Developers: Jinsi ya kufanya miamala ya ki Benki kuhifadhiwa kwenye mfumo wako!!

mpatto

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
766
1,027
Habarini Devs!!

Naomba msaada tafadhari!!
Ni kwa namna gani naweza kupata API za miamala iliyofanyika kwenye Benki automatically ili niihifadhi kwenye DB ya system yangu!?

Kwa mfano, nimetengeneza mfumo wa kumanage Wanafunzi chuoni, moja ya functions zake ni kutrack Nani amelipa kiasi gani! Sasa, nataka mwanafunzi akishalipa Benki, ile API ya ule muamala kutuka Benki hiyo, niipate na kisha niimanipulate kama vile kuihifadhi n.k

Nataka kitu kama vile mfumo Heslb ambapo mtu akishalipa basi anapata taarifa kutoka Heslb kwamba successful amelipa 30k

Mfumo upo tayari, bado sehemu hiyo tu ndio sina uzoefu nayo!! Naombeni msaada ndugu!!

Kudos!
 
Habari mkuu,
APIs ni interfaces za mifumo ambazo nyingi cyo public hususan hizi za taasisi za kifedha kama mabenki kwa sababu ya unyeti wa taarifa zinazopita. Yaani nyingi ni closed na ili upewe access lazima umtafute muhusika wa mfumo, utimize matakwa yake alafu ndo akupe access.

Wengi wanataka kuregister kwenye mfumo wao ili wakutambue na kisha wanakupa API key ambayo unai-append kwenye request zako ili upate taarifa. Hii unaweza kui-append kwa njia mbali mbali kama basic auth na token bearer. Kuna baadhi wanaregister for free wengine wanadau wanataka.

Kwa maelezo yako inaonekana utakata kupata taarifa ya malipa kwenye specific account ya mwanafunzi fulani. Kwa maana hiyo anae-initiate data transfer ni muhusika wa mfumo wa kibenki. Kwa maana hiyo unatakiwa ku-implement call back URL kwenye mfumo wako yakuupokea hizi taarifa kwa mfano kiasi kilicholipwa, nani kalipa, lini kalipa nk. Hii call back URL inakuwa stored kwenye mfumo wa benki na itakuwa triggered au called kila mara malipo yanayokidhi vigezo yakipita kwenye mfumo wake.

Lazima muundo wa taarifa zinazotumwa kati ya mfumo wake na wako uwe-enforced kwenye mfumo wako ili mifumo hii iongee lugha moja. Hii taarifa huwa inatumwa kwa muundo wa JSON au XML kutegemea ya aina ya intergration ya mifumo mliokubaliana. Yaani kama ni REST API au SOAP.

Kama mtua huduma wa benki amesha-implement API ya mfumo wake basi lazima atakuwa na API documentation ambayo ata-share na ww kama ukishakupata API key yake.

I hope nimeeleweka mkuu. I wish you all the best. Nisamehe muandiko wangu ...
 
We bro mpatto umemsoma bro Null Pointer , hivyo ndivyo ilivyo.

Kuna bank ambazo utataka student wazitumie, basi unaweza wacheki wakakupa maelekezo, maana ninavyofahamu mimi ni kama jamaa alivyosema.

Kutuma request za kujua info hizo ni lazima uwe na access ya server husika plus such keys hapo ndo unatembea kulingana na lugha waipendayo kama ni java+xml/json ama php n.k. Nenda kaulizie hilo bank.
 
Ndugu zangu mathsjery pamoja na Null Pointer ninawashukuru sana kwa majibu hayo mwanana!

Nilichotaka kufahamu ni kuwa, je ni hatua zipi rasmi za kufuata ili niweze sasa kupata access ya hizo closed API!?

mathsjery naona umegusia habari za kuzifuata Benki husika physically na kuongea nao, ili waweze kunipa access ya hizo API, je hiyo ndio njia rasmi!?
 
Mkuu nakuomba unielezee kwa undani kidogo jambo hili ndugu!

Ni nini hii!?

Ni platform ya malipo ambapo Mteja akilipa moja kwa moja anakuwa verified kuendelea na huduma nyingine ambayo alitakiwa alipie
 
Ndugu zangu mathsjery pamoja na Null Pointer ninawashukuru sana kwa majibu hayo mwanana!

Nilichotaka kufahamu ni kuwa, je ni hatua zipi rasmi za kufuata ili niweze sasa kupata access ya hizo closed API!?

mathsjery naona umegusia habari za kuzifuata Benki husika physically na kuongea nao, ili waweze kunipa access ya hizo API, je hiyo ndio njia rasmi!?
Njia sahihi ni kutembelea hizo benki ambazo unataka kupata taarifa za malipo. Baada ya ujio wa mfumo wa ulipaji wa serekali (GePG), taasisi za kifedha nyingi zimeboresha mifumo yao ili iwe na API za kuwasiliana na mifumo mingine ya malipo including GePG.

Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kila mtoa huduma atakuwa na vigezo ambavyo lazima mfumo wako uwe navyo ili aruhusu kuendelea na integration na mfumo wako.

Kikawaida wataku-link na kitengo cha integration cha mifumo yao. Then watakupa access ya test environment yao. Ukikamilisha development mtafanya user acceptance test (UAT). Kama mfumo wako ukipita hatua zote, utapewa access ya live environment yao na utapewa API key husika. Then you are good to go mkuu.
 
Hii ndio shida ya nchi kutokuwa na Stripe
Habarini Devs!!

Naomba msaada tafadhari!!
Ni kwa namna gani naweza kupata API za miamala iliyofanyika kwenye Benki automatically ili niihifadhi kwenye DB ya system yangu!?

Kwa mfano, nimetengeneza mfumo wa kumanage Wanafunzi chuoni, moja ya functions zake ni kutrack Nani amelipa kiasi gani! Sasa, nataka mwanafunzi akishalipa Benki, ile API ya ule muamala kutuka Benki hiyo, niipate na kisha niimanipulate kama vile kuihifadhi n.k

Nataka kitu kama vile mfumo Heslb ambapo mtu akishalipa basi anapata taarifa kutoka Heslb kwamba successful amelipa 30k

Mfumo upo tayari, bado sehemu hiyo tu ndio sina uzoefu nayo!! Naombeni msaada ndugu!!

Kudos!
 
Ndugu zangu mathsjery pamoja na Null Pointer ninawashukuru sana kwa majibu hayo mwanana!

Nilichotaka kufahamu ni kuwa, je ni hatua zipi rasmi za kufuata ili niweze sasa kupata access ya hizo closed API!?

mathsjery naona umegusia habari za kuzifuata Benki husika physically na kuongea nao, ili waweze kunipa access ya hizo API, je hiyo ndio njia rasmi!?

Yah! Hii ni njia sahihi, kwa sababu unapotengeneza API ili ya kufetch ama kutoa notification kuwa user kalipa, maana yake inafetch moja kwa moja kutoka kwenye db za bank husika. Sasa wewe kama wewe lazima ujue structure inayokubariwa na mfumo wao na hiyo inapatikana kwenye documentation ya mfumo wao, kwa hiyo kama utatumia XML ama JSON kuunda API yako lazima Kuna attributes zimatch na mfumo ambako unatuma request.

Hapo ndo kuna ulazima wa kwenda bank ama taasisi ya kifedha kuulizia hilo maana haziwekwi mtandaoni kiholela.

Nenda
 
Njia sahihi ni kutembelea hizo benki ambazo unataka kupata taarifa za malipo. Baada ya ujio wa mfumo wa ulipaji wa serekali (GePG), taasisi za kifedha nyingi zimeboresha mifumo yao ili iwe na API za kuwasiliana na mifumo mingine ya malipo including GePG.

Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kila mtoa huduma atakuwa na vigezo ambavyo lazima mfumo wako uwe navyo ili aruhusu kuendelea na integration na mfumo wako.

Kikawaida wataku-link na kitengo cha integration cha mifumo yao. Then watakupa access ya test environment yao. Ukikamilisha development mtafanya user acceptance test (UAT). Kama mfumo wako ukipita hatua zote, utapewa access ya live environment yao na utapewa API key husika. Then you are good to go mkuu.
Asante sana ndugu yangu!! Labda swali la nyongeza, unauzoefu wowote wa kutengeneza mifumo ya namna hii!?
 
Yah! Hii ni njia sahihi, kwa sababu unapotengeneza API ili ya kufetch ama kutoa notification kuwa user kalipa, maana yake inafetch moja kwa moja kutoka kwenye db za bank husika. Sasa wewe kama wewe lazima ujue structure inayokubariwa na mfumo wao na hiyo inapatikana kwenye documentation ya mfumo wao, kwa hiyo kama utatumia XML ama JSON kuunda API yako lazima Kuna attributes zimatch na mfumo ambako unatuma request.

Hapo ndo kuna ulazima wa kwenda bank ama taasisi ya kifedha kuulizia hilo maana haziwekwi mtandaoni kiholela.

Nenda
Asante sana kiongozi!
 
Back
Top Bottom