Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Na. M. M. Mwanakijiji
Siasa ni sanaa na sayansi. Sehemu ya sanaa ni sehemu ya kumanipulate events, situations, and yes even people. Hakuna namna moja ya kufanya siasa. Keshokutwa wabunge wa CDM wanaweza kurudi Bungeni kama kawaida na kuendelea na majukumu yao kama kawaida. Kutoka kwao Bungeni ni sehemu ya siasa kama vile wale walioamua kutumia jukwaa la siasa kubeza na kukejeli wenzao. Its part of politics. CDM hawaitaji kususia Bungeni, walichosusia ni kuburuzwa na ni wajibu wa kila Mtanzania ambaye anaamini katika dhamira yake kuwa CCM inataka kuliburuza Taifa kwenye mjadala wa Katiba. Ushahidi upo - japo watu wameshasahau - nitawakumbusha siku moja kuwa mchakato mzima ulipangwa uwe hivi na ndivyo utakavyokuwa.
Ninaamini uamuzi wa CDM ni sahihi kwani dhamira ya mwanadamu haina shurti. Hakuna kitu kikuu kwa mwanadamu kama dhamira yake. Ukiondoa imani ya Mungu, mwanadamu anaiamini dhamira yake zaidi kwani ni chombo hicho cha kibinadamu ambacho kinamfanya akubali au akatae. Wakati mwingine katika kukataa ni pamoja na gharama yake. Wapo watu waliotukuza dhamira zao mpaka mauti.
Binafsi naunga mkono uamuzi wa CDM kupinga na ninaunga mkono wale wote ambao watasimama kukataa kushiriki, kujadili, kujihusisha na hata kutolea maoni katika mchakato utakaoandaliwa na CCM. Kwa vile CCM imeamua kuteka hoja nzima ya Katiba Mpya (sote tunajua haijawahi kuwa hoja, ajenda wala mipango yao) ni wazi kuwa matokeo yake yatakuwa kama vile ambavyo CCM inataka. CDM wala hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kuwazuia katika hili. Hata hivyo, wanaweza kulazimisha sheria, wanaweza kuagiza vyombo vya dola na wanaweza kabisa hata kusitisha maandamano yote nchini.
Kitu ambacho hawawezi ndugu zangu ni kulazimisha dhamira zetu. Ni dhamira zetu ambazo ziko huru na unyanyasaji, kusumbuliwa, kutishwa au kushurutishwa kwa namna yoyote ile. Ni dhamira zetu ambazo zinasimama milele huru huku miili imetiwa pingu, na zinabakia huru wakati kejeli na matusi yanaporomoshwa na hata vitisho. Assad wa Syria na Gaddafi kule Libya wote walijaribu kuzima dhamira za watu. Walikuwepo watu waliokataa tawala hizo na hakuna chochote ambacho kiliweza kugeuza au kulazimisha upendo. Leo hii Assad anazidi kutengwa tena katika hali ya kushangaza kabisa kutengwa na Waarabu wenzake! Waarabu wanaamini katika kitu kinachoitwa "Arab Nation" wakizungumzia na kumaanisha unity ya jamii ya watu wao. Na wakiunganishwa siyo tu na utamaduni na nasaba zao lakini zaidi wakiunganishwa na dini vile vile. Leo hii Syria inakataliwa na Saudia, inatakaliwa na Uturuki, inakataliwa na Jordan! Lakini Assad anafikiri silaha zitazima dhamira za wananchi wake.
Nimesikiliza na kufuatili kwa siku hizi mbili maneno ya wabunge wetu Bungeni jinsi ambavyo wanasimama wakiwa wamelewa kabisa madaraka kiasi cha kuamini kwa mioyo yao yote kuwa wao ndio Tanzania na sisi wengine wote ni watu tulio chini yao. Wengine wanazungumza in what I could only describe as an utter contempt of the people of Tanzania. Yaani, kuna wengine walikuwa wanazungumza kana kwamba kwa vile wako madarakani na ni watawala basi hakuna wa kuwahoji, kuwapinga, kuwakatalia na sasa wanataka hata vyombo vya dola vitumike kulazimisha dhamira za watu!
