rules za game ambazo tayari sheria zinampa mpini - a Home team..
 
Nimesema, na nasema tena, naiunga mkono 'walkout' ya Chadema kama ishara ya protest dhidi ya kuburuzwa, lakini siungi mkono kuisusa hoja nzima at its totality, kwasababu, kupitia kanuni, Chadema had a chance ya kuisimamisha hoja nzima nzima, they lost that one and only chance kuisusa kabisa hoja yote ni another loss!..

CDM wangebaki unamaamini wangeweza kuwashawishi wabunge zaidi ya 300 wa CCM na CCM B wakubali hoja ya kusomwa muswada mara ya kwanza? Mkuu sidhani kama upo serious kwa hili. Na upo huko unaona wabunge hao zaidi ya 300 wanapo acha muswada wa katiba na kujadili watu na CDM ni wabunge wawili tu ndio angalai wamejikita kwenye muswada huo.
 
Mkuu Pasco, ungewapa CDM hiyo nondo ili iwasaidie, kwa kukaa kimya halafu unakuja kuongea afterwards sijui una maana gani.
Chesty, Kanuni ndio msahafu wao, Chadema kama chama makini, they should have known better!.

Ila pia kwenye timu ya Chadema iliyomu bungeni, kuna ma 'much know' kibao, kuna siku niliwaambia 'hawajajipanga', walinishukia kisawasawa, sasa ndio ningeweza kuwaelimisha kanuni?.
 
Pasco,
Kwa kuelewa kwangu mimi Chadema hawakuingia uwanjani kucheza isipokuwa walihudhuria mkusanyiko tayari kucheza ikiwa sheria kadhaa zitarekebishwa. Hotuba ya Lissu ilikuwa ni kueleza kwanza sababu ya wao kutshiriki wakijua fika kwamba CCM atapewa mpini na wao washike kwenye makali.. Tatizo limekuja ya kwamba CCM hawataki kubadilishwa kwa sheria, ama kushika upande wa makali wala kupokonywa mpini. Na Chadema wakasema kama mchezo wenyewe ndio huu sisi hatutaweza kushiriki - Kabla kabisa ya kipenga kupigwa..

Kwa hiyo kutumia kanuni ya 86 bado utarudi kesho kufikia kuitoa hiyo hotuba na kueleza kinachokufanya usitake kushiriki siku mtakapo rudi bungeni na yatakayo fuata ni sawa na yaliyotokea jana. Kwa hiyo badala ya kutokea haya bunge lijalo imetokea leo..Sijui kama umenielewa ama naomba msaada wako ktk hili maanake sielewi Chadema wangeweza vipi kubadilisha rules za game ambazo tayari sheria zinampa mpini - a Home team..

Mkuu Mkandara,

Hii ndio kanuni ya 86

86.-
(3) Haitakuwa halali katika hatua hii kuleta hoja ya kufanya
mabadiliko katika hoja isipokuwa tu kwamba:-
(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza
kutolewa kwa kusema:
"Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu
Kusomwa
Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….", na hapo
sababu za kupinga Muswada Kusomwa Mara ya
Pili zitatajwa kwa ukamilifu.

Hayo maneno kwenye bold ndio Lissu alitakiwa ayaseme na kutoa sababu. Hakutakiwa hata kutoa ile hotuba ya kambi ya upinzani.

Kwa kutamka maneno hayo na kutoa sababu, muswada ungesimamishwa!

CDM wangebaki unamaamini wangeweza kuwashawishi wabunge zaidi ya 300 wa CCM na CCM B wakubali hoja ya kusomwa muswada mara ya kwanza? Mkuu sidhani kama upo serious kwa hili. Na upo huko unaona wabunge hao zaidi ya 300 wanapo acha muswada wa katiba na kujadili watu na CDM ni wabunge wawili tu ndio angalai wamejikita kwenye muswada huo.
Fidel80, kanuni ni rules of the game,

86.-
(3) Haitakuwa halali katika hatua hii kuleta hoja ya kufanya
mabadiliko katika hoja isipokuwa tu kwamba:-
(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza
kutolewa kwa kusema:
"Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu
Kusomwa
Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….", na hapo
sababu za kupinga Muswada Kusomwa Mara ya
Pili zitatajwa kwa ukamilifu.

Hayo maneno kwenye bold ndio Lissu alitakiwa ayaseme na kutoa sababu. Hakutakiwa hata kutoa ile hotuba ya kambi ya upinzani.

Kwa kutamka maneno hayo na kutoa sababu, muswada ungesimamishwa! haijalishi CCM wako wangapi, muswada ungesimamishwa na hoja za kuupinga zingesikilizwa, kama ni kweli muswada ule ni mpya na sio ule wa awali, Chade ma wangeshinda
 
Labda mimi ndio sijui utaratibu wa Bunge na sheria zake lakini nakumbuka muswada huu ulikwisha letwa Bungeni na ukatolewa makosa na mapendekezo yake. Upande wa Upinzani walieleza wazi sehemu zinazotakiwa kufanyika marekebisho na mapendekezo yao lakini badala yake Muswada umerudi ukiwa umebadilishwa lugha tu lakini yote yaliyokataliwa toka mwanzo yalirudi kama yalivyo..Ukiendelea mbele yaani 4 hadi 9 inakupa picha zaidi usikomee namba 3 - maanake tumefikia hatua ya kutaka kutunga sheria wakati huko nyuma hatukufuata utaratibu!.

Sasa nenda kanuni ya 87 utaona inavyosema kuhusu kurejeshwa kwa muswada ktk kamati, nadhani kwa msingi huu ndio Lissu aliwakilisha..
 
Kwa kutamka maneno hayo na kutoa sababu, muswada ungesimamishwa! haijalishi CCM wako wangapi, muswada ungesimamishwa na hoja za kuupinga zingesikilizwa, kama ni kweli muswada ule ni mpya na sio ule wa awali, Chade ma wangeshinda

Pasco, sehemu inayofuatia hapo chini inasema:

(4) Iwapo hoja itatolewa chini ya fasili ya 3(a) na (b) ya Kanuni hii, Spika atalihoji Bunge ili kufikia uamuzi.

Kwanini unafikiria kuwa kwa kusema tu maneno hayo ya (3) basi mswada utasitishwa automatically?
 
this was the great class 4 me as lawyer and an activist, first i was delighted with Posco arguement on why he say CDM dd a horable mistake in walking out and leave th game to CCM but also i was thrired by his opponent, anyway that is not what i want to say today is that ok! Let assume or agree as Pasco has argued that CDM made one mistake but the only one who could save them, but let it b CDM TLP or CCM A and B we the people of Tanzania we are the one who put them there to work 4 us, the constitution wl not only bind CCM or CDM bt we the people and by the people i mean all of us from all group, so if our servand have not done the work we expected of them then let do it ourself and there are many way we can do it either the easy way or the hard way, the easy way we can just air our views and wish that they listen however if they dnt listen do it the hard way by demonstration, riotes and boycot! We are the people, we are the power.
 
Mkuu mwanakijiji nakubaliana na wewe 100%. CCM haina dhamira wala haidhamirii kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa huru kwa kupata katiba inayosimamia uhuru huo. Kinachofanyika sasa kama ambavyo walivyofanya 1992 kukubali mfumo wa vyama vingi ambao mpaka leo kwao wao ni kama haupo, ni ku torpedo pressure from foreign donors kuwa CCM inasimamia reform, kitu ambacho hata Mkapa alikisema lingekuwa ni kosa kuona linasimamiwa na wapinzani maana litazamaa matunda ambayo ni neema kwa Tanzania ila ni angamizo kwa mustakabali wa CCM.

CCM na wabunge wake wamekaa kama chama na kuweka mbele masilahi ya chama huku wakijaribu kuwaridhisha wafadhili kuwa wanasimamia mageuzi ya katiba. Katiba ya Tanzania haiwezi kupatikana wakati CCM ikiwa madarakani hata kidogo, kuna ushahidi tosha kuanzia Kenya, Ghana et al. Katiba ya kweli itapatikana pale wale waliopo CCM kwa sasa wataakapoona kuwa hawana cha kupoteza.

Njia pekee ni kuwaacha wacheze ngoma yao, sisi tuwe watazamaji tu, tukiingia kucheza na sisi basi tumeipatia uhalali ngoma hiyo mbele ya jumuiya za kimaifa. International community will not recognise this move if it leaves part of Tanzania out of the matrix box. Ndiyo maana najiuliza hivi CCM kupitia kina Membe walipokuwa wakisisitiza kuwa serikali ya mpito Libya iwajumuishe walibya wote hata wale waliokuwa ndani ya gaddafi katika kupata national consesus walikuwa wanamaanisha nini hasa?. Ni kwamba wanaimba wimbo wasioujua?. Charity begins at home, CCM inafanya nini kutuunganisha watanzania katika huu mchakato muhimu?.

They are wrong! they are wrong! and history will judge them that they are wrong!.

NIMEKUSOMA VEMA lakini siamini kwamba wabunge wa CCM wanatetea maslahi ya chama lah!!! Wajanja wachache ambao hawajui mustakabali wa maisha yao pindi nchi yetu ikiongozwa na katiba ya Wanachi ambayo itatoa uhuru wa maamuzi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka tume huru ya uchaguzi na mazingira huru kwa uchaguzi na itokee chama pinzani kikashinda hao ndiyo hasaa ambao kwa ujanja ujanja na kutumia baadhi ya wasomi wetu uchwara wamewaaminisha wengi wa wabunge wa CCM kwamba kutetea upuuzi ni utetezi wa CHAMA.
Ni janja ya mafisadi ambao wanaogopa NURU wangependa GIZA liendelee hao hasa ndo wameprogramme mawazo ya wabunge wa CCM hadi wamebaki mazezeta hawawezi hata kutafakari mstakabali wa taifa letu,wamebakia kuunga mkonokila uppuzi kwa jina la utetezi wa CHAMA.
Busara ya kawaida inasema ukikuta palipo watu wengi wanakubaliana jambo pasipo na kupinga,BASI wengi wao hawafikiri,hivyo ndivyo ilivyo kwa Wabunge wa CCM.
 
Hebu tizama habari hii! Hivi huyu kijana ni kweli huwa anasikiliza yale anayoyaongea yeye mwenyewe? Well, CDM inafadhiliwa na wengi pengine hata mimi katika kusimamia ukweli (facts) ambazo zitaishi milele pengine, wasiwasi wangu ni kama kweli huyu mtumwa ano uwzo wowote wa kujadili lolote! objectivity! Mshangao ni kwamba hao wana-CCM je wameelewa na kwa 'dhamira' zao wanakubaliana na huo mwelekeo! juzi juzi mwingine alidai CDM ina fadhiliwa na Conservative party ya Uingereza, likini pivoting kwamba Cameron ametetea ushoga na ndiyo mwenyekiti wa hicho chama, kama uhalali wa haki ya mwenye kuelewa kupewa nafasi ingekuwa bado inatawala ombaomba huyu sijui angekuwa wapi! Tuendelee na mjadala!

Habari za Kitaifa

Mbunge- Ujerumani inafadhili wapinzani
Imeandikwa na Maulid Ahmed, Dodoma; Tarehe: 17th November 2011 @ 19:59 Imesomwa na watu: 1353; Jumla ya maoni: 4

UJERUMANI imetajwa bungeni kukitumia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupinga kusomwa kwa mara ya pili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

Tuhuma hizo zilitolewa na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), wakati akichangia muswada huo uliojadiliwa kwa siku ya tatu sasa na unaotarajiwa kuhitimishwa leo.

Wakati Lusinde akitoa tuhuma hizo, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amewataka Watanzania kutatua matatizo yao bila ya kukimbilia kwa mabalozi na kuonya kuwa vinginevyo watakuwa wakiendekeza ukoloni mamboleo.

Lusinde katika madai hayo, aliweka bayana kuwa Ujerumani imewachochea wapinzani na wanaharakati kufanya vurugu na imewaahidi fedha ikiwa watafanikisha muswada huo usomwe mara ya kwanza bungeni.

“Ujerumani wanawasaidia hawa wanaopinga muswada huu, wamewaahidi fedha kama muswada utasomwa kwa mara ya kwanza…kuna watu wanafanya udalali wa kisiasa hapa,” alisema mwanasiasa huyo kijana.

Katika mjadala wa muswada, Chadema na NCCR Mageuzi wamesusia majadiliano ya muswada huo baada ya kuwasilisha maoni ya Kamati yao ya Upinzani iliyowasilishwa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu.

Akijibu tuhuma hizo, Katibu wa Wabunge wa Chadema, John Mnyika alisema; “hizo ni taarifa za uzushi, propaganda zenye lengo la kuwapotosha Watanzania, sisi tunapinga kusomwa mara ya pili kwa sababu wananchi wanapinga hivyo.”

Gazeti hili lilipomuuliza Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) kuhusu tuhuma hizo zilizotolewa na Lusinde, alisema taarifa hizo za kuahidiwa fedha si za kweli.

“Mataifa ya Ulaya ndiyo yanafaidika na sera za CCM kuliko upinzani, haiwezekani leo watufadhili sisi kuiondoa Serikali ya CCM inayowasaidia wao kama kwenye madini,” alidai Kafulila na kuungwa mkono na mwenzake wa Kasulu Mjini, Moses Machali aliyesema; “Lusinde ni mpigadebe wa CCM, hatunyimi usingizi.”

Lusinde pia alisema kutokana na kauli za Chadema, inaonesha Wazanzibari walioko kwenye chama hicho wanajipendekeza na wanadharauliwa na hawatakiwi.

Kuhusu kauli ya Chadema kuwa Rais wa sasa ni wa kifalme, Lusinde alisema: “Chadema ni chama cha wabinafsi na wanaweka viongozi kwa unasaba.

“Angalieni humu bungeni kuna mtu na mkwewe na mwanawe, yupo mwingine na dada yake na yupo aliyemuweka mzazi mwenzake, sasa nani anayefuata uongozi wa kifalme, sisi au wao?” alihoji.

Kwa upande wa Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza (CCM), alishauri muswada huo uondoe kipengele cha kuundwa kwa Bunge la Katiba na ibaki Tume ya kukusanya maoni pekee ili kupunguza gharama kubwa pamoja na kuepusha usumbufu wa kisiasa.

“Katika demokrasia kuna uwakilishi wa moja kwa moja na kupitia uwakilishi sasa tume ingechukua maoni na kuandaa rasimu na kuirudisha kwa wananchi. Kuondolewe Bunge la Katiba ambalo linakuwa la uwakilishi, duniani kote wanachagua njia moja, lakini sisi tunataka kuchukua njia zote mbili hii haina maana,” alisema.

Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alipendekeza jina la muswada libadilishwe kutoka Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuwa Muswada wa Kutunga Katiba mpya, kutokana na kwamba Katiba inaandikwa upya na haifanyiwi mabadiliko ya vipengele vya sasa.

Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abdalla (CUF), alitaka Watanzania waliopo nje waangaliwe namna ya kuwasilisha maoni yao kwa Tume itakayoundwa kukusanya maoni.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Clara Mwatuka (CUF), aliwataka wabunge wenzake kuachana na kujadili kauli ya Chadema na badala yake kuujadili muswada huo.

“Tusiwapuuze (Chadema) katika waliyosema yapo mengine machache mazuri tuyachukue kuyafanyia kazi,” alisema Mwatuka.

Waziri Mkuu mstafu, Warioba, alisema Watanzania lazima wajitathimini wenyewe kujiletea maendeleo yao na kutatua matatizo bila ya kukimbilia kwa mabalozi na kuonya kuwa vinginevyo watakuwa wakiendekeza ukoloni mamboleo.

Alisema hayo jana katika warsha ya kumuenzi Baba wa Taifa, Malimu Julius Nyerere, iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro inayojulikana kama ‘Mzumbe Nyerere Day’.

“Inasikitisha kuona tumepoteza maadili na nidhamu yetu ambayo Baba wa Taifa alituachia kama tunu na sasa mtu anatafuta uongozi ili kujipatia mali,” alisema Jaji Warioba.

Alisema wanasiasa wana wajibu wa kukaa pamoja na kuondoa tofauti zinazoendelea hivi sasa nchini, ili kutoa fursa kwa Taifa kufanya shughuli zake.

Warioba alisema siku hizi hajui nchi inakwenda wapi kwa sababu watu wamepoteza imani ya nchi na kila mtu analalamika, kiongozi analalamika na wananchi wanalalamika.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa alisema chuo chake kinaandaa kila mwaka kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya ili yaweze kukumbukwa na vizazi vya sasa na vya badaye na kuwa chachu ya maendeleo.

“Leo hii ni siku ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye alitumikia Taifa kwa uadilifu na alipenda Taifa lake liwe na wasomi wa ngazi mbalimbali ikiwemo ya elimu ya juu ili kuwa nguzo ya maendeleo ya nchi,” alisema Profesa Kuzilwa.
 
Asante, Mzee Mwanakijiji kwa hili, ila mimi naomba kutofautiana na wewe, na msimamo wa Chadema.

Wakati wa kutangaza matokeo ya urais, mimi binafsi nilikuwepo pale ukumbini, Chadema walisusa, nilitofautiana nao na nikasema humu kuwa hiyo ni golden opportunity ya kuiambia dunia kuwa uchaguzi wetu haukuwa huru na wa haki, you just tell it infrot of their faces, mpaka CNN, BBC na vyombo vya habari vya kimataifa vilikuwepo. Nilishambuliwa sana, ila nilisimama niliposimama.

Waliposusio hatuba ya rais pale bungeni Dodoma, pia nilikuwepo, nilisema tena it was not right na tulipofanya mjadala wa kumtambua rais au kutomtambua, pia nilisema, its a waste, kutomtambua kwa kauli na kumtambua kwa vitendo. Rais ana axist in real man hivyo umtambue usimtambue anabaki ni rais na yupo, hivyo kutomtambua ni kujidanyanya.

Nikimalizia hili la juzi, kwanza Lissu ni school mate wangu pale Ilburu, hivyo namfahamu fika, pili tulikuja kukutana nae Atlanta akiwa mwana harakati wa LEAT, hotuba yake ilikuwa na lots of flaws, kwa vile yeye ndie waziri kivuli wa sheria, Chadema walimwachia afanye kila kitu kwenye hotuba ile, laiti kama ingepitiwa na wabunge wengine wa Chadema, makini zaidi ya Lissu, wangekuja bna hotuba nyingine bora zaidi.

Naunga mkono walkout kama ishara ya protest lakini siungi mkono kuususia mjadala mzima bungeni unaomalizika leo. Japo Chadema inao wanasheria makini, lakini ni bure kabisa, wameshindwa kutumia upportunities za kuuzuia uwasilishwaji wa muswada huo kwa mara ya pili ambazo ziko proivided for na kanuni, hivyo kupoteza golden chance ya kuusimamisha muswada ule.

Kanuni za bunge ziko wazi kabisa kwa mbunge asiyeridhika na uwasilishwaji wa muswada na unaeleza wazi nini cha kufanya!. Chadema hawakufanya walichotakiwa kufanya na sasa wanaishia kuysusa huku wenzao wanazungumza!. Leo muswada unamalizika, bunge litakaa kama kapati kupitia kifungu kwa kifungu, vifungu vyote vitaafikiwa, bunge likakaa kama bunge, watausoma kwa mara ya tatu na kuupitisha hapo hapo.
Na kwa hasira na kibri, Jumatatu, JK atausaini kwa mbwembwe pale ikulu na utakuwa sheria!. Who are the looses?!.

Maadam Chadema wameamua kufa kuzungu na tai shingoni, na hawawezi tena kumeza matapishi yao, hii naiongeza kwenye ile list yangu ya "Chadema are Wrong!. That was yet Another Big Mistake!". (Naianzishia thread yake).

Pasco.

Sad sad sad reasoning...taarifa ndefu lakini haina mashiko, what were you trying to tell us kuhusu Chadema? i can bet hata thread utakayoianzisha juu ya Chadema haitapata majibu au michango yenye akili hata kidogo, sana sana utajuta hata kwanini umeanzisha. Let me advice you, kwa nini usianze kuwa advisor wa Chama cha "Magamba" badala ya kupoteza muda kutoa advises katika chama chenye wenye akili na waliojawa busara kama Chadema? nenda kawape wale wenye "magamba" ushauri wako, i guess kule ndio watakusikiliza maana wanawasubiri watu kama ninyi wa kutoa ushauri wa bure.

Ukifanikiwa kupenyeza na kuwa advisor wa Magamba, after ONLY three months rudi humu kwenye forum utupatie listi ya mema uliyoyashauri na idadi iliyokubaliwa na kufuatwa. hapo utaweza anzisha thread yenye kuweza kutoa mlinganisho wa nani kashauriwa na hakusikia ila akachukua njia nyingine ya busara zaidi, au nani hata sikio la kukusikiliza hakukupa na bado hali ya nchi na wananchi inazidi kuwa mbaya.Nakutakia kila la heri unapojipanga kutafuta njia ya kupata kibarua cha u-advisor kwenye chama cha magamba.
 
POMPO, inapotokea premise ika differ na conclusion ndio kipimo chako cha akili isiyo timamu?.
Nimesema, na nasema tena, naiunga mkono 'walkout' ya Chadema kama ishara ya protest dhidi ya kuburuzwa, lakini siungi mkono kuisusa hoja nzima at its totality, kwasababu, kupitia kanuni, Chadema had a chance ya kuisimamisha hoja nzima nzima, they lost that one and only chance kuisusa kabisa hoja yote ni another loss!.

Ukifuatilia kanuni ya 86 ya bunge, fasiri ya 2007, utakuta muswada ukiwasilishwa kwa mara ya kwanza, hautoi fursa za kujadiliwa, mjadala ni unapowasilishwa mara yapili tuu, sasa Chadema wamesusa na mjadala, muswada utapita na kuwa sheria, bila imput ya Chadema!

Who is the looser?.
when u r protesting u must expect certain results....na huwezi kushiriki kitu ambacho hukiamini kwani still dhamira itakusuta ...i thnk cdm wananafasi ya kuwaelimisha wananchi nje ya bunge what they where standing for badala wangesemea bungeni ambapo michango yao isingejumuishwa kama sehemu ya mabadiliko.
 
"Emancipate yourself from mental slavery, none but ourselves can free our mind" - Bob Marley. WaZanzibar wamedanganyika kwa mstari mmoja tu kubadilishwa, kweli wameponzwa na "sisimu B" kweli wametema BIG -G kwa karanga za kuonjeshwa. Watanganyika wachache wamekua huru kimawazo na sasa wanawaelimisha wenzao kuhusu hii danganya toto ya hawa magamba. kamwe Hatutaipitisha katiba ambayo haikupatikana kihalali
 
this was the great class 4 me as lawyer and an activist, first i was delighted with Posco arguement on why he say CDM dd a horable mistake in walking out and leave th game to CCM but also i was thrired by his opponent, anyway that is not what i want to say today is that ok! Let assume or agree as Pasco has argued that CDM made one mistake but the only one who could save them, but let it b CDM TLP or CCM A and B we the people of Tanzania we are the one who put them there to work 4 us, the constitution wl not only bind CCM or CDM bt we the people and by the people i mean all of us from all group, so if our servand have not done the work we expected of them then let do it ourself and there are many way we can do it either the easy way or the hard way, the easy way we can just air our views and wish that they listen however if they dnt listen do it the hard way by demonstration, riotes and boycot! We are the people, we are the power.
Thank You!.... Jamani kwa nini wananchi wanalitazama swala hili kama ni la CCM/CDM na NCCR halafu kwa ujinga wetu tunabishana hapa what happened bungeni wakati hili ni swala letu sisi?..

Sisi wenyewe kama raia tunahitaji kusimamia nafasi yetu kwa kutaka Katiba inayotulinda sisi wananchi, na sii kutazama jinsi CCM na CDM wanavyochezeana. mwaka 2011 utakumbukwa duniani kama ni mwaka uloanzisha harakati za kimfumo kupinga Udikteta na Ubepari ambao Mafisadi wamekuwa viongozi na katiba zetu zimewaachia kundi dogo la watu kutawala uchumi wa dunia. Tunataka kuibadilisha katiba kwa sababu hatutaki mfumo kinzani na principals of our founding fathers - UTU.

Nikiwa kama Mhafidhina naamini kwamba Free Trade ni muhimu kiuchumi, na kujumu la serikali ni kulinda maslahi ya wananchi wake wasidhulumiwe lakini inapofikia Mashirika binafsi yana control serikali, kundi la watu wachache matajiri wanachukua jukumu la Kifisadi kuchagua na kupanga masharti kwa serikali dhidi ya misingi iliyotuletea Uhuru wetu...Nitapingana na sera zozote zinazowapa kundi dogo la watu to make decision that define our nation expectations - KATIBA ni ya WANANCHI sio ya vyama vya siasa. Na wewe mwananchi popote Ulipo, kwa itikadi yoyote unayoifuata, fikiria Katiba inayokulinda wewe na siii ushabiki wa vyama.
 
Mkandara,

Niliwahi kusema huko nyuma kuwa kama katiba inaliliwa kwa maslahi ya vyama basi tusitegemee kupata katiba inayokidhi mahitaji. Narudia kusimamia maneno yangu yale yale kuwa katiba hii inayopiganiwa na vyama vya siasa ni yenye maslahi ya CCM, Chadema. Naungana na CUF wameona mbali wamejikalia kimya kwani you can clearly see kuwa sio upande hata mmoja unaoangalia maslahi ya wananchi na watanzania kwa ujumla. Katiba ni kimbilio la wananchi lakini wanasiasa badala ya kuifanya katiba imlinde mwananchi wanataka iwalinde wao na maslahi yao.

I just wish watanzania wangelitazama katiba kama mkataba wa kazi kwa mtu yeyote atakayepewa jukumu la kuendesha nchi yetu. Na hivyo watu wote tushirikiane kuunda mfumo utakaoleta manufaa kwa jamii yetu. Vyenginevyo kuna hatari katiba kuwa hijacked by political opportunists
 
Sad sad sad reasoning...taarifa ndefu lakini haina mashiko, what were you trying to tell us kuhusu Chadema? i can bet hata thread utakayoianzisha juu ya Chadema haitapata majibu au michango yenye akili hata kidogo, sana sana utajuta hata kwanini umeanzisha. Let me advice you, kwa nini usianze kuwa advisor wa Chama cha "Magamba" badala ya kupoteza muda kutoa advises katika chama chenye wenye akili na waliojawa busara kama Chadema? nenda kawape wale wenye "magamba" ushauri wako, i guess kule ndio watakusikiliza maana wanawasubiri watu kama ninyi wa kutoa ushauri wa bure.

Ukifanikiwa kupenyeza na kuwa advisor wa Magamba, after ONLY three months rudi humu kwenye forum utupatie listi ya mema uliyoyashauri na idadi iliyokubaliwa na kufuatwa. hapo utaweza anzisha thread yenye kuweza kutoa mlinganisho wa nani kashauriwa na hakusikia ila akachukua njia nyingine ya busara zaidi, au nani hata sikio la kukusikiliza hakukupa na bado hali ya nchi na wananchi inazidi kuwa mbaya.Nakutakia kila la heri unapojipanga kutafuta njia ya kupata kibarua cha u-advisor kwenye chama cha magamba.

Mary Goerge,

Mimi sio Advisor rasmi, bali ni advisor humu humu jf.

Mwaka jana niliutoa ushauri huu kwa CCM kwenye thread yangu ya CCM Imechokwa!, Chadema Haijajipanga!.

Humu nimeweka tuu yale ya kuyihusu CCM!

Wanabodi,

Nikiwa hapa Dom, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na viti maalum ndio usiseme kabisa, wengi ni makapi tuu, kama sio vidumu, basi ni kwa ajili ya kutoa huduma na kibinaadamu, na hili litathibitishwa na michango yao kikao cha Januari.

Nilipoongea na wale makamanda walikata magogo kanda ya ziwa, nao ni wa kawaida tuu, hivyo nimefikia jibu moja la uhakika, CCM imechokwa baadhi ya maeneo, upinzani hata ungesimamisha jiwe, lingechaguliwa, nadhani ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi hawakujitokeza waliona ni kujisumbua.

Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa toka Asilimia 80% niliyohakikishiwa na mwana CCM mwandamizi mpaka asilimia 60% ni uthibitisho tosha, Watanzania wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzania kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani hawajaonyesha wako tayari kukamata dola.

Najua kwa dhati, japo JK anafurahia ushindi kwa furaha ya machoni, lazima atakuwa na huzuni moyoni kwa kukataliwa na hiyo asilimia 20% kukataliwa ni kukataliwa tuu, kunauma. Hivyo CCM lazima watakaa na kujiuliza kulikoni, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down!.

Dawa pekee ya kuitibu CCM, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba should go first with his old guards team. Msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too late. If you are to du anything, doi it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaweza siasa za kisasa za dot com type.

Kama CCM iko ICU na Chadema haijajipanga, 2015 tutegemee nini?.

Unaweza kufuatilia mabadiliko ndani ya CCM, sisemi ndio walichukua ushauri wangu, bali matokeo tumeyaona.
 
Pasco,

..if CDM were wrong, then CCM must be right.

..sasa hebu tueleze kwanini CCM wako right, na zaidi kwanini mswada huu ni mzuri manake wameupitisha.

..CDM walked out, and lets assume kwamba that was childish. Then were was CCM's maturity ktk kuurekebisha mswada ili ulingane na mazingira ya Tanzania ya leo? Hivi unataka kusema CDM ina wasomi na wanasheria wenye uzoefu kuliko CCM?
 
Back
Top Bottom