Dhambi ya Ufisadi yaanza kutafuna Habari corporation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhambi ya Ufisadi yaanza kutafuna Habari corporation

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyoofu, Mar 4, 2008.

 1. M

  Mnyoofu Senior Member

  #1
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Habari nilizozipata kupitia kingo za ukuta za kuaminika, viongozi waandamizi wa Habari Corporation wameanza kujiuzuru mmoja mmoja baada ya kushinikizwa na Rostam Aziz kumsafisha kupitia magazeti yake! Maanayake Habari Corporation imeshaanza safari ya kwenda makaburini kujizika!

  Chanzo changu kinasema Viongozi hao wamekataa shinikizo hilo ili kuepuka kupingana na ethics na integrity ya profession zao!

  Hii inatia moyo, ninawatia hima na moyo wa ujasiri viongozi hao ambao sitapenda kuyataja majina yao kwa wakati huu!

  This is the best atittude transformation, maana tulipofika palikuwa ni pabaya mno. Hii conscience ni ya kizalendo ni muhimu ikapaliliwa wakati huu ili kuwa na taifa la watu wanaojiamini na sio kutumiwa tumiwa tu.

  Nitawapakulia zaidi kadiri habari hizi zinavyojiri.
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  KWELI? wewe upo Birminghan...una data kuliko waliopo TZ? hizo news wires hatari....Ukishindwa kwa Hoja ukubaliane na matokeo...
  Kama Kweli basi watakuwa ni wandishi wachache ktk waandishi tulionao zama hizi, ambapo waandishi wameweza kuwa mafisadi ili watajirike faster..wamiliki magari faster...oohh..ukiwakuta vijiweni wanasema huu ni wakati wao kutajirika...ila kuweni Makini yasije kuwakuta kama yalivyomkuta S.Kubenena!!!
   
 3. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mnyoofu, wataje tu tuwape hongera zao please...kama wamefanya jambo la pongezi, why unaficha majina? Unawanyima haki yao ati!
   
 4. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chuma, nadhani alipo mtu sio hoja, muhimu ni chanzo chake cha habari na hapa watu wana vyanzo mbali mbali haijalishi umbali. Hoja ni content ya alichosema, ninavoona ndivyo walivotakiwa wafanye ili kulinda maadili ya uandishi wa habari (kama yapo kwetu, hilo ni jingine)
   
 5. t

  tibwilitibwili Senior Member

  #5
  Mar 4, 2008
  Joined: Sep 12, 2006
  Messages: 181
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Deo Balile alikuwa Tanzania Daima lakini alinunuliwa na akina Salva na wajinga wenzake kwenda Habari Corp je na yeye kakataa ? Maana alikuwa Arusha na Lowasa hadi Monduli .Hebu lete majina tuone .
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hizi habari ni za kweli kwani jana (jumatatu) kulikuwa na mkutano ambao kwa wale wanaokumbuka ilizungumzwa humu ni jinsi gani vyombo vya RA vilipangwa kutumika kuwasafisha kina EL na RA. Mambo yalienda kombo na kuwaudhi waandishi wengine waandamizi kufuatia ripoti ya Balile toka Monduli ambayo ilikuwa imejaribu kupamba kwa maneno kurudi kwa EL jimboni kwake.

  Ripoti ile siyo tu iliwaudhi baadhi ya waandishi waandamizi lakini ilitengeneza ufa ambao nadhani sasa wameamua kuushughulikia..
   
 7. T

  TAIKUBWA Senior Member

  #7
  Mar 4, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Stay In Tune Another Mwakyembes,s In Teh Air
  Glory B To God
   
 8. t

  tibwilitibwili Senior Member

  #8
  Mar 4, 2008
  Joined: Sep 12, 2006
  Messages: 181
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  There you are .Mara ya mwisho nimekutana na Balile hapa Arusha akiwa kanunuliwa laptop mpya na connection toka Vodacom ya kasi anatesa mjini Arusha anakaa hotel kali.Nikamuuliza vipi wewe akasema anatokea Bukoba lakini kasahau kwamba mimi nilikuwa kwenye msafara na tulikuwa sote bila yeye kujua kwa kuwa alikuwa ana hangaika na kupamba mambo ya Lowasa.This young man walifika bei kwake akiwa UK pale Hull University , baada ya kumpata wakataka kuhamia kwa Ngurumo lakini Ngurumo ni kichwa wakashindwa.Membe alimtuma Salva wakamwita Hotelini London akawajibu kwa mkato kwamba ana heshimu maandiko yake na anasimamia anayo yaamini .salva akawa anaendelea kupiga simu kwa Ngurumo lakini akawa hawezi kupeleka Ujumbe .