Wengine wanasema - na siwezi kushangaa hatua kali zaidi zikachukuliwa - watu wanaopinga mchakato huu wa CCM kuandika Katiba basi washughulikiwe na vyombo vya dola. Na sitoshangaa vitu kama Jukwaa la Katiba vikapigwa marufuku na baadhi ya watu wakaanza kunyanyaswa kwa sababu tu wamekataa kuingizwa kwenye mkokoteni usio na matairi wa huu unaoitwa mchakato wa Kuandika Katiba Mpya. Kwa kadiri nilivyowasikiliza nilitambua jambo moja kwa usahihi kabisa na kwa wazi katika akili zangu - wamelewa ugimbi wa madaraka kiasi kwamba hawakumbuki, hawajui, na hawataki kuamini kwani walikataliwa zaidi mwaka jana kwenye uchaguzi mkuu.
Walikataliwa mwaka jana kwa sababu walishindwa kulazimisha dhamira ziwakubali. Walitumia kila mbinu kulazimishwa kupendwa lakini mwisho wake walikuwa wametengeneza mapenzi ya hofu. NI sawa na mwanamama ambaye anajifanya anampenda mwanamme ambaye amemteka na kumbaka na kumzalisha watoto. Mwanamme yule akiona tabasamu anafikiri anapendwa, akiona mama amempikia chakula anaamini anapendwa. Hajui tu kiilele cha chuki kilichomo ndani ya mtu. Upendo wa hofu ni upendo wa kisasi.
NI upendo ambao mtu akipewa nafasi ya kufanya kitu kibaya atakifanya kibaya kuliko akili za mwanadamu zinavyoweza kudhania. Namkumbuka miaka hiyo (SIMULIZI LA KWELI) mwanamke mmoja ambaye baada ya kunyanyaswa sana na mume wake (ambaye aliamini anapendwa) alikesha usiku mmoja akiwa amefikia kikomo cha uvumilivu wake na dhamira yake ikimtia moyo na kumsubiri mumewe aliyekuwa amekwenda kilabuni. Mume aliporudi bwiii alianza vituko vyake na mwisho akalala sebuleni kwenye kochi. Kumbe mwanamke alikuwa anachemsha sufuria la mafuta ya kupikia. Jamaa akiwa amelala mdomo wake na harufu ya pombe mwanammke yule alikuja na kumiminia mafuta yale kama mtu anavyomimina mafuta kwenye galoni bila kutumia mrija! Jamaa hakupata hata nafasi ya kuuliza "why!". Mwanamke aliuchukua mwili na kuuweka kwenye gari na akarudi zake kulala!
CCM iangalie sana inavyolishughulikia suala hili la Katiba Mpya. Sasa hivi hawana hoja ya kutushawishi bali wana hoja ya kutalazimisha. Hawana hoja ya kwanini tuwasikilize wao bali wana hoja kwanini tusiwasikilize wapinzani. Wanatumia nguvu kubwa sana kulazimisha. Kwa wale tunaokumbuka tunakumbuka kuwa walifanya hivi kwenye Sheria ya Uchaguzi Mkuu na tukawatakalia hawakuamini lakini kilipokuja kuwauma wao wenyewe wakaanza kulalamika! Hawajajifunza. Wanaamini kabisa kuwa wao ni zawadi ya Mungu kwa Tanzania! Na ambao wamenitibua zaidi ni wale ambao walikuwa wanazungumza kana kwamba watu hawajui tunachogombania ni nini! Wanafikiria kuwa wao wamezama katika kuelewa kwa kina kila kilichomo kiasi kwamba mawazo yoyote yakitolewa na watu nje ya CCM basi yamekosewa prima facie. Yaani, hawajachukua hata muda wa kuangalia kutoka upande mwingine. Wameamua kuangalia kutoka upande wao tu na ni upande wao tu ndio uko sahihi.
Wamechagua upande mbaya wa historia. Hata hivyo, uzuri wa historia ni kuwa haina ubaguzi sote tumo kwenye historia hiyo hiyo na historia itaamua ni upande gani umechagua upande sahihi wa historia. Upande ambao unatumia dhulma, vitisho, madaraka, na hata kuwa tayari kutumia dola ili hoja zake zikubaliwe mara zote umeoneshwa na historia kuwa ni upande mbaya! Upande huo wapo kina Milosevic na Hitler, upande huo wapo kina Stalin na Mussolini! Upande ambao unashindwa kuheshimu dhamira za watu na uhuru wao kukataa ni upande mbaya na wa kukataliwa.
Ndugu zangu, hakuna shaka sheria hii itapitishwa na itasainiwa kwa mbwembwe - isipokuwa kama Kikwete ataamua kuja upande sahihi wa historia kwa kukataa - kama walivyofanya kwenye mswada wa Sheria ya Uchaguzi. Na ikipitishwa kama ilivyo na kusainiwa kuwa sheria ni wajibu wetu kwetu sisi wenyewe na dhamira zetu na ni wajibu wetu kwa ajili ya kizazi kijacho kukataa kabisa kushiriki mchakato huu, kuupinga, na hata ikibidi kuhamasisha watu kutoshiriki (hili linaweza kufanywa kuwa kosa!). Jamani hatuna cha kupoteza isipokuwa utu wetu na thamani ya kutambuliwa utu huo. Hatuna nguvu, fedha, madaraka na vyombo vya dola kuwalazimisha wakubali kuangalia upya, lakini tunazo dhamira na uhuru wetu.
Nimesema mara nyingi kuwa fikra huru hazifungwi pingu lakini niongeze leo kuwa dhamira hazifungwi minyororo kuvutwa! Walikuwepo watu ambao wameteswa na kunyanyaswa na kuambiwa wachague kusema uongo waachiliwe lakini walikataa kufanya hivyo kwa sababu hawakuwa tayari kuishi na kusaliti dhamiri zao. Naam, wapo watu ambao watatoka na kwenda upande mbaya wa historia lakini wale ambao tumeamua kukaa upande sahihi wa historia tusijali vitisho wala kejeli. Jana nimepata nafasi ya kuwatia moyo wanaharakati kadhaa - wasio wanasiasa - waliopo nchini na kuwaambia kuwa uamuzi wowote wa kupinga mchakato huu wa CCM utakuja na gharama kubwa kama tulivyoona Bungeni. Wataitwa majina, akili zao zitahojiwa na mashambulizi ya wazi dhidi yao yatafanywa na mashine za wale walioko madarakani. Lakini watakuwa na uchaguzi ama kuheshimu na kutii dhamira zao au kufuata mkumbo.
Ndugu zangu, mwanadamu anapoteza utu wake pale anapokataa kutii dhamira yake. Kama unaamini CCM inafanya jambo jema na kuwa inafanya haya kwa nia nzuri na kuwa sheria hii ni nzuri na ndicho tunachokihitaji basi una uchaguzi mmoja tu - kuunga mkono sheria hiyo, kujitokeza kwenye mchakato huu na kuwashawishi wengine kufanya hivyo ili waone makosa ya maamuzi yao. LAKINI!!... kama dhamira yako inakutuma na kukufanya uamini kuwa mchakato mzima umekosewa toka mwanzo na unalengo la kulazimisha vile ambavyo CCM inataka kwenye Katiba Mpya na ya kuwa hukubaliani na mtindo mzima unavyokwenda - uchaguzi wako nao ni mmoja tu. Kupinga, kukataa na kuamua kutokushikiri hadi pale ambapo mfumo mzuri, huru na wenye kuheshimu KANUNI YA KWANZA (Soma Tanzania Daima leo) ya kuandika Katiba Mpya.
Hakuna uamuzi wa katikati.