Dhamana kwa mdhamini

kande kavu

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
234
86
Waungwana naomba msaada wa mawazo kisheria.

Nimemdhamini bwana mdogo wangu ambaye anatuhuma za kupora pesa kwa mtandao. Kabla ya kukubali dhamana mheshimiwa hakimu alinieleza maana ya mimi kuwa mdhamana na mwisho akanitaka nitoe jibu la mwisho kama niko tayari kuendelea na dhamana, nami nikakubali, dhamana ikapokelewa.

Kinachonisumbua akili ni kauli ya Mh. Hakimu kuwa endapo mtuhumiwa atakimbia, kama ilivyo, mimi nitakamatwa. Nikikamatwa hatakubali mimi niwekewe dhamana kwa namna yoyote ile na atanifungulia shitaka la kumtorosha mtuhumiwa. Sina mpango wa kumtorosha mtuhumiwa na muda wote nahakikisha yuko within reach, lakini huyu ni binadamu!

Je ni kweli sina haki kisheria kuwekewa dhamana. Na kama nina haki hiyo, ninawezaje kuidai dhidi ya hoja za Mh. Hakimu?

Msaada tafadhali.
 
Back
Top Bottom