Dhamana ya kuongea hadharani

Mwanandahani

New Member
Jun 6, 2009
3
0
Naomba niwashukuru wote walioanzisha tovuti hii na wale wote wanaoshiriki kwa kutoa mchango wao wa mawazo ili yaweze kusomwa hadharani. Pia shukrani nyingi kwakuniwezesha kuwa mdau wa tovuti hii.

Natambua kuwa kuwezeshwa kupata fulsa ya kutoa mawazo ili yaweze kusomwa au kujadiliwa na jamii (mtandaoni) ni dhama ambayo jamii imetukabidhi kwakuwa inatambua mtu yeyote anaweza kuijenga kama mwanajamii.

Ili shukrani zangu ziwe za kweli na maana, ninaahidi kuiheshimu jamii yote inayoshiriki katika "forum" hii kwakuyajali na kuyathamini maoni na mawazo ya wote nikiwa na uhakika kuwa yatanifunza kitu fulani. Nitaitumia dhamana niliyopewa na jamii hii kwakuijenga na si kuibomoa jamii. Natambua kuwa uhuru wa kuongea niyawazayo hauniruhusu kuwatusi au kuyabeza mawazo au matendo ya wengine, hasa pale ambapo sina ufahamu wa kina kuhusu mawazo ya wengine au mazingira yaliyopelekea wao kusema au kutenda kama walivyofanya.......

Mjenga nchi ni mwananchi....:)
 
Back
Top Bottom