CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,920
Huyu Bashe si sio raia sasa ana work na resident permits? Hiyo kazi haiwezi kufanywa na Mtanzania mapaka foreigner aifanye?
Hivi huyu Bashe ndiye yule aliyegombea ubunge wa CCM Nzega,?
Watanzania tuna tatzo la kutokujua magazeti yepi ya kusoma kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavyo ...wana JF tunaomba mtoe elimu hii kwa wasomaji wetu
Rweye, kwa vile nawe ni mwana JF na umegundua Watanzania tuna tatizo la kutokujua magazeti yepi ya kusoma kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavyo, hivyo kuwaomba wana JF kutoa elimu hii kwa wasomaji wetu, ningekuomba tuanzie na wewe kutuelimisha ni magazeti yepi ya kusoma kwa faida ya yetu na vizazi vijavyo?.
Mwananchi
The citizen
Raia Mwema
MwanaHalisi
Guardian
Daily News ( kama sio wakati wa kampeni za uchaguzi )
Kulikoni
Tanzania Daima
Nipashe.
Kama wewe ni mpenda mabadiliko chanya ya kweli, anza Jumatano ijayo kusoma gazeti la Raia Mwema. Lina uchambuzi wa upeo mkubwa wa masuala katika kupigania mabadfiliko chanya kupitia kwa waandishi wenye weledi mkubwa wa fani.Katika misingi ya kimabadiliko chanya naweza nikasema bila kusita sita kwamba kwa sasa gazeti hilo la kina Jenerali Ulimwengu, Johnson Mbwambo,John Bwire, Francis Chirwa na wengine liko juu mno positively kimabadiliko.Prove that yourself.Hapo umenena! Ila hayo yenye Red siyaamini amini vile? Raia Mwema sijawahi hata kulisoma. Daily News sidhani maana linamilikiwa na Serikali ya Mafisadi haliwezi kututendea haki wa-TZ ila unaweza kulinunua na kukimbilia kwenye ukurasa wa matangazo ya nafasi za kazi tu basi!
Zamani nilikuwa mpenzi sana wa magazeti ya Habari Corporation lakini tangu yameuzwa sina hamu nayo kabisa wala sikumbuki kama huwa najishughulisha hata kusoma vichwa vya habari kwa wauza magazeti!!!
Nafikiri hayo magazeti ya Fisadi Mkuu tukiyasusia atafunga kampuni ya magazeti. Tunaomba siku moja apatikane mtu wa kutuhamasisha kufanya mgomo.
Mtoa mada unatakiwa kupewa semina ili ujuwe jinsi ya kuyatambuwa magazeti huru, hivi wewe na akili zako timamu Habari corpotion ndio inayomiliki gazeti la Mtanzania, na hiyo kampuni ni mali Fisadi Rostam Aziz, wewe unategemea habari gani yenye maslahi ya Taifa kutoka kwenye media hiyo? na ni kwa nini unaendelea kununuwa magazet hayo ili hali huku ukijuwa unazidi kumtajirisha huyu Jambazi Rostam Aziz?