  Wakapanga sasa kumnuanua Mwanakijiji kwa gharama kubwa nako wakaja wakakwama ila bado vyanzo vyangu vinasema wanajaibu bado .Balile was cheap and he is still cheap.
   
 9. D

  Dotori JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Imefika wakati waandishi wa habari waheshimu na kuthamini taaluma yao.
  Hali hii ya kujirahisisha na kutimiza malengo ya wale wenye nia mbaya, kunaidhalilisha na kutafanya taaluma hii ipoteze imani kwa wananchi.
  As they say, charity begins at home.
   
 10. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli kwa haya, Jumuhiya ya wana JF inawapongeza sana hao wanahabari na kuwa nao bega kwa bega wakati huu ngumu wa transition.
  Ok ningependa tuwajue tu jamani, hao ni mashujaa sana kama akina Mwakyembe, kama tunawajua Mafisadi (EL,RA, balali) Iweje Mashujaa muwafiche, tuelezeni jamani
   
 11. m

  mtalii JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2008
  Joined: Dec 14, 2006
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chuma.

  Thread hii itakupa mwanga kumjua BALILE alivyokwenda kwa Membe inawezekana alishindwa kumtunza na sasa kaenda kwingine.
   
 12. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..ukishanunua waandishi,what next? kununua wananchi au?
   
 13. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  .."penye dhiki penyeza rupia"
   
 14. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Kumbe Balile mganga njaa tu. Si ajabu tunaye humu humu ndani akiwatetea mafisadi. Kazi kweli kweli.
   
 15. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Dunia ni sawa na kijiji kaka
   
 16. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 914
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  ni kweli kabisa,waliojiuzuru ni wakurugenzi wawili,ambao ni MULINGO na MWALIMU na mwingine aliyejiuzuru ni ATTLYO TAGALILLE.
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mulingo au Muhingo Rweyemamu?
   
 18. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 914
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  aksante kwa kunisahihisha ,kubwa,ndiye huyohuyo!,na inasemekena BALILE alijiuzuru na akatimkia uganda,ila FISADI RA ALIMPIGIA SIMU ya kumwomba arudi na kuendelea na nafasi yake,BALILE alirudi j3 asubuhi na kukutana na kikao ambacho kilisababisha watu hao kujiuzuru
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Mar 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ..taarifa ni mtandao kujeukana ..kila mmoja jk .muvi na muiran..wanajua umaarufu unapatikana kwa kununua waandishi!!!

  duru zinasema kuna waandishi wamepewa milioni 40 na upande wa muiran na muvi....wakala,baadaye wakaenda kwa upande wa muungana wakawaambia wamelambishwa 40 wapambe upande wa pili,..napo wakalambishwa maradufu.....sasa nashindwa kuhusisha moja kwa moja kutimka kwa waandishi wa habari na hii sintoelewa..kujua kati ya hao waliokula kote kote ni wepi waliojiuzulu au waliobaki! but picha iko hivyo.......hadi kufikia hapo nachelea kuita yeyote kati ya hao kuwa shujaa@@@!!!!
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wakiwanunua waandishi wote wa habari sisi akina MADELA WA MADILU tutaanzisha vyombo vyetu vya habari.

  Sasa hivii natumia less than 10% ya muda wangu wote kuchangia hapa JF. Hebu fikiria leo hii niamua kutumia 30% ya muda wangu wote kuandika na kutafuta habari kiongozi gani atasimama huko Tanzania?

  Je nikiamua kuifanya kazi yangu ya pili je?

  Kabla yauchaguzi wa 2010 tutakuwa na INVESTIGATIVE JOURNALIST wengi sana Tanzania, waaandishi ambao mara zote hutoa makala 2 au 3 kwa mwaka kwa sababu hutumia miezi zaidi ya 6 kutafiti na mara utafiti ukikamilika hutumia wiki 2 kuandika makala. Makala za naman hiyo siku zote ni zile zakutikisa na kulegeza vizingiti vyote vya vya watendaji wengi wa serikali.

  Kwa asili sisi akina Madela Wa Madilu, si kwamba hatununuliki, la hasha, tunanunulika kwa gharama isiyoweza kumpa faida mnunuzi yeyote.

  Lowassa akija taka kununua chombo changu cha Habari bei yake ni poa kabisa, Uhai wake tu. Akikubali nimtoe kafara yeye na mkewe nitakuwa tayari kuandika mazuri kuhusu yeye. Lakini itamsaidia nini wakati kesha yaonja mauti??
   
Loading...