Deus Kibamba: Rais Kikwete alijaribu kwa Siri kubadilisha katiba ajiongezee mihula ya Urais ikashindikana.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,198
6,416
Habari zenu familia ya JF.
Niende kwenye mada hapo juu.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini, Deus Kibamba akihojiwa hivi punde na Radio DW Idhaa ya kiswahili ya Born Ujerumani, ktk kipindi cha Africa Wiki Hii, amesema Kikwete alijaribu kwa siri sana kuongeza mihula ya Urais lakini mpango wake wa kubadili kipengele hicho cha katiba ukashindikana.

Cha ajabu ni kuwa Kikwete alikuwa akidai kauchoka urais na anatamani muda wake uishe akapumzike. Hivi Kikwete kipindi kile angeibuka hadharani na kutangaza nia yake hiyo ya kutaka kuendelea na uongozi wa nchi hali ingekuwaje wakati huo?

Je kama Kikwete ndiye Rais hadi Leo tungekuwa na hali gani kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na maeneo mengine muhimu?
 
Anaposema kisiri siri ana maanisha nini?
Ni vyema akafafanua vyema.

Yaliyopo sirini mwa marais wetu ni mengi na mengine ni baya kuliko tunavyodhani.
Sasa tuambiwe hayo ya sirini ya Kikwete.

Na siku Magu akitoka madarakani yale yote ya sirini aliyoyafanya tutaelezwa tu, ikiwemo lile la.........
 
Naona kuna jaribio la kumchafua mstaafu, hivi unaweza kuongeza vipi muda na wasaidizi wake wasijue, Bunge linalotunga sheria lisijue na watanzania wasijue?
Wanasheria kama akina kibamba wanaweza kujibu hili swali ambalo hata mimi nakosa jibu lake!
 
Anaposema kisiri siri ana maanisha nini?
Ni vyema akafafanua vyema.

Yaliyopo sirini mwa marais wetu ni mengi na mengine ni baya kuliko tunavyodhani.
Sasa tuambiwe hayo ya sirini ya Kikwete.

Na siku Magu akitoka madarakani yale yote ya sirini aliyoyafanya tutaelezwa tu, ikiwemo lile la.........
Hata mi nimenshangaa Kibamba, anamanisha alitaka kubadili katiba kwa siri akianzia kwa watu wake wa Karibu, mpango ukashindikana.
 
Hata siamini, maana mchakato wa kubadili Katiba huanzia kwa Wananchi > Bungeni > Raisi.

Ukiona nchi inabadili katiba kupitia wananchi ujue hapo pressure ni kubwa. Lakini hapa kwetu ni rais na wabunge ndio wanaamua kubadili katiba.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom