Elections 2010 Dhambi iko mlangoni!

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
500
Ndugu zangu watanzania,
Ni kweli uchaguzi umekwisha kama wengi wanavyoandika hapa na kusisitiza tuangalie ya mbele. Mimi naogopa kusema tu tuangalie ya mbele bila kuangalia tuliposimama. Hapa tulipo mara baada ya kile tunachosema "uchaguzi umemalizika" tuko katikati ya miiba mibaya sana. Miiba ya kuwaamulia watanzania nani wa kuwaongoza na kupuuza maamuzi yao yanayofanywa kwenye masanduku ya kura kwa makusudi.
Kwa ccm na washirika wake ni muhimu sana kukumbuka kuwa watu wana hasira sana na mfumo mzima wa uongozi, uongozi ambao umegeuka kuwa tabaka dogo la mabilionea wanaorithishana madaraka bila kujali umma mkubwa usio na huduma bora za afya, maji safi na salama watu wanatembea usiku kilometa kadhaa kufuata ndoo moja ya maji yasiyosalama, uhakika wa elimu bora hakuna, secondary za kata zinazaa form four failier, hakuna barabra wala matumaini ya masoko ya mazao yao. Watanzania walio wengi wanaishi kwenye matembe au mabanda kwa wale wa mijini kama huelewi ninachosema nenda manzese, Dar, mabatini mwanza au pale bugando utagundua hata vyoo watu hawana wanajisaidia kwenye mifuko ya rambi na kutupa vinyesi barabarani, mlo mmoja ni jambo la kusotea kutwa nzima na matatizo mengine mengi.
Silaha yetu tunapobadilisha mamuzi yao ni mabomu, vitisho, risasi na propaganda za vyombo vya habari. Tunafanya hivyo kulinda maslahi yetu huku tukiwaimbia wimbo wa amani hadharani. Watu wanaona wanasikia na wanapima tambo zetu. Kama tusipofikiri namna ya kushugulika na miiba hii kwa makini sana na bila kiburi wala dharau tuliyonayo, Basi amini usiami dhambi iko mlango inatuotea, Somo la Mwanza, Mbeya, Musoma, Arusha katika uchaguzi huu ni kielelezo tu cha kuonyesha hasira za wananchi na huenda nguvu za mabomu, risasi ulaghai wa vyombo vya habari zikashindwa kuhimili maamuzi ya watanzania walio wengi na wanaoishi hali ya ufukara wa kutisha.
kama ccm na washirika wake wanadhani kuwa ni lazima waendelee kuwa watawala basi chukuweni hatua za makusudi za majibu ya hiyo miiba vinginevyo msije mkasema kama tuliona kwa nini hatukusema mapema. Nchi zote zilizowahi kuwa na vita si kwamba watu hawakupenda amani ni matokeo ya wachache kufaidi keki ya taifa huku walio wengi wakiisha maisha ya ufukara wa kutisha kama ilivyo hapa Tanzania.
Tumewaambia Mapema
Nawasilisha
 

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
195
Ndugu yangu wewe hujui kuwa Salma (Marie-Antoneitte) alipopita kule Mbeya nadhani Tunduma na Mbeya Vijijini watu alipowapungia mkono watu wakamnyooshea vidole viwili alilalamika sana kuwa watu hawana shukrani kwani CCM imewafanyia mengi. Anashangaa kama Marie-Antoneitte kwamba kama watu hawana mkate kwa nini wasipewe keki? Sasa hao ndio viongozi wetu wao kilio cha Watanzania ni uongo kwani madhali wao wanaishi vizuri basi mambo kwa kila mtu ni mazuri.
 

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,523
2,000
Iedit kidogo mkuu na kuiwekea paragraphs, manake haivutii kuisoma kisha nitarudi na my comments!
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
Mkuu umeongea point nimeiona but haivutii kuisoma ikiwezekana iedit kidogo isomeke vizuri!
Ni kweli ccm ingekomesha ufisadi kwanza ndiyo iangalie mengine, kwasasa kila kitu ni rushwa na hakuna mtua asiyejua hilo kwanini wasipambane na ufisadi? Mali tuliyonayo inaweza kutubadilisha maisha kama tu itatumika vyema! Tuache unafiki jamani kwenye ukweli ujulikane ccm wajilekebishe kwa miaka hii mitano!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom