Deus Kibamba: Rais Kikwete alijaribu kwa Siri kubadilisha katiba ajiongezee mihula ya Urais ikashindikana.

.....smg dodoma.
Anaposema kisiri siri ana maanisha nini?
Ni vyema akafafanua vyema.

Yaliyopo sirini mwa marais wetu ni mengi na mengine ni baya kuliko tunavyodhani.
Sasa tuambiwe hayo ya sirini ya Kikwete.

Na siku Magu akitoka madarakani yale yote ya sirini aliyoyafanya tutaelezwa tu, ikiwemo lile la.........
 
Wewe ndio huwezi kuunganisha historia ya nyuma na mambo ya sasa, na ndio.maana hata mkisoma.maphd yenu hayawasaidii.....hili alilotwambia leo maana yake ni kubwa san, kwamba ccm haijaanza leo mbinu chafu za kubadilisha katiba kibabe
IQ yetu watanzania ipo chini sana. Sasa siri hii ina maana gani kwa sasa? Katiba inabadilishwaje kwa siri kwa mfano? Mungu tupe salama na generation hii ya wajinga.
 
Deus Kibamba Ana chuki nzito sana kwa Mh. Kikwete
Kwake Jk Hana Jema wala zuri!
Alipoingia JPM akaanza kusema si busara kumkosoa Rais hadharani, Sijui wakati ule anamkejeli Jakaya alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri
 
Habari zenu familia ya JF.
Niende kwenye mada hapo juu.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini, Deus Kibamba akihojiwa hivi punde na Radio DW Idhaa ya kiswahili ya Born Ujerumani, ktk kipindi cha Africa Wiki Hii, amesema Kikwete alijaribu kwa siri sana kuongeza mihula ya Urais lakini mpango wake wa kubadili kipengele hicho cha katiba ukashindikana.

Cha ajabu ni kuwa Kikwete alikuwa akidai kauchoka urais na anatamani muda wake uishe akapumzike. Hivi Kikwete kipindi kile angeibuka hadharani na kutangaza nia yake hiyo ya kutaka kuendelea na uongozi wa nchi hali ingekuwaje wakati huo?

Je kama Kikwete ndiye Rais hadi Leo tungekuwa na hali gani kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na maeneo mengine muhimu?
mbona mijadala mikali inakuja kwa wingi baada ya tukio la Lissu? Lengo ni kufifisha mjadala wa kushambuliwa kwa Lissu au imebidi tu ije?
 
Wewe ndio huwezi kuunganisha historia ya nyuma na mambo ya sasa, na ndio.maana hata mkisoma.maphd yenu hayawasaidii.....hili alilotwambia leo maana yake ni kubwa san, kwamba ccm haijaanza leo mbinu chafu za kubadilisha katiba kibabe
Mkuu usilinganishe mambo ya nyuma na haya madudu yanayoendelea. JK alisema bayana hana mpango wa kuongeza hata siku moja na ndivyo ilivyokuwa. Katiba yetu ni mbovu sana. Ni bahati huko nyuma tulikuwa tukipata marais wenye chembe za utu moyoni. Kasheshe pale inapokywa kinyume chake.
 
Mkuu usipende sana ku rely kwenye maneno ya hawa watu kwani huyu wa sasa yeye anaongea nini na anatenda nini?? Acts speaks louder than words
 
Anaposema kisiri siri ana maanisha nini?
Ni vyema akafafanua vyema.

Yaliyopo sirini mwa marais wetu ni mengi na mengine ni baya kuliko tunavyodhani.
Sasa tuambiwe hayo ya sirini ya Kikwete.

Na siku Magu akitoka madarakani yale yote ya sirini aliyoyafanya tutaelezwa tu, ikiwemo lile la.........
Malizia
 
kulikuwa kuna hoja ya kumuongezea muda ili asimamie mchakato wa katiba mara nyingi wanaoanzisha hayo mambo ni watu wanaonufaika na utawala uliopo
 
Hivi kumbe kweli
hawa watu wako awamu zote Nyerere angestaafu mapema ila kila siku walimwaminisha bila yeye nchi itayumba, wakati wa Mwinyi ilibidi Nyerere aingilie kati, wakati wa Mkapa, Kikwete na hata rais wa sasa kuna watu wana mawazo hayp ya kuongeza muda wa madaraka ili mradi waendelee kufaidika binafsi lakini system yetu ilishakataa mambo ya kuongeza muda
 
Back
Top Bottom