Dhambi ya zinaa ni ile ile uzini na kahaba au asiyekuwa kahaba

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,836
Mwanaume anaechukua kahaba akaenda nae kufanya uzinzi na akaachana nae akaendelea na hamsini zake,na yule anaetafuta watoto wasafi waliokuwa wako nyumbani wametulia akazini nao wakuu dhambi ni ile ile.

Jamii isiwaseme sana wale wanaochukua makahaba ikawaacha wale ambao wanachukua wasiokuwa makahaba na kuona kwamba hii sio shida sana.

Jamii ijikite kuwasema na kuwazuia watoto wa kike na kuwatunza kimaadili zaidi ili wasiingie kwenye ukhaba,watakapofanya hivi wanatengeneza kizazi cha baadae huku kizazi cha sasa cha makahaba kikipotea taratibu.

Ukahaba hauishi kwa sababu jamii inaona kwamba ukahaba ni dhambi kubwa kuliko ile ya zinaa,wakati zinaa ni ile ile moja na dhambi ni ile ile tu.

Mwanaume akizini na kahaba,na mwanaume mwingine akizini na asiyekuwa kahaba hawa wote wamefanya uzinzi,lakini jamii itamchukia zaidi huyu aliyefanya na kahaba kuliko mwingine huyu,haya ni makosa inatakiwa wakemewe wote.

Zinaa ni moja dhambi ni ile ile,msikuze sana ionekane ukahaba ni dhambi kubwa kuliko hizo za kuzini na asiyekuwa kahaba.

Uzini kwa kutoa pesa ama uzini bure kinachoandikwa ni dhambi tu haijalishi umeifanya kwa kugharamia au bure.

Wanaoathirika na ukahaba zaidi ni wanawake.

Mzazi unapomuacha mwanao afanye zinaa na mwanaume wake lakini ukamkataza ukahaba ujue kuwa unamkataza asiww kahaba kwa jina lakini kimatendo anafanya sawa sawa na wale makahaba.

,USIKATAZE JINA,KATAZA MATENDO.
 
Dhambi ndio kitu gani?

Kama kutembea na wanawake ni dhambi ama ndio inaitwa dhambi ya uzinzi mbona hata Mungu mwenyewe alikua anaruhusu watu wanatembea na wanawake kibao?

Biblia inasema Daudi alikua ni jicho la Mungu lakini bado Daudi alikua anatafuna wake za watu kama hana akili nzuri.

Suleiman alikua kiongozi na alikua anatafuna wanawake kama mashine.

Ibrahim alikua na vimada kibao hadi wadada wa kazi alikua anajilia tu.

Waizrael walipokua wanarudi toka misri Mungu aliwaambia kila kijiji waue wanaume wote halafu wanawake ni mali yao, kila mtu ajichukulie wanawake idadi anayotaka, mbona haikua dhambi?

Achana na hadith za dini hakuna kitu kinaitwa dhambi, una nguvu za kiume na una uwezo tafuna kadri uwezavyo.
 
Dhambi ndio kitu gani?

Kama kutembea na wanawake ni dhambi ama ndio inaitwa dhambi ya uzinzi mbona hata Mungu mwenyewe alikua anaruhusu watu wanatembea na wanawake kibao?

Biblia inasema Daudi alikua ni jicho la Mungu lakini bado Daudi alikua anatafina wake za watu kama hana akili nzuri.

Suleiman alikua kiongozi na alikua anatafuna wanawake kama mashine.

Ibrahim alikua na vimada kibao hadi wadada wa kazi alikua anajilia tu.

Waizrael walipokua wanarudi toka misri Mungu aliwaambia kila kijiji waue wanaume wote halafu wanawake ni mali yao, kila mtu ajichukulie wanawake idadi anayotaka, mbona haikua dhambi?

Achana na hadith za dini hakuna kitu kinaitwa dhambi, una nguvu za kiume na una uwezo tafuna kadri uwezavyo.
Kwahiyo neno dhambi limebuniwa na wahuni fulani ili kulinda maslahi yao au vipi?
 
Inategemea unafanya na nani.

Ukifanya na wale ambao umeruhusiwa nao kufanya ngono kwa mujibu wa imani husika basi sio dhambi.
Imani husika ndio kitu gani?

Ndio maana tunasema dini ni mambo ya kitapeli.

Kwamba mungu amaruhusu wamaume wa kikiristo wawe na mke mmoja tu, halafu mungu huyo huyo akaruhusu wanaume wa kiislamu wawe na wake 4, ana akili timamu?

Sasa sisi ambao hatutambui hayo maelekezo yake ya kitaahira tukiamua kua na wanawake hata 10 nani anatuzuia?
 
Hakuna atakayekuzuia.
 
Back
Top Bottom