Deus Kibamba: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Mkuu wa 2020 unaweza kushirikisha wapiga kura wachache kuliko chaguzi zote

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,571
Mwanaharakati huru Deusi Kibamba amesema figisu za uchaguzi zilianzia kwenye kura za maoni za CCM na wale waliopitishwa ndio " hao" wanaolazimishwa kupita bila kupingwa.

Kibamba amedai kuwa demokrasia ya Tanzania imegawanywa katika vipande viwili wale wanaoruhusiwa kufanya siasa na wale waliozuiwa na hii ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Mwisho mwanaharakati huyu anasema uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020 unaweza kuweka historia ya kuhusisha wapiga kura wachache zaidi kuwahi kutokea kwani wapiga kura halisi wamekatishwa tamaa.

Source BBC Dira ya Dunia
 
Mwanaharakati huru Deusi Kibamba amesema figisu za uchaguzi zilianzia kwenye kura za maoni za CCM na wale waliopitishwa ndio " hao" wanaolazimishwa kupita bila kupingwa.

Source BBC Dira ya Dunia
Kwani ni nani kamdanganya kuwa kutakuwa na uchaguzi? Huu utakuwa upikaji wa matokeo. Hakutakuwa na uchaguzi kabisa. Watu mtaendelea na majukumu yenu, Lakini jioni mtakuta matokeo yenye namba nzuri sana za asilimia 90. Hii yote kuonyesha kuwa anaabudiwa kama Mungu.
 
sehemu zingine hata hao ccm hawataenda kupiga kula mana mgombea wao tayari kesha pita bila kupigwa. Yaani sasa hivi wanasheherekea ushindi kabla hata kampeni hazijaanza!
 
Wanasubiri kuapishwa tu na baada ya muda kupewa dozi kwa ajili ya uchaguzi 2020.
 
Hilo lilikuwa wazi, maana wananchi wengi walisusia kujiandikisha. Wananchi wengi kwa sasa wanauelewa wa kutosha na hawako tayari kuingia kwenye siasa za kishenzi. Wabaki hao wala rushwa wagawane vyeo bila ridhaa ya umma wakati tunaandaa plan B.
Una ushahidi kuwa wananchi wengi walisusia kujiandikisha?!
 
Siku hizi hakuna uchaguzi, badala yake kuna uchafuzi....

DW
77414550_429484467740078_516728448588705826_n.jpeg
 
Mwanaharakati huru Deusi Kibamba amesema figisu za uchaguzi zilianzia kwenye kura za maoni za CCM na wale waliopitishwa ndio " hao" wanaolazimishwa kupita bila kupingwa.

Kibamba amedai kuwa demokrasia ya Tanzania imegawanywa katika vipande viwili wale wanaoruhusiwa kufanya siasa na wale waliozuiwa na hii ni hatari kwa ustawi wa jamii.

Mwisho mwanaharakati huyu anasema uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020 unaweza kuweka historia ya kuhusisha wapiga kura wachache zaidi kuwahi kutokea kwani wapiga kura halisi wamekatishwa tamaa.

Source BBC Dira ya Dunia
Mkakati wa aliye madarakani uchaguzi usifanyike watu wapite bila kupingwa.Huwezi ukakataza mikutano ya kisiasa halafu ukataka watu wakapige kura
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom