Deus Mallya: Maswali na majibu ya Kifo cha Wangwe, Siasa n.k

Sitta ni mwana ccm,fuatilia vyema aliyoyasema.Na alimtahadharisha Wangwe kuhusu uwakilishaji wa hoja hiyo iliyohusiana na kampuni ya uchimbaji wa madini...fwatilia mkuu.Kipindi hicho Sitta akiwa spika wa bunge la jamuhuri.

Kwa ninavyowafahamu viongozi wa CDM kama kungekuwa na mkono wa serikali povu lingewatoka na kulaani,wangetangaza siku yake maalum lakini leo hata kwa bahati mbaya Chacha Wangwe hatajwi katika harakati za CDM.Kwa kuwa alikuwa shujaa nje ya chama lakini ndani ya chama ni kikwazo kwa wezi wa pesa za ruzuku. Sitoshangaa Mallya akilipwa fadhila kwani mission accomplished.
 
Kwanza naomba Radhi kwa kuchelewa kujibu hapa. Account yangu ya Deus F Mallya ina tatizo najaribu kuingia nasahau Password (Au ni tatizo la kiufundi).
Pili nitajibu hoja zote kwa umakini (Japo kwa ufupi) kwama ifuatavyo:
1. Swali la Kugombea au kutokugombea Ubunge Jimbo la Moshi Vijijini sijawahi kutangaza popote. Hata hivyo wakati ukifika na nikiamua kugombea si dhambi. (Rufaa #52/2010 chini ya Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mhe.Jaji.H.R.Nsekela walinipa ushindi baada ya kugundua makosa makubwa yaliyokuwepo kwenye shauri langu dhidi ya Serikali mkoani Dodoma kuhusiana na ajali ya gari mwaka 2008)
2. Ni kweli kuwa Cyril Chami (Mbunge wa Sasa) ni Ndugu yangu (Mjomba mdogo).
3. Si kweli kuwa nimeoa Mtoto wa kiongozi wa ccm huko Kilimanjaro. (Sijao bado)
....Naendelea kujibu mengine.
 
bwana deus hata kama cyril n ndugu yako hakuna mantik ya kutogombea hapo, kwanza ww una undugu wa mbali sana na watu wa chami huku ni kwa wajomba wako tu(DAKAU)
 
huyu si ndo Lipumba aliema ana taarifa za kiintelijensia kuwa kafunzwa ugadi libya

Lipumba,Mrema na Mbatia ni kati ya wanasiasa wa Hovyo sana hapa Tanzania!.. Nilisoma kauli zao walizozitoa wakati ule nikaamua kusitisha rasmi mpango wangu wa kuwajadili.. Hata hivyo mpango wa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria utakamilika hivi karibuni kwa sababu walichokisema ni uongo usiofikirika!.
 
bwana deus hata kama cyril n ndugu yako hakuna mantik ya kutogombea hapo, kwanza ww una undugu wa mbali sana na watu wa chami huku ni kwa wajomba wako tu(DAKAU)

Anko nimesema wakati ukifika na nikiamua kugombea sintozuilika.
Ujomba si sababu ya kunizuia kuwatumikia wananchi. Even now yeye yupo CCM na mimi nipo CHADEMA bado undugu wetu 'wa mbali' uko pale pale.
 
Kwa ninavyowafahamu viongozi wa CDM kama kungekuwa na mkono wa serikali povu lingewatoka na kulaani,wangetangaza siku yake maalum lakini leo hata kwa bahati mbaya Chacha Wangwe hatajwi katika harakati za CDM.Kwa kuwa alikuwa shujaa nje ya chama lakini ndani ya chama ni kikwazo kwa wezi wa pesa za ruzuku. Sitoshangaa Mallya akilipwa fadhila kwani mission accomplished.

Alikuwa na udouble agent flani,upande wa pili ndo walimgeuka.Umemsahahu kaka yake ambaye ni ccm nadhani anaitwa samweli wangwe kama sikosei.Yeye alikataa hata uchunguzi wa ziada kwa mwili wa marehemu usifanyike.Na kulitokea mgogoro serikali ya ccm ikauteka mwili wa Wangwe RIP.Kumbuka kulikuwa na tetesi za yeye kupigwa risasi ya mdomo.
 
Kuna taarifa kutoka sehemu mbali mbali huku Moshi Vijijini na baadhi ya maeneo ya Dar kuwa yule mfanyabiashara aliyehusishwa na ajali ya Chacha Wangwe (Deus Mallya) anaendelea na mikakati yake ya kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Moshi Vijijini ambalo kwa sasa linaongozwa na Cyril Chami 'Aliyepigwa chini' kwenye baraza jipya la mawaziri la JK.
Mara kadhaa Deus Mallya amekuwa akikwepa kujibu hili sasa tunaomba kwa kuwa yupo huku atujibu.

Nawasilisha.
Nimeshangaa kwa nini GT wanahangaika kukujibu ili hali wanajua lengo lako. Kama hawalijui nina mashaka na u GT wao.
Mimi nimepita tu.
 
Kwanza naomba Radhi kwa kuchelewa kujibu hapa. Account yangu ya Deus F Mallya ina tatizo najaribu kuingia nasahau Password (Au ni tatizo la kiufundi).
Pili nitajibu hoja zote kwa umakini (Japo kwa ufupi) kwama ifuatavyo:
1. Swali la Kugombea au kutokugombea Ubunge Jimbo la Moshi Vijijini sijawahi kutangaza popote. Hata hivyo wakati ukifika na nikiamua kugombea si dhambi. (Rufaa #52/2010 chini ya Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mhe.Jaji.H.R.Nsekela walinipa ushindi baada ya kugundua makosa makubwa yaliyokuwepo kwenye shauri langu dhidi ya Serikali mkoani Dodoma kuhusiana na ajali ya gari mwaka 2008)
2. Ni kweli kuwa Cyril Chami (Mbunge wa Sasa) ni Ndugu yangu (Mjomba mdogo).
3. Si kweli kuwa nimeoa Mtoto wa kiongozi wa ccm huko Kilimanjaro. (Sijao bado)
....Naendelea kujibu mengine.

Inshaallah.. Ahsante kwa majawabu murua kabisa.
 
kuna huyu mtu wanamwita NICAS yeye ndo ananguvu zaidi huku moshi vijijin nadhan yeye ndo atampiga chini huyu bwana mdogo cyril chami
 
Huyu Malya kafundishwa ugaidi nchi Libya na baadhi ya nchi nyingine za kiarabu!!! Nina wasiwasi naye na kumwogopa kuliko SIMBA jike!!! Naomba fafanulia jamvi hili tukufu elimu yako uliisomea nchi gani na kwa fani ipi? Just curious to know ili angalau usafishe jina maana wengine tunakufahamu kwa mabaya.
 
Majibu mengine:

"Inadaiwa kuwa kuna watu waliokuwa 'Nyuma ya pazia' kwenye kesi ile (Ndiyo maana ilifunguliwa wilaya ya Dodoma Mjini badaya ya Kongwa)."

Binafsi sina majibu hapa Duniani. Mimi ni Binaadamu kama walivyo wengine. Pia mimi ni mgumu sana kuzungumza nisichokuwa na uhakuka nacho. Ikiwa wapo waliokuwa 'Nyuma ya pazia' kuzuia lengo langu 2010 (Japokuwa halikuwepo kiukweli) Nilishamwambia Mungu Ashughulike nao.

Kuna mdau hapo juu amesema kuwa 'Atapitishwa' Komu 2015. Naomba kumhakikishia kuwa CHADEMA na CCM ni tofauti kama ilivyo Jehanum na Mbinguni. Maamuzi ya CHADEMA huwa hayafanywi kama ya CCM!.. CHADEMA kuna viongozi, CCM kuna Watawala. Kuna taratibu za kumpata mgombea kwa mujibu wa katiba kwa maana hiyo hata kama nisipogombea/kutokupitishwa kwenye kura ya maoni bado nitakuwa na imani na Kiongozi atakayepitishwa. By the way bado tupo kwenye main road kuelekea M4C nadhani haya si vyema sana kujadili kiundani kwa sasa.

Sote ni ndugu, tatizo ni CCM!.
 
Alikuwa na udouble agent flani,upande wa pili ndo walimgeuka.Umemsahahu kaka yake ambaye ni ccm nadhani anaitwa samweli wangwe kama sikosei.Yeye alikataa hata uchunguzi wa ziada kwa mwili wa marehemu usifanyike.Na kulitokea mgogoro serikali ya ccm ikauteka mwili wa Wangwe RIP.Kumbuka kulikuwa na tetesi za yeye kupigwa risasi ya mdomo.

Wangwe, Samwel (Prof) ambaye kwa sasa ndiye Executive Director wa the former REPOA ni SSM damu. Na aligombea Kibaha mjini 2010 Koka akambwaga kwa kura ya maoni. Na ni mtu wa ..... kwa hivyo asingekubali mwili ufanyiwe uchunguzi maana ingeleta mzozo kwa waliohusika na mauaji yale na Deus Malya anafahamu fika kilichotokea maana yeye hakuumia japo gari lilikuwa nyang'anyang'a. Kitendawili kigumu sana kuhusiana na kifo cha Mpiganaji Chacha Wangwe.
 
Majibu mengine:
Inadaiwa kuwa kuna watu waliokuwa 'Nyuma ya pazia' kwenye kesi ile (Ndiyo maana ilifunguliwa wilaya ya Dodoma Mjini badaya ya Kongwa). Binafsi sina majibu hapa Duniani. Mimi ni Binaadamu kama walivyo wengine. Pia mimi ni mgumu sana kuzungumza nisichokuwa na uhakuka nacho. Ikiwa wapo waliokuwa 'Nyuma ya pazia' kuzuia lengo langu 2010 (Japokuwa halikuwepo kiukweli) Nilishamwambia Mungu Ashughulike nao.
Kuna mdau hapo juu amesema kuwa 'Atapitishwa' Komu 2015. Naomba kumhakikishia kuwa CHADEMA na CCM ni tofauti kama ilivyo Jehanum na Mbinguni. Maamuzi ya CHADEMA huwa hayafanywi kama ya CCM!.. CHADEMA kuna viongozi,CCM kuna Watawala. Kuna taratibu za kumpata mgombea kwa mujibu wa katiba kwa maana hiyo hata kama nisipogombea/kutokupitishwa kwenye kura ya maoni bado nitakuwa na imani na Kiongozi atakayepitishwa. By the way bado tupo kwenye main road kuelekea M4C nadhani haya si vyema sana kujadili kiundani kwa sasa.

Sote ni ndugu,tatizo ni CCM!.

dah ... mkuu upo makini

I wish you all the best
 
Hivi ndugu Deus F Malya unajibu maswali yote?ama ni ya kuhusu uchaguzi peke yake?maana hata miye nina maswali kadhaa.Naomba unijulishe kama utajibu maswali yanahusiana na ile ajali yako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom