Development expenditure struggles

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Thursday, December 29, 2016
Development expenditure struggles


development_1.jpg



In Summary
Development expenditure for October was set at Sh713.7 billion, financed by local and foreign resources, but only Sh380.2 billion, or 53.27 per cent, was released.

By Alawi Masare @AMasare malawi@tz.nationmedia.com

Dar es Salaam. The government is still facing a tough time implementing its budget as it misses both revenue collection and development expenditure targets.

Development expenditure for October was set at Sh713.7 billion, financed by local and foreign resources, but only Sh380.2 billion, or 53.27 per cent, was released.

It was expected that international development partners would have pumped in Sh276.2 billion, but only Sh45.2 billion was released during the month, according to the Bank of Tanzania’s monthly economic review released yesterday.

The government released Sh335 billion of the Sh437.5 billion that was to have been sourced locally for development expenditure.

During the period under review, total government expenditure was Sh1.35 trillion, out of which recurrent expenditure was Sh969 billion, and development expenditure Sh380.2 billion, according to the report.

Revenue collection amounted to Sh1.24 trillion, which was 83.8 per cent of the target. Tax revenue collected was Sh1.11 trillion, 15.9 per cent higher than the collection during the corresponding period in 2015, but 93.1 per cent of the target.

Local government collections from own sources totalled Sh35.5 billion against the projected Sh55.5 billion.

Forty per cent of the government’s Sh29.5 trillion budget for 2016/17 has been set aside for development expenditure.

Only 26.6 per cent of the development budget for September was released, while domestic revenue collection was 16 per cent short of target.

The current account balance recorded a deficit of $1.84 billion in the year ending October 2016 compared with $4.79 billion registered in the preceding year. The shortfall was mainly attributed to a decrease in imports of goods and services coupled with an increase in exports.

The value of exports was $9.47 billion, being 7.5 per cent higher than the sum recorded in the corresponding period in 2015.

“This development was attributed to good performance in exports of traditional commodities, gold as well as increase in travel receipts,” the BoT report says.

Tourism is still the leading foreign exchange earner, having generated $2.2 billion during the year under review followed by gold at $1.39 billion and manufactured goods, which brought in $1.25 billion.

The value of traditional exports, which include tobacco, cashew nuts, tea, cotton, cloves, coffee and sisal, amounted to $850 million during the year.

The value of imports of totalled $10.69 billion in October compared with $13.23 million recorded in the corresponding month in 2015, the report shows.

With the exception of oil and industrial raw materials, all other categories of imports recorded a decline.

The decline in imports was partly attributed to exchange rate depreciation, particularly due to demand for consumer goods and completion of major projects such as cement factories, power plants and exploration activities. During the period, oil imports increased by 1.7 per cent to $2.97 billion, largely driven by an increase in volumes.

The prices of crude oil and white petroleum products declined mainly due to a rise in supply from Opec member countries.

National debt

Tanzania’s external debt stock reached $16.4 billion as at the end of October, being an increase of $7.8 million from the amount recorded during the preceding month.

On an annual basis, the stock of debt was $1.03 billion higher than the amount recorded at the end of the corresponding period in 2015 mainly due to new disbursements.
 
DK. MPANGO: HAKUNA MDORORO WA UCHUMI: Really Mr Mpango!?
 
total government expenditure was Sh1.35 trillion, out of which recurrent expenditure was Sh969 billion, and development expenditure Sh380.2 billion


Hapa ndipo tatizo kubwa la matumizi ya fedha nyingi za umma yasiyo ya kimaendeleo lilipo. Serikali iondoe kabisa au kupunguza vyeo kama ukuu wa wilaya, na makatibu tawala. Pia iondoe au kupunguza baadhi ya nafasi za utumishi kwenye halmashauri; kwasababu kwanza halmashauri nyingi hazipati fedha za kutosha kutekeleza majukumu yake. Watu wanaingia kazini na kutoka kilasiku huku wakiwa hawajafanya kazi yeyote ya maana na bado mwisho wa mwezi mshahara wanalipwa kwa kiwango kilekile. Pia serikali ipige panga posho za Wabunge wanazolipwa kwa ajili ya matumizi yao majimboni. Hizi nyingi zinaishia kwenye matumbo na miradi binafsi ya wabunge ambayo haina faida kubwa kwa jamii wanazozitumikia. Serikali ikifanya haya, itaokoa fedha nyingi ambazo zinaweza kutumika kwenye miradi ya maendeleo.
 
Daaaah pesa hakuna kabisa uchumi mbovu ...........

Yaani tukienda hivi na mwaka huu mpya ni hatari sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hali ni mbaya sana Mkuu lakini bado jamaa hawa wanaendelea kutuzuga Watanzania kama vile hali ya uchumi ni shwari kabisa.

Daaaah pesa hakuna kabisa uchumi mbovu ...........

Yaani tukienda hivi na mwaka huu mpya ni hatari sana
 
National debt

Tanzania’s external debt stock reached $16.4 billion as at the end of October, being an increase of $7.8 million from the amount recorded during the preceding month.

On an annual basis, the stock of debt was $1.03 billion higher than the amount recorded at the end of the corresponding period in 2015 mainly due to new disbursements.

Hilo deni veeep, mbona kama mwendokasi? Wachumi hebu tuwekeni sawa.
 
Mkuu pitia huu uzi. Nadhani hapa wanazungumzia Deni la Taifa nchi za nje bila kuweka deni lote la Taifa na lile ambalo Serikali imekopa kupitia mabenki ya ndani. Ninachojua kuna mkopo mpya toka Benki ya Exim ya China wa $7.6 billion sawa na T shs 16 trillion. Sasa sijui ni sababu zipi zinawafanya wasizungumzie deni lote la Taifa kwa ujumla wake. Kikwete 2005 alilikuta deni likiwa ni trilioni 10 na alipomaliza awamu yake deni lilikuwa limefika trilioni 43 sawa na ongezeko la 33 trilioni katika miaka 10.

Magufuli katika bajeti yake ya 2016/2017 kulikuwa na bajeti deficit ya 8 trilioni ambazo wamekopa ili kujazilia kwenye bajeti na hivyo deni la Taifa kufikia 51 trillion. Huu Mkopo wa kutoka benki ya Exim ya China wa 16 trilioni uliongeza deni la Taifa kutoka 51 trilioni hadi 67 Trillioni.

Kwa maneno mengine Magufuli kishaongeza deni la Taifa kwa mwaka mmoja tu kwa 24 Trillioni ambazo ni sawa na 55.8% kutoka 43 trilioni hadi kufikia 67 trillion, lakini cha kushangaza naona kama kuna juhudi za nguvu kulificha hili la deni kuongezeka katika kasi kubwa kiasi hiki.

Reli ya Kati: Benki ya Exim (China) wakubali kutoa mkopo wa Sh. Trilioni 16 kwa Serikali ya Tanzania

Hilo deni veeep, mbona kama mwendokasi? Wachumi hebu tuwekeni sawa.
 
Tuesday, January 3, 2017
Wachumi washtushwa na kasi ya kufungwa biashara Dar, Arusha



wachumi_1.jpg



Kwa ufupi
Juzi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali imebaini kuwa karibu wafanyabiashara 2,000 wamefunga biashara zao Dar es Salaam na Arusha lakini akasema uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya asilimia saba na unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka huu.

By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wataalamu na wadau wa uchumi na biashara wameeleza kushtushwa na taarifa za wafanyabiashara kufunga biashara zao na kushuka kwa ukuaji wa kilimo, huku wakiitaka Serikali kuweka mazingira wezeshi ya kusisimua uchumi.

Juzi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali imebaini kuwa karibu wafanyabiashara 2,000 wamefunga biashara zao Dar es Salaam na Arusha lakini akasema uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya asilimia saba na unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka huu.

Pamoja na ukuaji huo, Waziri Mpango alisema kilimo kimeshuka kutoka asilimia 2.7 mwaka 2015 hadi asilimia 0.3 mwaka 2016.

Wataalamu wa uchumi na kilimo waliopigiwa simu na mwandishi wetu kuhusu taarifa hiyo ya Waziri Mpango aliyoitoa alipokuwa akizungumzia hali ya uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana, walisema hiyo ni ishara mbaya na kuitaka Serikali kuchukua hatua za haraka.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja alisema taarifa ya wafanyabiashara kufunga biashara zao inatokana na kilio chao cha muda mrefu kisichosikilizwa na Serikali.

“Tunachokijua ni kuwapo kwa mtikisiko wa uchumi kwa mwaka 2016 kiasi kwamba wafanyabiashara wanalalamika kukosa wateja. Siyo kufunga biashara tu, wengine wamerudisha hata TIN (namba ya utambulisho wa mlipakodi) kwa kushindwa masharti,” alisema Minja. “Tunachotofautiana na Serikali ni kuhusu sababu, sisi tunachojua chanzo ni masharti magumu ya kufanya biashara ndicho kinachowashinda watu. Sasa kama Waziri Mpango hajui basi kuna udhaifu kiuongozi.”

Alikuwa akizungumzia kauli ya waziri kwamba sababu za kufungwa kwa biashara hizo hazijabainika kutokana na ugumu wa kupata taarifa kwa wahusika, lakini akabainisha sababu tano za jumla zinazoweza kuwa chanzo ambazo alizitaja kuwa ni kushindwa kuingiza bidhaa nchini bila kulipa kodi stahiki, kushindwa kulipa au kulipwa madeni, kubadilisha aina ya biashara, kushindwa kusimamia biashara, gharama kubwa za uendeshaji na wabia katika biashara kutoelewana.

Minja aliitaka Serikali kujenga mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara: “Unapoona mlipakodi mmoja kati ya 99 anajitoa, unatakiwa uwaache hao 99 umrudishe huyo mmoja, lakini kama hujui hata sababu, basi huo upungufu kiuongozi,” alisema Minja.

Katibu Mtendaji wa Jukwaa la Kilimo (Ansaf), Audax Rukonge alisema kushuka kwa ukuaji wa kilimo kutoka asilimia 2.7 hadi asilimia 0.3 ni ishara kuwa umaskini umeongezeka.

“Ni wazi kwamba katika mwaka mmoja, tumetengeneza maskini wengi kuliko miaka mingine iliyopita. Tusijidanganye kwamba kuna sekta nyingine kama madini au gesi ndivyo vitabeba uchumi wetu. Hata uchumi wa viwanda unategemea kilimo,” alisema Rukonge.

Akizungumzia hali ya kilimo na biashara, Profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Ntengua Mdoe alisema imekuwa mbaya kwa sababu Serikali haiwekezi.

“Wananchi wengi wanategemea kilimo, japo kuna baadhi ya sekta zinazokuza uchumi. Kama ukuaji wa kilimo umeshuka, basi kuna asilimia 75 ya Watanzania wanaendelea kuwa maskini,” alisema.

Profesa Mdoe aliongeza, “Hata biashara zimekuwa ngumu, tunaona hoteli zikifungwa hapo Dar es Salaam na nyingine zikibadilishwa matumizi, ni kwa sababu hakuna mzunguko wa fedha, uwezo wa watu kununua umeshuka. “Serikali inapaswa kuongeza fedha kwenye mzunguko hasa kwenye sekta binafsi ili uwezo wa kununua uongezeke.”

Mtaalamu aliyebobea katika uchumi, Profesa Samuel Wangwe alisema ukuaji wa uchumi hautakuwa endelevu kama kilimo hakikui.

“Kama hali ya hewa itakuwa nzuri basi na uchumi nao utakuwa mzuri, lakini hali ikiwa mbaya na mavuno yasipopatikana, uchumi hauwezi kukua.”

Profesa Wangwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ameishauri Serikali kujenga uhusiano na sekta binafsi ili iweze kuajiri na kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom