Devil's Advocate Kwa Mohammed Dewji

Fredwash

JF-Expert Member
Oct 27, 2009
1,032
1,372
Jamani najaribu kuwa Devil's Advocate kwenye hii Saga ya Manara VS Mo/Barbara/Simba

Nitaenda kwenye kupande ambao Manara ana claim Simba inanyonywa na Mo, kuwa kusema Mo anasema hapati faida ni uongo
naomba anaejua.

Simba kwenye mikataba yake ya 5 yrs ago kuanzia Sport pesa na mengineyo ukiacha huu wa Vunjabei ambao ni wa mwaka huu simba wanaingiza shilingi ngapi then tuchukue gharama za uendeshaji wa team tuone je, kuna faida inabaki?

Kwa haraka haraka tukichukua report ya Yanga ya mapato na matumizi, utaona Yanga walitengeneza faida ya between 50m to 150m kama sikosei katika miaka miwili nyuma kabla ya hapo walikuwa na hasara, ila GSM alivyo pump in moneys nje ya mkataba wake wa jezi ndio mambo yakaonekana kiasi fulani stable, so kwa faida hiyo ya Yanga tunaweza kusema kuwa wame break even tu.

Maana 100m ni kuweza kusajili local players tu huwezi kuleta mchezaj wa maana kutoka nje au utaweza kulipa mishahara pengine ya mwez tu.

Sasa tukija kwa Simba kwa scenario hiyo hiyo japo wao hawajatoa mapato na matumizi ila nina uhakika mapato yao kutoka vyanzo vingine hawatofautiani sana na Yanga, labda kuanzia mwaka huu.

Ina maana kama Yanga walisema wametumia zaidi ya 7b kwenye huu msimu na wameingiza about the same, na wala hawakushiriki kimataifa, basi naamini Simba nao watakuwa wametumia a bit more pengine 8b au 9b kwa msimu huu, maana wao walishiriki kimataifa. Na bonus za mechi hazipungui kati ya 50m hadi 100m kutegemea umuhimu wa mechi na hapo bado bonus za ubingwa ambapo mshindi sijui anapata ngapi zaidi ya sportpesa kutoa 100m.

Kwahiyo wapi Mo kapata faida kwa Simba, mnaweza kusema kwenye matangazo yake ya kwenye jersey ambapo aliingia mkataba na Simba wa 200m kwa mwaka, je tuseme asingekuwepo kuna kampuni gani 4 years ago ingetoa hata 500m kwa kuweka udhamini wa jersey ndio maana hata GSM ana tender ya ku supply jersey kit na kapiga matangazo yake ya magodoro kwenye jersey

So tukubali tukatae pengine Mo ataanza kupata faida Simba lakini sio ndan ya hii 5 years iliopita na pengine ni mpaka another 5 yrs to come

Same goes to Yanga na GSM kama wakija kuwa investors maana wanachofanya GSM na MO ni kuanza kuaandaa shamba na kupanda mbegu, shamba walilolokuta Porin tukisema wanapata faida eti sababu club zina mashabiki wengi, mashabiki ambao hawaingizi hata 500m kwa miez sita achilia mbali mwezi tutakuwa tunaongea porojo, imagine app ya yanga iliingiza 100+m kwa mwaka mzima wa fedha.

Wakati kama mashabiki laki tano tu wa Yanga wangepakua app na kulipia tuseme buku maana yake Yanga wangeingiza 500m
lakini wameingiza 100m kwa mwaka ndio mnasema hawa watu wanapata faida kwenye hizi club, kivipi?

Wakiondoka GSM Yanga na MO simba haijalishi mchakato ya mabadiliko imekamilika ama la kama hatatokea mtu mwenye mapenzi na mpira halafu pia ana mapenzi na team husika, amin nawaambia hizi club hazitatoboa.

Kuwekeza Simba na Yanga inabidi upende mpira kwanza then uwe mshabiki lia lia wa team hizo, maana ni mapenzi kwa team pekee ndio yatakayo kufanya uthubutu kuweka pesa yako huku ukijua hutapata faida.

