Deus Gracewell Seif: The godfather of trade unions

Mar 14, 2015
85
105
Wakati Fulani unajiuliza Hawa watu aina ya Huyu bwana Deus Seif ambaye ni katibu mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania anatoa wapi Nguvu kubwa aliyonayo hata Leo hii aendelee kutesa na cheo alichonacho pamoja na tuhuma zote alizo nazo.

Bwana huyu tangu ameajiriwa na Chama Cha walimu akitoka kuwa Afisa elimu huko Geita amekua ni mtesi mkubwa mno dhidi ya yeyote aliye kinyume na yeye.

Mojawapo ya Viongozi walioonja machungu na Nguvu za Katibu mkuu huyu ni Wajumbe wa Kamati ya utendaji taifa kutoka mkoa wa Dar es Salaam ambaye baada ya kusimama kidete juu ya matumizi mabaya ya Mali za walimu hususani kwenye ununuzi wa sare za mei mosi aliundiwa zengwe Baya kupitia Baraza la mkoa wa Dar es Salaam na kumng'oa madarakani.

Bwana huyu amekua akituma Nguvu yake popote pale ambapo Kuna kiongozi mwenye msimamo ili atoke madarakani kiasi Cha kwamba chama Cha walimu kujaza chawa wengi mno ambao kazi yao ni kumtukuza na kupeleka majungu ili Deus awateue kuwa makatibu wa wilaya.

Bwana Deus huyu mpaka Sasa anayo kesi mahakamani ya matumizi mabaya ya Mali za walimu kwa kutumia fedha za walimu kwenda Cape Verde yeye na Mweka hazina Bwana Alawi lakini mpaka Leo wanadunda ofisini.

Mwezi June Baraza la wadhamini walimtimua Bwana Deus na kumtaka kukabidhi Mali za walimu kwao lakini kwa ujeuri mkubwa na Nguvu yake aliwapuuzia mbali na Leo hii wanaonja joto ya jiwe kutoka kwa Mtu waliyemwajiri wao wenyewe.

Bwana Deus ni mojawapo ya Viongozi wengi ambao Bado wanaaamini wanalindwa kwa maagizo kutoka juu mpaka Sasa akitumia Nguvu hiyo kuumiza wengine na kutengeneza hofu kubwa kwa walimu wenye njaa kali Sana.

Kubwa kuliko yote ni Leo hii hatimaye baada ya kukosana na Rais wa Chama Mwl Leah Ulaya ameitisha Baraza na kumtimua bosi wake ambaye kiutaratibu huchaguliwa na mkutano mkuu, Viongozi wengi wa Baraza la taifa walilipwa marupurupu yao mapema Sana ili kutimiza kilichotarajiwa na hatimaye Rais wa CWT Yuko nje ya ulingo huku mtendaji mkuu wa Chama akitesa madarakani pamoja na kesi Zake TAKUKURU.

Yaani Rais wa CWT anatimuliwa na Baraza kwa kesi ya kutowasemea walimu wakati mtendaji mkuu anaendelea kutesa pamoja na kesi za matumizi mabaya ya Mali za walimu na kuwavalisha walimu sare za mei mosi siku ya nanenane.

Viongozi wote wa CWT taifa ni zao la ubatili wa kupachikwa ili kunyamazisha kundi kubwa l watumishi kiasi Cha walimu kulimia meno kwa muda mrefu huku asilima mbili za mishahara yao ikitumiwa na kina Deus kwenda matembezi Cape Verde na kupiganisha vita za madaraka.

Wito wangu ni Serikali kuiangalia CWT Sasa kwa making kwani imekua si mtetezi Tena wa walimu na bwana huyu Deus amekua ni Mungu mtu ndani ya chama kiasi Cha kutia shaka nani yupo nyuma yake awamu hii ya sita. Leo hii amemtimua Rais wake kesho hawezi shindwa kuuza Mali yoyote ya chama na akanyamaziwa kwa vile Ana watu nyuma yake

Kadhalika walimu wapunguze njaa, unafki, ukuda na uzandiki wakumbuke yapo maisha baada ya laki 5 wanazopewa kuumiza wenzao kwenye uongozi.

Mama Samia mtazame Deus,Alawi,Dinna na wenzao wote ni sumu,kupe na mchwa wabaya Sana katika Vyama vya wafanyakazi.

Alamsikh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom