Dhambi ya Ukabila ni Mbaya tumeanza na Wamasai wengine Watafuata

Mmeanza.Hili suala halina chembe za ukabila bali hayo ni matokeo ya ghilba za wanasiasa zilizodumu miaka nenda rudi kwa maslahi yao ya kisiasa na upande wa pili nh ukaidi wa asili wa wamaasai.Kama umdpata kuishi na wamaasai utakuwa umenielewa ninaposema maasai mi wabishi na wakaidi.
na wanasiasa hao ni wanaccm
 
Rwanda walianza hivi hivi kwa kuitana cockroaches.

Sasa unafikiri hiyo jamii pale wakiondolewa wataiona vipi serikali hasa viongozi waandamizi.

Mambo kama haya hayafai kufanyika hasa nyakati hizi ambapo watu wengi wamekwenda shule hivyo level ya ustaarabu ipo juu kidogo.
Saaa wamasai wale wataifanya nini serikali?Wacha vichekesho
 
Miaka 61 baada ya kuwa na Tanganyika huru leo tunashuhudia kampeni kubwa na ya aina yake katika taasisi mbali mbali hapa nchini ya kuwataka wamasai ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 60 kutakiwa kuya hama makazi yao ambayo vizazi na vizazi wamekua wakiita nyumbani.

Jamii hii ya kabila la wamasai ambao wamekua sehemu muhimu ya utambulisho wa Mbuga ya Ngorongoro wamejikuta wakikumbana na kashfa na kejeli za kila aina kutoka kwa wadau mbali ambao ni kama vile hawapendezwi na uwepo wao katika eneo hilo wakisahau kwamba jamii hiyo imeshiriki katika kuikuza mbuga hiyo kufikia sifa iliyo nayo sasa.

Kitendo cha kuwatambua wakazi wa eneo hilo kwa ukabila wake na wala si kama raia wenye haki ya kuishi popote ni cha kibaguzi na kinalenga kuleta mgawanyiko hapa nchini kama kikiachwa kiendelee.

Leo tutashangilia kuwafukuza wamasai na kuwatambua kwa kabila lao ila kesho watafuata wengine mpaka iwafikie wale ambao ni wanufaika wa mfumo huo wa kibaguzi.

Baba wa Taifa aliwahi kuonya kuhusiana na madhara ya ukabila na udini maonyo ambayo bado yanafaa kuyapa nafasi hata sasa kwani hakuna jamii itayokuwa salama kama vitendo vya kibaguzi vitapewa nafasi.

Ni imani yangu kwamba Serikali itichukulia swala hili kwa umuhimu wake na kulitafutia suluhu ya kudumu kwani likiachwa liendelee madhara yake hapo baadae ni makubwa zaidi.

.

Naona hii ni vita ya urais 2025 mama asipite,maana si kwa kumuangushia majumba mabovu huku.
Magu na ubabe wake woye hakufanya haya,mara tozo,masai,ukija huku mbowe yaani dah.
 
wamasai na ng'ombe, mbuzi na kondoo......wanauzwa na wamasai wenzao......wanaojiita WASOMI.....kweli wamesoma....why wasirudi kule kuwaelimisha wenzao......hii suala litawatesa watanzania sana......
 
Kumbe wamasai kuna WASOMI na WASIOSOMA wanaohitaji kuelimishwa?
Well
Waelimishwe sasa ili waache kung'ang'ania ujinga
 
Miaka 61 baada ya kuwa na Tanganyika huru leo tunashuhudia kampeni kubwa na ya aina yake katika taasisi mbali mbali hapa nchini ya kuwataka wamasai ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 60 kutakiwa kuya hama makazi yao ambayo vizazi na vizazi wamekua wakiita nyumbani.

Jamii hii ya kabila la wamasai ambao wamekua sehemu muhimu ya utambulisho wa Mbuga ya Ngorongoro wamejikuta wakikumbana na kashfa na kejeli za kila aina kutoka kwa wadau mbali ambao ni kama vile hawapendezwi na uwepo wao katika eneo hilo wakisahau kwamba jamii hiyo imeshiriki katika kuikuza mbuga hiyo kufikia sifa iliyo nayo sasa.

Kitendo cha kuwatambua wakazi wa eneo hilo kwa ukabila wake na wala si kama raia wenye haki ya kuishi popote ni cha kibaguzi na kinalenga kuleta mgawanyiko hapa nchini kama kikiachwa kiendelee.

Leo tutashangilia kuwafukuza wamasai na kuwatambua kwa kabila lao ila kesho watafuata wengine mpaka iwafikie wale ambao ni wanufaika wa mfumo huo wa kibaguzi.

Baba wa Taifa aliwahi kuonya kuhusiana na madhara ya ukabila na udini maonyo ambayo bado yanafaa kuyapa nafasi hata sasa kwani hakuna jamii itayokuwa salama kama vitendo vya kibaguzi vitapewa nafasi.

Ni imani yangu kwamba Serikali itichukulia swala hili kwa umuhimu wake na kulitafutia suluhu ya kudumu kwani likiachwa liendelee madhara yake hapo baadae ni makubwa zaidi.

.

Haijaanza sasa, ilianza kitambo ukimsikiliza kwa makini Mwl. Nyerere utaelewa ni lini ilianza
 
wamasai na ng'ombe, mbuzi na kondoo......wanauzwa na wamasai wenzao......wanaojiita WASOMI.....kweli wamesoma....why wasirudi kule kuwaelimisha wenzao......hii suala litawatesa watanzania sana......
Kuna hitajika umakini badala ya kupiga siasa.
 
Miaka 61 baada ya kuwa na Tanganyika huru leo tunashuhudia kampeni kubwa na ya aina yake katika taasisi mbali mbali hapa nchini ya kuwataka wamasai ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 60 kutakiwa kuya hama makazi yao ambayo vizazi na vizazi wamekua wakiita nyumbani.

Jamii hii ya kabila la wamasai ambao wamekua sehemu muhimu ya utambulisho wa Mbuga ya Ngorongoro wamejikuta wakikumbana na kashfa na kejeli za kila aina kutoka kwa wadau mbali ambao ni kama vile hawapendezwi na uwepo wao katika eneo hilo wakisahau kwamba jamii hiyo imeshiriki katika kuikuza mbuga hiyo kufikia sifa iliyo nayo sasa.

Kitendo cha kuwatambua wakazi wa eneo hilo kwa ukabila wake na wala si kama raia wenye haki ya kuishi popote ni cha kibaguzi na kinalenga kuleta mgawanyiko hapa nchini kama kikiachwa kiendelee.

Leo tutashangilia kuwafukuza wamasai na kuwatambua kwa kabila lao ila kesho watafuata wengine mpaka iwafikie wale ambao ni wanufaika wa mfumo huo wa kibaguzi.

Baba wa Taifa aliwahi kuonya kuhusiana na madhara ya ukabila na udini maonyo ambayo bado yanafaa kuyapa nafasi hata sasa kwani hakuna jamii itayokuwa salama kama vitendo vya kibaguzi vitapewa nafasi.

Ni imani yangu kwamba Serikali itichukulia swala hili kwa umuhimu wake na kulitafutia suluhu ya kudumu kwani likiachwa liendelee madhara yake hapo baadae ni makubwa zaidi.

.

Huyo nyerere wa nini hapo? Nchi aliingiza kwenye umasikini

Watafutiwe makazi sehemu ingine, kwa usalama wao, na pia kwa usalama wa akina swala, simba na mbweha n.k. waache kulialia, alafu hiyo ngorongoro ni sehemu ya serengeti kama ckosei? Watafutiwe makazi Arusha
 
Akuna ukabira apo suala ni wamezidi wanatakiwa wapunguzwe au waondolewe wote
Sasa wanapunguzwa au kuondolewa kwq njia gan ni Suala la serikar na wasomi wake iliyowaajiri kwa ajiri ya kaz kama iZo
 
We kijana wa juzi tulia huelewi chochote! Aliewauzia ni baba yako mwinyi mzanzibar sio mtz! Na mama yako hapa anataka kuiuza nchi kwa hao mitume wenu
Unaniita kijana wa juzi kumbe huna chochote unachoelewa, Mwinyi sio Mzanzibari, amezaliwa Kivure Kisarawe na hata huko Unguja kwenyewe alikwenda kupata elimu na kuendelea kubakia kama Mwalimu wa Kiswahili na kufundisha kwenye shule ya Mangapwani (Shule aliyosoma). Hivyo Mwinyi ni Mbara mwenzenu...Zanzibar alipitia tu! Weka akilini hilo!!
View attachment 2120092
 
Nasikia harufu ya mbwa hapa nilipo!
Kama nimekukwaza sorry sana! Lakini huo ndio ukweli, hawezi kuwaita waliotoa hela yao halali tena kamili kununua kitu kilichouzwa isipokuwa Mtanzania mwenziwe aliyeuza kwa tamaa na maslahi yake! Au nimekosea!!
 
Hii haina uhusiano na kabila hata kidogo ni wewe tu umetafasiri hivyo kutokana na upeo au uelewa mdogo wa mambo mkuu.

So hebu tuelekeze, wakati bomoa bomoa ya nyumba za mabondeni inafanyika walikuwa wanashambulia kabila gani?!

Wakati wakazi wa kimara wanabomolewa nyumba kupisha upanuzi wa barabara ya morogoro ni kabila gani lilikuwa linabomolewa pale?!

Wakazi wa kiwalani waliobomolewa nyumba na kuhamishwa kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege walikuwa ni kabila gani hebu utuelezee mtaalamu wetu wa tribalism bullying technology.

Je,hapo mbagala waliobomolewa nyumba kupisha utanuzi wa barabara za mwendo kasi walikuwa ni kabila gani eti?!

So unaona,swala ni umefeli kutafakari umekurupuka kwa kifupi umetumia hisia au feelings kufikiri badala ya logic au akili ya kiume.....

Hii ndio shida ya watu wa jamii moja kuishi sehemu moja kuna kuwa na vijimaneno vya kuhisi kuonewa onewa pale maamuzi magumu yakipitishwa na serikali na mamlaka zake.
 
Back
Top Bottom