Asante, Mzee Mwanakijiji kwa hili, ila mimi naomba kutofautiana na wewe, na msimamo wa Chadema.
Wakati wa kutangaza matokeo ya urais, mimi binafsi nilikuwepo pale ukumbini, Chadema walisusa, nilitofautiana nao na nikasema humu kuwa hiyo ni golden opportunity ya kuiambia dunia kuwa uchaguzi wetu haukuwa huru na wa haki, you just tell it infrot of their faces, mpaka CNN, BBC na vyombo vya habari vya kimataifa vilikuwepo. Nilishambuliwa sana, ila nilisimama niliposimama.
Waliposusio hatuba ya rais pale bungeni Dodoma, pia nilikuwepo, nilisema tena it was not right na tulipofanya mjadala wa kumtambua rais au kutomtambua, pia nilisema, its a waste, kutomtambua kwa kauli na kumtambua kwa vitendo. Rais ana axist in real man hivyo umtambue usimtambue anabaki ni rais na yupo, hivyo kutomtambua ni kujidanyanya.
Nikimalizia hili la juzi, kwanza Lissu ni school mate wangu pale Ilburu, hivyo namfahamu fika, pili tulikuja kukutana nae Atlanta akiwa mwana harakati wa LEAT, hotuba yake ilikuwa na lots of flaws, kwa vile yeye ndie waziri kivuli wa sheria, Chadema walimwachia afanye kila kitu kwenye hotuba ile, laiti kama ingepitiwa na wabunge wengine wa Chadema, makini zaidi ya Lissu, wangekuja bna hotuba nyingine bora zaidi.
Naunga mkono walkout kama ishara ya protest lakini siungi mkono kuususia mjadala mzima bungeni unaomalizika leo. Japo Chadema inao wanasheria makini, lakini ni bure kabisa, wameshindwa kutumia upportunities za kuuzuia uwasilishwaji wa muswada huo kwa mara ya pili ambazo ziko proivided for na kanuni, hivyo kupoteza golden chance ya kuusimamisha muswada ule.
Kanuni za bunge ziko wazi kabisa kwa mbunge asiyeridhika na uwasilishwaji wa muswada na unaeleza wazi nini cha kufanya!. Chadema hawakufanya walichotakiwa kufanya na sasa wanaishia kuysusa huku wenzao wanazungumza!. Leo muswada unamalizika, bunge litakaa kama kapati kupitia kifungu kwa kifungu, vifungu vyote vitaafikiwa, bunge likakaa kama bunge, watausoma kwa mara ya tatu na kuupitisha hapo hapo.
Na kwa hasira na kibri, Jumatatu, JK atausaini kwa mbwembwe pale ikulu na utakuwa sheria!. Who are the looses?!.
Maadam Chadema wameamua kufa kuzungu na tai shingoni, na hawawezi tena kumeza matapishi yao, hii naiongeza kwenye ile list yangu ya "Chadema are Wrong!. That was yet Another Big Mistake!". (Naianzishia thread yake).
Pasco.
Naunga mkono mtazamo wako. Itabidi sasa kutafuta dignifying re- entry kwa kutengeneza kafujo hivi kaku-win public sympathy