Ni lazima ukubali kupoteza pesa nyingi sana ili uziweke hizo club stable, na mbaya zaidi kuziweka stable ni pamoja na kubadili watendaji. Kuondoa habari ya "hii team yetu" kuwe na professionalism kila idara.

Sikatai wanaotoa hoja kuwa Mo lazima atakuwa kuna vitu amefanya kujinufaisha kwa kutumia brand ya simba wanahoja yenye mashiko.. shida inakuja

Je brand ya Simba kabla ya Mo ilikuwa inamnufaisha nani.. kwa hoja ile ile ya Mo kujinufaisha basi kabla yake waliokuwepo wanaonufaika..

ila wametofautiana uwekezaji kuna walioweka kwa kila mtu kuleta mchezaji wake (alleged friend of simba group) kisha baadae aidha wawauze au wajilipe kwenye mapato mlangoni na kuna walionufaika kwa kutengenea jersy feki na kuziuza (baadhi ya wanachama)..

kumbuka hapo kabla simba na yanga jersey wanapata kwa mdhamin.. mara tbl mara sijui nani. na pia kuna walionufaika kwa kukodisha maduka pale msimbazi au kula ten percent kwenye activities zote za club kuanzia safar hadi malazi

.. maana yake ni kama shamba la urithi anaweza kulima kwa jembe sawa anaeweza kukodisha sehem ya shamba kwa mtu mwingine sawa. hakukuwa na utaratibu wa mwamachama wa kawaida sio tu kuhoji bali hata kuchangia..

wanachama walikuwa wanagombana na kuwaondoa viongoz kama team inafanya vibaya otherwise wanawaacha wajilie.. sasa leo tukisema wanachama wananyonywa ni lini wanachama waifaidika ikiwa hawa wao pia hawakuchangia chochote kuijenga club..

Namuona kama Mo alieamua kuja kulima kwa trekta kwenye shamba la urithi.. tofaut yake na waliokuwepo miaka ya nyuma ni uwezo wa kuwekeza .. waliokuwepo waliwekeza kwa kuleta wachezaj na kujilipa kwenye mapato au kuuza wachezaj au jersy feki.. yeye kuwekeza pa kubwa so analima shamba lote..

sasa kama hatutaki haya tuleten njia mbadala itakayo fanya kazi sio ya kwenye makaratasi msiseme mara kuna fans base kubwa.. kwa nchi zetu za africa hasa east africa.. fan base hata wawe 100m watabak kupiga kelele.. labda 1% ndo watakuwa wanachangia club..

sie hatuna desturi kama za wazungu mtu ananunua jearsy kila mwaka na analipia kila ticket.. na hapo team 80% inamikiwa na handfull of ppl tu.

yanga walikuwa wanachangishana wanapata 30m kwa mwez na waliweka harambee kwenye "kubwa kuliko" wakapata 900m ambazo kulikuwa na ahad ndan yake tena hata hao wanachama waliochangia hawakufika hata 1000. ukiondoa watu kama rostam waliotoa 100m + sasa nambie club zenye mashabiki zaid ya 1m michango kwa mbinde.

siku zote chema kinajiuza.. brand ikiwa katika hali ya kuweza kujiuza itapata zaid sasa huna cha ku offer lazima atakaekuja atakupa kutokana uhalisia sio mawazo ya kwenye makaratasi

kama kumpinga Mo au GSM.. inatakiwa iwe kwa data mnamuambia, bwana club yetu sie kujichanga 1b au 500m kwa mwez kawaida ww unataka kuja kuwekeza tuambie unaweka ngap..

sio useme tuna wanachama 3m ila club inaingiza 1b kwa wadhamin, mapato ya uwanjan ukijaa full 300m.. tena special mechi.. ulaya wanajaza uwanja hata team ikicheza na team ya daraja la pili FA.. ila huku team za kujaza uwanja ni zile za top 3 basi..

chelsea inamilikiwa na Mrusi lakin wanajaza uwanja.. mwanachama wa kawaida hapat mgao kutoka kwa mrusi yule

MPIRA NI URAIBU KAMA URAIBU MWINGINE WOWOTE.. hakuna anaefundishwa kupenda mpira unazaliwa unajikuta umechizika na huu mchezo au team flan. so you dont care to spend money hata kama hiyo pesa inaenda kwa mtu maana yake furaha yako ni yeye ajenge team akupe furaha ya mafanikio basi.. ila kama anapata pesa anaiwekeza kwengine team inafanya vibaya ndo hapo mtamnyooshe kidole..

man utd wanapiga kelele na glazers family sababu haifany vizur ila kila mwaka wanajaza uwanja na turnover zao ziko helthier.. Arsenal ndo kabisa ila bado watu wananunua jearsy na kununua tickets.. sababu tayar ni WALEVI WA SOKA NA WAPENZI WA MAISHA WA HIZO CLUB so wanalipia kupewa burudan kama mtu yoyote yule anaekwenda kwenye matamasha ya mzik tu

So jaman tujadili tukiwa positive ili tupate njia sahihi ya nini cha kufanya
 
Nimeshangaa hoja dhaifu ya manara kwamba bidhaa za MO zimejaa kwenye jezi basi anapata faida, kuweka tangazo hakukupi uhalali wa wewe kupata faida, Vodacom wana logo zao kwenye kila timu ya ligi kuu, lakini bado wameondoka kudhamini kisa hasara.
Manara uswahili mwingi kuliko kua realistic.
Akina Hanspop wamekaa mahabusu kisa kushtumiwa kwa ajili ya simba, lakini bado wamekua watiifu kwa timu.
Huu ndio hujuma dhairi ya Haji dhidi ya simba, inawezekana alikua msaliti muda mrefu kwenye timu.
Afu anatoa hoja eti ameondoka kwa ajili ya maslahi ya kibiashara, Je, hayo maslahi ya kibiashara kati ya nani na nani? Je, ni simba na Yanga? Au ni GSM, MO na Azam ? Kama ni hao,Je Azam ndio waliomtuma kuichafua klabu ya simu kisa ugomvi wao na MO?
 
Mbona unaongea kitoto sana

Mara useme pengine
Mara useme hakuna Kampuni zingejitokeza.

Hizi ndo facts?

Hivi unajua maana ya mkataba?

Mkataba unasema utangaze bidhaa zote zako?
Zote?

Ukiingia Mkataba na pespsi .. Mkataba unasema utangaze pepsi..
Sio pepsi na mirinda na seven up na everything hata biscuits za pepsi kama zipo..

Hiyo ni vurugu
 
Nimeshangaa hoja dhaifu ya manara kwamba bidhaa za MO zimejaa kwenye jezi basi anapata faida, kuweka tangazo hakukupi uhalali wa wewe kupata faida, Vodacom wana logo zao kwenye kila timu ya ligi kuu, lakini bado wameondoka kudhamini kisa hasara.
Manara uswahili mwingi kuliko kua realistic.
Akina Hanspop wamekaa mahabusu kisa kushtumiwa kwa ajili ya simba, lakini bado wamekua watiifu kwa timu.
Huu ndio hujuma dhairi ya Haji
AZAM ndio wako nyuma ya hii move full stop sema ngoma wanaicheza wafuasi wa utopolo bila kujua
 
Tatizo hizi hoja zinaongelewa kishabiki au watu wanaoongelea uelewa wao kwenye maswala ya biashara au uwekezaji ni mdogo. Kwanini Azam amewekeza pesa nyingi ili kutangaza ligi kuu na pia kuingia mkataba mkubwa na yanga kwa miaka 10. Ni kwa sababu kwenye mpira kuna pesa. Mo anasema hataki mkataba wa Azam kwa sababu Simba ina thamani kubwa kuliko Yanga, yuko sahihi lakini anatakiwa atafute mkataba ambao utazidi thamani ya Azam na sio yeye kusema timu ikihitaji pesa yeye atatoa kwa kifupi anataka timu imtegemee badala ya timu kujitegemea mfano tumeona yanga Manji alivyoondoka timu iliyumba mpaka gsm alipokuja kuokoa jahazi. Pia akaona thamani ya Simba ni kubwa na inastahili mkataba mkubwa aache kutangaza bidhaa zake kwa pesa ndogo milioni 200.
 
Jamani najaribu kuwa Devil's Advocate kwenye hii Saga ya Manara VS Mo/Barbara/Simba

Nitaenda kwenye kupande ambao Manara ana claim Simba inanyonywa na Mo, kuwa kusema Mo anasema hapati faida ni uongo
naomba anaejua.

Simba kwenye mikataba yake ya 5 yrs ago kuanzia Sport pesa na mengineyo ukiacha huu wa Vunjabei ambao ni wa mwaka huu simba wanaingiza shilingi ngapi then tuchukue gharama za uendeshaji wa team tuone je, kuna faida inabaki?

Kwa haraka haraka tukichukua report ya Yanga ya mapato na matumizi, utaona Yanga walitengeneza faida ya between 50m to 150m kama sikosei katika miaka miwili nyuma kabla ya hapo walikuwa na hasara, ila GSM alivyo pump in moneys nje ya mkataba wake wa jezi ndio mambo yakaonekana kiasi fulani stable, so kwa faida hiyo ya Yanga tunaweza kusema kuwa wame break even tu.

Maana 100m ni kuweza kusajili local players tu huwezi kuleta mchezaj wa maana kutoka nje au utaweza kulipa mishahara pengine ya mwez tu.

Sasa tukija kwa Simba kwa scenario hiyo hiyo japo wao hawajatoa mapato na matumizi ila nina uhakika mapato yao kutoka vyanzo vingine hawatofautiani sana na Yanga, labda kuanzia mwaka huu.

Ina maana kama Yanga walisema wametumia zaidi ya 7b kwenye huu msimu na wameingiza about the same, na wala hawakushiriki kimataifa, basi naamini Simba nao watakuwa wametumia a bit more pengine 8b au 9b kwa msimu huu, maana wao walishiriki kimataifa. Na bonus za mechi hazipungui kati ya 50m hadi 100m kutegemea umuhimu wa mechi na hapo bado bonus za ubingwa ambapo mshindi sijui anapata ngapi zaidi ya sportpesa kutoa 100m.

Kwahiyo wapi Mo kapata faida kwa Simba, mnaweza kusema kwenye matangazo yake ya kwenye jersey ambapo aliingia mkataba na Simba wa 200m kwa mwaka, je tuseme asingekuwepo kuna kampuni gani 4 years ago ingetoa hata 500m kwa kuweka udhamini wa jersey ndio maana hata GSM ana tender ya ku supply jersey kit na kapiga matangazo yake ya magodoro kwenye jersey

So tukubali tukatae pengine Mo ataanza kupata faida Simba lakini sio ndan ya hii 5 years iliopita na pengine ni mpaka another 5 yrs to come

Same goes to Yanga na GSM kama wakija kuwa investors maana wanachofanya GSM na MO ni kuanza kuaandaa shamba na kupanda mbegu, shamba walilolokuta Porin tukisema wanapata faida eti sababu club zina mashabiki wengi, mashabiki ambao hawaingizi hata 500m kwa miez sita achilia mbali mwezi tutakuwa tunaongea porojo, imagine app ya yanga iliingiza 100+m kwa mwaka mzima wa fedha.

Wakati kama mashabiki laki tano tu wa Yanga wangepakua app na kulipia tuseme buku maana yake Yanga wangeingiza 500m
lakini wameingiza 100m kwa mwaka ndio mnasema hawa watu wanapata faida kwenye hizi club, kivipi?

Wakiondoka GSM Yanga na MO simba haijalishi mchakato ya mabadiliko imekamilika ama la kama hatatokea mtu mwenye mapenzi na mpira halafu pia ana mapenzi na team husika, amin nawaambia hizi club hazitatoboa.

Kuwekeza Simba na Yanga inabidi upende mpira kwanza then uwe mshabiki lia lia wa team hizo, maana ni mapenzi kwa team pekee ndio yatakayo kufanya uthubutu kuweka pesa yako huku ukijua hutapata faida.

Ni lazima ukubali kupoteza pesa nyingi sana ili uziweke hizo club stable, na mbaya zaidi kuziweka stable ni pamoja na kubadili watendaji. Kuondoa habari ya "hii team yetu" kuwe na professionalism kila idara.
Mechi zenyewe za ndani zinazolipa ni mbili tu yaani moja kila mtani akiwa home tu zingine hazina maingizo. Yaan ikipigwa simba na yanga ndio yenye maingizo mechi na timu zingine mmmmhhh. Tuwaheshimu hawa watu wamejitolea kwa moyo japo cc watu weusi tuna tabu saana. Tuna taka tunachokiamini hata kama sio kweli iwe hivyo hivyo tofauti na ilivyo
 
Tatizo hizi hoja zinaongelewa kishabiki au watu wanaoongelea uelewa wao kwenye maswala ya biashara au uwekezaji ni mdogo. Kwanini Azam amewekeza pesa nyingi ili kutangaza ligi kuu na pia kuingia mkataba mkubwa na yanga kwa miaka 10. Ni kwa sababu kwenye mpira kuna pesa. Mo anasema hataki mkataba wa Azam kwa sababu Simba ina thamani kubwa kuliko Yanga, yuko sahihi lakini anatakiwa atafute mkataba ambao utazidi thamani ya Azam na sio yeye kusema timu ikihitaji pesa yeye atatoa kwa kifupi anataka timu imtegemee badala ya timu kujitegemea mfano tumeona yanga Manji alivyoondoka timu iliyumba mpaka gsm alipokuja kuokoa jahazi. Pia akaona thamani ya Simba ni kubwa na inastahili mkataba mkubwa aache kutangaza bidhaa zake kwa pesa ndogo milioni 200.

Mkuu hivi unataka timu ijitegemee kwa vipato vipi kwa hizi timu zetu? Watu tu kununua jezi ya elfu 30 ni mbinde, kuingia uwanjani tu hadi zile mechi kubwa kubwa, watu hawalipi ada za uanachama hivi unategemea timu zitaweza kujiendesha? Nakuambia bila kubadili muundo timu zetu zitarudi kulekule kwa nyuma, mpira wa sasa ni pesa.

Kipindi Manji yupo Yanga kulikua hakuna njaa sababu alikua anaweka pesa yake kwa mapenzi yake, wachezaji hawakuwahi kulia njaa na walisajiri mchezaji yeyote waliemtaka niambie Simba kwa kile kipindi ilikuaje?

Manji kaondoka Yanga ulioona njaa ilivyoipiga Yanga? Hadi walishindwa kuwalipa wachezaji likaanza kutembea bakuri. Simba akaingia Mo Msimu wa 2016-2017neema ikaanza wakaanza usajiri mzuri na hakukua na malalamiko ya mishahara, msimu huo ubingwa wakakosa kidogo tu na baada ya hapo hadi leo ni story, simply kila kitu kipo vizuri.

Issue ya kuniambia Yanga na Simba wanakngiza mapato mengi kwa source zipi?
Simba anamkataba na Sportpesa ambao umeisha mwaka huu kila mwaka alikua namapata 1B, alikua na mkataba na UHL wa jezi alikua analipwa 300M per msimu, akaingia Mo extra akawa anatoa 300M kwa msimu na Azam wakawa wanawapa Simba 360M kwa mwaka ukiangalia hapo ni kama 2.2B.

Source nyingine ni viingilio ktk mechi ambapo mechi ya uhakika kuingiza pesa nyingi ni moja tu kwa msimu kama timu haitacheza Champions league mechi ya watani ambayo timu inauhakika wa kupata 400m baada ya makato mechi zilizobaki kuipata hata hiyo 90m ni kwa mbinde. Ukiweka majumuisho yako hapo timu inaingiza kwa mwaka kama 4B tena makadilio ya juu haya.
Bajeti ya Simba kwa msimu wa 2019-2020 ambapo iliishia hatua za awali katika champions league ilikua 6.3B na mapato yalikua kama nilivyo analyze hapo je unaona timu inajiendesha kwa faida hapo? Hapo inabidi sasa Mo kama mzamia ama aikopeshe timu maana ule mzigo wa 20B ulikua haujawekwa.

Ndio maana unakuta kila msimu Simba inapata Mkopo wa pesa Nyingi kwa Mo maana bila hivyo haitaweza kujiendesha kuitunza Simba kwa sasa si mchezo, Mo akiondoka tu top players wote hutawaona Simba maana uwezo wa kuwalipa na hata kuwasajiri tu Simba haitakuwa nao, hata hiyo Yanga yenyewe nakuhakikishia inajiendesha kwa hasara, haiwezi jiendesha kwa hivyo vipato vya timu labda kwa sasa kwa lile deal jipya la Azam linaweza kuwapush zaidi zaidi hapo GSM anaweka mzigo wake kuokoa jahazi.

Tuwaheshimu watu wanaojitokeza kuwekeza katika hizi timu zetu.
 
Timu inajitegemea kwa uwekezaji kama inaoingia sasa hivi, mauzo ya jezi na bidhaa nyingine, mikataba ya kibiashara kama yanga walioingia yanga na azam media au sportpesa, mapato ya uwanjani ya uwanjani yanachangia kidogo sana ila cha muhimu viongozi kuwa waadilifu
 
Mkuu kongole kwa bandiko hili,
Nachoona watu wanajitoa ufahamu kwa makusudi labda kutokana na mahaba kwa Manara au chuki dhidi ya Mo.

Huyu mwanapropaganda Manara anawafanya watu kama musukule kwa kushindwa kutumia akili zao vizuri.

Tujiulize yanga chini ya Manji waliwezaje kutamba kibabe kwenye premier bila ya "akta" je,wangeweza kufanya umafia wa kumnyakua Mbuyu Twite bila kiburi cha hela?

Watanzania tuache chuki dhidi ya hawa wawekezaji katika soka na kama tunahisi wananufaika zaidi ni bora kukaa mezani na siyo kuleta dharau na kebehi.

Manara rudi madrasa ukajifunze adabu ya kufikisha ujumbe kwa mtu epuka kuzalisha fitna.
 
Mechi zenyewe za ndani zinazolipa ni mbili tu yaani moja kila mtani akiwa home tu zingine hazina maingizo. Yaan ikipigwa simba na yanga ndio yenye maingizo mechi na timu zingine mmmmhhh. Tuwaheshimu hawa watu wamejitolea kwa moyo japo cc watu weusi tuna tabu saana. Tuna taka tunachokiamini hata kama sio kweli iwe hivyo hivyo tofauti na ilivyo

Ngozi nyeusi tunashida ya kukiona kikombe kikiwa "half empty" na sio kukiona "half full".. mpenda maendeleo siku zote huwa optimistic ma wala sio pessimistic... mbaya zaid claims zetu zinakuwa za kihisia tu hakuna grounds..

mtu akiambiwa aweke facts ya anachokisema utaona maelezo maarefu. ukiwa muongeaji sana kuliko msikilizaji siku zote utakuwa mtu wa maamuz ya kihisia zaidi na utaona unaonewa au unadhulumiwa
 
Mkuu hivi unataka timu ijitegemee kwa vipato vipi kwa hizi timu zetu? Watu tu kununua jezi ya elfu 30 ni mbinde, kuingia uwanjani tu hadi zile mechi kubwa kubwa, watu hawalipi ada za uanachama hivi unategemea timu zitaweza kujiendesha? Nakuambia bila kubadili muundo timu zetu zitarudi kulekule kwa nyuma, mpira wa sasa ni pesa.

Kipindi Manji yupo Yanga kulikua hakuna njaa sababu alikua anaweka pesa yake kwa mapenzi yake, wachezaji hawakuwahi kulia njaa na walisajiri mchezaji yeyote waliemtaka niambie Simba kwa kile kipindi ilikuaje?

Manji kaondoka Yanga ulioona njaa ilivyoipiga Yanga? Hadi walishindwa kuwalipa wachezaji likaanza kutembea bakuri. Simba akaingia Mo Msimu wa 2016-2017neema ikaanza wakaanza usajiri mzuri na hakukua na malalamiko ya mishahara, msimu huo ubingwa wakakosa kidogo tu na baada ya hapo hadi leo ni story, simply kila kitu kipo vizuri.

Issue ya kuniambia Yanga na Simba wanakngiza mapato mengi kwa source zipi?
Simba anamkataba na Sportpesa ambao umeisha mwaka huu kila mwaka alikua namapata 1B, alikua na mkataba na UHL wa jezi alikua analipwa 300M per msimu, akaingia Mo extra akawa anatoa 300M kwa msimu na Azam wakawa wanawapa Simba 360M kwa mwaka ukiangalia hapo ni kama 2.2B.

Source nyingine ni viingilio ktk mechi ambapo mechi ya uhakika kuingiza pesa nyingi ni moja tu kwa msimu kama timu haitacheza Champions league mechi ya watani ambayo timu inauhakika wa kupata 400m baada ya makato mechi zilizobaki kuipata hata hiyo 90m ni kwa mbinde. Ukiweka majumuisho yako hapo timu inaingiza kwa mwaka kama 4B tena makadilio ya juu haya.
Bajeti ya Simba kwa msimu wa 2019-2020 ambapo iliishia hatua za awali katika champions league ilikua 6.3B na mapato yalikua kama nilivyo analyze hapo je unaona timu inajiendesha kwa faida hapo? Hapo inabidi sasa Mo kama mzamia ama aikopeshe timu maana ule mzigo wa 20B ulikua haujawekwa.

Ndio maana unakuta kila msimu Simba inapata Mkopo wa pesa Nyingi kwa Mo maana bila hivyo haitaweza kujiendesha kuitunza Simba kwa sasa si mchezo, Mo akiondoka tu top players wote hutawaona Simba maana uwezo wa kuwalipa na hata kuwasajiri tu Simba haitakuwa nao, hata hiyo Yanga yenyewe nakuhakikishia inajiendesha kwa hasara, haiwezi jiendesha kwa hivyo vipato vya timu labda kwa sasa kwa lile deal jipya la Azam linaweza kuwapush zaidi zaidi hapo GSM anaweka mzigo wake kuokoa jahazi.

Tuwaheshimu watu wanaojitokeza kuwekeza katika hizi timu zetu.

hawajui njia anazotumia MO kuitengenesa Simba ndo hizo hizo anapita GSM.. GSM kachukua approach ya MO kaiacha approach ya Manji.. GSM mara kibao tumesikia anaweka pesa nje ya mkataba wake. tena yeye pia anafanya na biashara anasambaza jearsy. na kilamsiku anapiga kelele ya counter fit ya Jersey zake

kwa team zetu ili at least hawa wawekezaji wawe na mwanga huko mbele wa kuanza kupata faida ni lazima waweke pesa nyingi kwa hasara na waishike team ili kuondoa wapigaji.. sasa tatizo team ilishakuwa stable mnapiga kelee yunanyonywa ila mnasahau imefikaje hapo. ndo maana Manji alikuja na approch ya kukodishwa team

alichokifanya MO ndo anafanya GSM... sasa hivi Yanga iko chini ya GSM kuanzia kusajili na hadi team ikae wapi.. Uongoz wa Yanga uko kwneye makaratasi tu kiuhalisia hawana mamlaka..

na wala mie sipingi.. kama ili club zetu ziendelee inabidi tuwa na "Necessary evils" basi haina shida.. Asilimia kubwa ya Team nyingi Dunian zilianzishwa na vikundi vya watu.. wenye pesa wamekuja baadae kuzinunua tu.
 
Mechi zenyewe za ndani zinazolipa ni mbili tu yaani moja kila mtani akiwa home tu zingine hazina maingizo. Yaan ikipigwa simba na yanga ndio yenye maingizo mechi na timu zingine mmmmhhh. Tuwaheshimu hawa watu wamejitolea kwa moyo japo cc watu weusi tuna tabu saana. Tuna taka tunachokiamini hata kama sio kweli iwe hivyo hivyo tofauti na ilivyo
Mkuu, wapo watu walivyo amini vitu fulani, kuwabadilisha ni vigumu sana.
 
Ngozi nyeusi tunashida ya kukiona kikombe kikiwa "half empty" na sio kukiona "half full".. mpenda maendeleo siku zote huwa optimistic ma wala sio pessimistic... mbaya zaid claims zetu zinakuwa za kihisia tu hakuna grounds..

mtu akiambiwa aweke facts ya anachokisema utaona maelezo maarefu. ukiwa muongeaji sana kuliko msikilizaji siku zote utakuwa mtu wa maamuz ya kihisia zaidi na utaona unaonewa au unadhulumiwa
Kuna msanii anaitwa marehemu langa aliimba moja ya nyimbo yake kuna mstari anasema "ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye vitabu" sisi tunaleta ujima na hatutaki kufuatana na kuheshimu maadili ya taasisi. Na nyerere alisema tuna maadui wa 3 sasa kizazi hiki yule adui ujinga tunaye saaana aisee
 
hawajui njia anazotumia MO kuitengenesa Simba ndo hizo hizo anapita GSM.. GSM kachukua approach ya MO kaiacha approach ya Manji.. GSM mara kibao tumesikia anaweka pesa nje ya mkataba wake. tena yeye pia anafanya na biashara anasambaza jearsy. na kilamsiku anapiga kelele ya counter fit ya Jersey zake

kwa team zetu ili at least hawa wawekezaji wawe na mwanga huko mbele wa kuanza kupata faida ni lazima waweke pesa nyingi kwa hasara na waishike team ili kuondoa wapigaji.. sasa tatizo team ilishakuwa stable mnapiga kelee yunanyonywa ila mnasahau imefikaje hapo. ndo maana Manji alikuja na approch ya kukodishwa team

alichokifanya MO ndo anafanya GSM... sasa hivi Yanga iko chini ya GSM kuanzia kusajili na hadi team ikae wapi.. Uongoz wa Yanga uko kwneye makaratasi tu kiuhalisia hawana mamlaka..

na wala mie sipingi.. kama ili club zetu ziendelee inabidi tuwa na "Necessary evils" basi haina shida.. Asilimia kubwa ya Team nyingi Dunian zilianzishwa na vikundi vya watu.. wenye pesa wamekuja baadae kuzinunua tu.
Hakika umeandika vema. Hawa jamaa GSM na MO inapaswa waheshimiwe maana jiulize tu hz timu zetu zikipiga ligi ya ndani tu mechi yenye maingizo itakua cku ya simba na yanga kidogo na azam ila hizo zingine hazina maingizo. Afu mtu anakuja anajitapa eti maneno yameijenga timu tuwe na shukrani
 
Mie sijui lolote katika mpira na katika biashara Ila hakuna mfanya biashara yeyote anaeweza kuchezea hela bila kuingiza hapa hamtanidanganya kamwe
 
Mbona unaongea kitoto sana

Mara useme pengine
Mara useme hakuna Kampuni zingejitokeza.

Hizi ndo facts?

Hivi unajua maana ya mkataba?

Mkataba unasema utangaze bidhaa zote zako?
Zote?

Ukiingia Mkataba na pespsi .. Mkataba unasema utangaze pepsi..
Sio pepsi na mirinda na seven up na everything hata biscuits za pepsi kama zipo..

Hiyo ni vurugu
Hata voda walikuwa na mkataba na matangazo wakaweka haikuwalipa, na sasa wameondoka. Mkataba na matangazo hazitoshi kuwa sababu ya pekee kupata faida.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom