Dhambi ya kuua humchukiza sana Mwenyezi Mungu

Mr Director

JF-Expert Member
May 10, 2015
306
1,000
Mnatendea watu ubaya alafu mnajificha kujitetea kwenye kivuli cha Mungu hapendi kuua...
Aiseee as long as unaweza kumuua mtu wee ua tu tena kikatiri, binadam mna makusudi sana...
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,980
2,000
Swali langu ni; ni kweli kila linalotokea duniani ni mipango yake?

Mimi naona hapana!

Mengine ni mipango ya Wanadamu wenyewe!

Matharani dereva aendeshe gari mwendokasi akipata ajali tuseme mipango ya Mungu? Hapana nakataa.

Mtu aache kushika kanuni za kiafya ili kuepuka uchafu na magonjwa akiugua tuseme Eti mipango ya Mungu? Hapana!

Uache kufanya kazi ukikosa chakula useme mipango ya Mungu?

Mgonjwa asiende hospitali au asinywe dawa halafu ikitokea vinginevyo mseme mipango ya Mungu? Hapana

Vinginevyo uzembe , uvivu n.k tutasema mipango ya Mungu wakati Mungu hapendezwi nayo
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,980
2,000
Kitendo cha kutoa uhai wa mtu mwingine makusudi kinamchukiza sana Mwenyezi Mungu. Kitendo hiki kinaingilia na kuvuruga uumbaji na mioango ya Mungu kwa mwanadamu duniani.

Kabla ya kushushwa kwa Amri kumi za Mungu, watu waliuana sana. Waliuana katika kuteka miji na utawala, visa vya kujilikimbizia mali na hata kupoteza ushahidi.

Amri kumi zikienezwa Ulaya na dola ya Warumi, kabla ya hapo Wazungu waliuana sana. Waliona fahari kutundika mafuvu ya vichwa ukutani kama fahari kuonyesha idadi ya watu ulio wahi kuwaua.

Wauwaji hawana maisha marefu duniani, wale wanaoishi huishia kuishi maisha ya mateso. Kutoa mimba pia ni uuaji na humchukiza Mwenyezi Mungu.

Watakuambia Mungu anasamehe dhambi zote mtu akiomba toba!

Lakini nawaambia watu sizani kama ni rahisi kiivyo kukubaliwa toba kwa dhambi kama hiyo ya kuua mwanadamu maana siri ya uhai wake ni kubwa sana na aijuae ni Mwenyezi Mungu pekee.

Pia kusamehewa ni jambo moja lakini ku-suffer the consequences zitokanazo na dhambi aloifanya mtu au watu ni jambo lingine.

Hata Adam na Eva/Hawa baada ya kumtenda Mungu dhambi walikuja kusamehewa badae baada ya Yesu kuja lakini the consequences/madhara/athari /laana/mabaya /yatokayo na ile dhambi hadi leo Duniani yanaendelea kizazi hata kizazi.

-kuzaa kwa uchungu
-kuhangaika kutafuta riziki kwa miiba na michongoma
-uadui wa nyoka na mwanamke
-n.k

Yote bado yapo pamoja na msamaha lakini madhara yatokanayo na ile dhambi hayaondoki.

Tuepuke sana kutendeana mabaya maana yana adhabu endelevu.
 
Roger Sterling

JF-Expert Member
May 10, 2015
12,716
2,000
Mimi naona hapana!

Mengine ni mipango ya Wanadamu wenyewe!

Matharani dereva aendeshe gari mwendokasi akipata ajali tuseme mipango ya Mungu? Hapana nakataa.

Mtu aache kushika kanuni za kiafya ili kuepuka uchafu na magonjwa akiugua tuseme Eti mipango ya Mungu? Hapana!

Uache kufanya kazi ukikosa chakula useme mipango ya Mungu?

Mgonjwa asiende hospitali au asinywe dawa halafu ikitokea vinginevyo mseme mipango ya Mungu? Hapana

Vinginevyo uzembe , uvivu n.k tutasema mipango ya Mungu wakati Mungu hapendezwi nayo

Kwa hiyo kimsingi yanayomtokea mwanadamu yako mikononi mwake mwenyewe, sio?
 
GRANDPUBA

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
722
1,000
Kitendo cha kutoa uhai wa mtu mwingine makusudi kinamchukiza sana Mwenyezi Mungu. Kitendo hiki kinaingilia na kuvuruga uumbaji na mipango ya Mungu kwa mwanadamu duniani.

Kabla ya kushushwa kwa Amri kumi za Mungu, watu waliuana sana. Waliuana katika kuteka miji na utawala, visa vya kujilikimbizia mali na hata kupoteza ushahidi.

Amri kumi zikienezwa Ulaya na dola ya Warumi, kabla ya hapo Wazungu waliuana sana. Waliona fahari kutundika mafuvu ya vichwa ukutani kama fahari kuonyesha idadi ya watu ulio wahi kuwaua.

Wauwaji hawana maisha marefu duniani, wale wanaoishi huishia kuishi maisha ya mateso. Kutoa mimba pia ni uuaji na humchukiza Mwenyezi Mungu.
Mungu hana hasira, hana furaha, hana Upendo na wala hana chuki. Hizi ni attitudes za binadamu, Mungu sio binadamu.

Hicho kinachoitwa MUNGU ni hali ya kuwa (State of Being), haitendi chochote. (Hii mada ni ndefu na kwa sasa sina muda).

Chochote kinachotokea hapa Duniani kinasababishwa na binadamu au matokeo ya nature yenyewe namna inavyoji_organise na inavyoratibu matukio yenyewe, unachomfanyia X ndio hicho hicho utafanyiwa wewe, hata kama utafanyiwa na Y na siyo X lakini kitakufika tu kwa namna yeyote.

Karma is Real na haisababishwi na Individual yeyote, iko automatically.

Nature is Real, na inaji_organize yenyewe.

Mungu sio lijitu fulani kubwa lenye midevu ambalo liko hapo juu mbinguni kana kwamba linatuangalia sisi hapa chini na linasababishwa matukio, kwamba nani afanikiwe, nani asifanikiwe, nani ampe na nani asimpe. Hakuna upuuzi kama huo.

Kinachotokea Duniani ni jitihada.za binadamu na kudra ya Nature kwa namna inavyo_support au kuto_support hizo energy kwa wakati huo.
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,309
2,000
Ben,Azory et al waliuawa na kupotezwa familia zao zisishuhudie makaburi yao.Ni ukatili uliopitiliza.
Wataficha wapi sura zao "wasiojulikana" wanaojulikana na Dhambi hii??
Ni SAwa na kisa cha lazaro na tajiri wametenganishwa na ukuta mrefu.
Azori na ben ndio lazaro wa sasa peponi.
 
Kitimoto

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
1,770
2,000
Kitendo cha kutoa uhai wa mtu mwingine makusudi kinamchukiza sana Mwenyezi Mungu. Kitendo hiki kinaingilia na kuvuruga uumbaji na mipango ya Mungu kwa mwanadamu duniani.

Kabla ya kushushwa kwa Amri kumi za Mungu, watu waliuana sana. Waliuana katika kuteka miji na utawala, visa vya kujilikimbizia mali na hata kupoteza ushahidi.

Amri kumi zikienezwa Ulaya na dola ya Warumi, kabla ya hapo Wazungu waliuana sana. Waliona fahari kutundika mafuvu ya vichwa ukutani kama fahari kuonyesha idadi ya watu ulio wahi kuwaua.

Wauwaji hawana maisha marefu duniani, wale wanaoishi huishia kuishi maisha ya mateso. Kutoa mimba pia ni uuaji na humchukiza Mwenyezi Mungu.
Kweli, ogopeni sana hii dhambi
 
mzushi flani

JF-Expert Member
Jan 20, 2020
1,636
2,000
Mungu hana hasira, hana furaha, hana Upendo na wala hana chuki. Hizi ni attitudes za binadamu, Mungu sio binadamu.

Hicho kinachoitwa MUNGU ni hali ya kuwa (State of Being), haitendi chochote. (Hii mada ni ndefu na kwa sasa sina muda).

Chochote kinachotokea hapa Duniani kinasababishwa na binadamu au matokeo ya nature yenyewe namna inavyoji_organise na inavyoratibu matukio yenyewe, unachomfanyia X ndio hicho hicho utafanyiwa wewe, hata kama utafanyiwa na Y na siyo X lakini kitakufika tu kwa namna yeyote.

Karma is Real na haisababishwi na Individual yeyote, iko automatically.

Nature is Real, na inaji_organize yenyewe.

Mungu sio lijitu fulani kubwa lenye midevu ambalo liko hapo juu mbinguni kana kwamba linatuangalia sisi hapa chini na linasababishwa matukio, kwamba nani afanikiwe, nani asifanikiwe, nani ampe na nani asimpe. Hakuna upuuzi kama huo.

Kinachotokea Duniani ni jitihada.za binadamu na kudra ya Nature kwa namna inavyo_support au kuto_support hizo energy kwa wakati huo.

Unless mtu anajua kuhusu spirituality, hatakuelewa! ila uko very clear!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom