Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?


Pearl

Pearl

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2009
Messages
3,042
Likes
46
Points
135
Pearl

Pearl

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2009
3,042 46 135
You celebrate it, you enjoy it - but have you ever wondered what is Christmas? Calling you friends and families over for delectable meals, exchanging gifts by the side of beautifully adorned trees, this is what we comprehend of the Christmas holidays.

But what exactly is this widely celebrated time of the year all about?

What is Christmas?
When it comes to discussing the origins of Christmas, many theories have been brought forward claiming one thing or the other about Christmas. The widely-believed theory suggests that Christmas has been with us for over 4,000 years and celebrations similar to that of Christmas took place even before the birth of the Christ child.

Although Christmas is celebrated on December 25 every year, About Christmas it has been said that Jesus was in fact born in the spring. Well, you get it right - there are a lot of contradictory statements associated with the origins of Christmas.

But this doesn't really hamper the meaning of Christmas. Christmas is about celebrating the birth of the Lord Jesus while coming together with your friends and family and bonding with one another. The religious meaning of Christmas, however, has been declining slowly.

These days, it's more of commercialism associated with the holidays. People flocking at Target and Wal-mart stores with shopping carts full of gifts and ornaments are a common sight. Have we become more inclined to the commercial aspect of the holidays? It is important that the tradition of family bonding associated with the Christmas holidays continues forever and the essence of Christmas stays among us.

Your opinion please is needed.!
HISTORIA FUPI YA KRISMASI.

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii.


Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".

Historia ya Krismasi
Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni waWayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.


Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.

Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200. Mwandishi MkristoKlemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.

Labda kadirio la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.

Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Krismasi na sikukuu ya Sol Invictus

Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kuchukua nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika").

Lakini pengine mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari walianzisha sikukuu hiyo, halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili kushindana na Ukristo uliokuwa bado chini ya dhuluma ya serikali yao.

Aliyeingiza sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" (Mitra) huko Roma ni Eliogabalus (kaisari kuanzia 218 hadi 222). Baadaye Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273, hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba.

Wakati wa Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba.

Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo.

Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki na sehemu ya Waprotestanti naWaorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katikakalenda.

Habari za Krismasi katika Biblia

Habari za Krismasi kama sherehe hazipatikani katika Biblia kwa sababu zilizotajwa hapa juu.

Lakini hasa vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo na Luka.

Mathayo anasimulia habari hizo katika mlango wa kwanza kuanzia aya 18 na katika mlango wa pili.

Bikira Maria alipata mimba wakati alipokuwa mchumba wa Yosefu. Yosefu alitaka kumwacha lakini aliambiwa na malaika aanze kuishi naye na kumkubali mtoto kama wake kwa kumpa jina "Yesu".

Mamajusi kutoka mashariki waliwatembelea na kuwaletea zawadi kwa sababu waliona nyota ya pekee iliyokuwa kwao alama ya kuzaliwa kwa mfalme mpya katika Uyahudi ikawaongoza hadi Yerusalemu. Lakini walipompitia mfalme Herode Mkuu, huyo alikasirika akimwogopa mfalme mpya. Hata hivyo aliwaelekeza Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.

Yosefu alipata tena ujumbe kutoka kwa malaika akaondoka na mtoto na Maria kukimbilia Misri kabla ya askari wa Herode hawajaweza kumuua Yesu.

Baada ya kifo cha Herode walirudi kutoka Misri lakini hawakuenda tena Bethlehemu bali kuhamia Nazareti katika mkoa wa Galilaya.
Katika Injili ya Luka


Katika taarifa ya Luka (mlango wa 1 na 2) Maria alipokea huko Nazareti ujumbe wa malaika mkuu Gabrieli kwamba atapata mimba na mtotowa pekee.

Yosefu na Maria walikwenda Bethlehemu kwa sababu ya sensa iliyowataka kwenda katika mji asili wa ukoo wa Yosefu. Hapo Yesu alizaliwa katika hori la kulishia wanyama; wachungaji mabondeni walitangaziwa na malaika habari hiyo wakaja kumwona mtoto.

Baada ya kuzaliwa wazazi walimpeleka Yesu Yerusalemu katika hekalu kufuatana na sheria ya Agano la Kale (Kitabu cha Kutoka 13,2; 13,15) halafu wakarudi kwao Nazareti.

Kama kawaida, imani na liturujia ya Kikristo zinaitikia haja za binadamu.

Mojawapo ni kukutana na watu wa kupendeza kwa wema wao.

Kipindi cha Noeli kinatimiza haja hiyo, kwa kuwa kinaadhimisha kuzaliwa kwa mtu mpya kabisa ambaye anatuvutia kwa wema wake na ambaye tukimuona tumemuona Mungu, tena tukimpokea tunazaliwa upya kama wana wa Mungu.

?Leo amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana?.

Tunapoadhimisha Noeli tangazo hilo la malaika kwa wachungaji linatufikia sisi. Si kujidanganya, kana kwamba Yesu angezaliwa leo, wala hatukumbuki tu tukio la zamani, bali fumbo la kuzaliwa Bwana linatufikia leo katika liturujia na kutuletea neema zake. Hivyo tunaweza tukazaliwa upya kwa kushiriki kuzaliwa kwa kichwa chetu.

Liturujia inashangilia hivi, ?Lo! Mabadilishano ya ajabu! Mwana wa Mungu anakuwa mtu kusudi mtu awe mwana wa Mungu!?. Tena si binadamu tu, bali viumbe vyote vinapata heshima mpya kwa Neno wa milele kujifanya kiumbe.

Desturi za Krismasi
Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo.


1. Pango la Noeli:
- Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio (Italia) na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa.


2. Mapambo ya krismasi:
- Ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemuinawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka.


3. Mti wa Krismasi:
- Ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kamamwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi.


4. Zawadi za Krismasi
- Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2.


Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira.

4. Baba Krismasi / Baba Sara Noeli
(Chanzo cha habari hii ni WIKIPEDIA)
Kuhusu Pango la Noeli, Baba Krismasi (Father Christmass), pamoja na baadhi ya mapokeo si Wakristo wote wanakubaliana na hayo mapokeo ingawa wengi huadhimisha kwa kukukumbuka kuzaliwa kwake Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu.
Je! Nini hasa maana ya siku hii katika maisha yetu ya leo?


Krismasi maana yake ni ishara ya wokovu wa mwanadamu. Krismasi haimaanishi kula, kunywa, kuvimbewa, wala kupumzika majumbani pamoja na familia zetu. Krismasi - Ibada ya Yesu (kuzaliwa kwa Bwana Yesu) ni ishara ya WOKOVU kwa wanadamu. Krismasi ni ishara ya UKOMO WA DHABIHU ZA WANYAMA ambao walitumika kuleta utakaso kwa watenda dhambi. Krismasi ni ishara ya UPENDO MKUU wa Mungu kwa watu wake waliopotea; kwa maana amewapatia msamaha wa dhambi bure. Krismasi ni ishara ya ushindi dhidi ya Shetani na majeshi yake kwa maana Yesu ni Bwana wa mabwana, Jemedali wa vita, Mungu mwenye nguvu, Mungu wa miungu, Mfalme wa amani, na Ndiye Alfa na Omega, Mweza wa yote.

Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye..." - Yn 3:16-17


Kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni ishara ya WOKOVU katika maisha yetu sisi tumwaminio. Japokuwa tarehe rasmi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa uhakika; bali jambo la muhimu ni kufahamu kuwa Bwana Yesu alizaliwa ili atuokoe sisi wanadamu na kuturejeshea uhusiano mwema kati yetu na Mungu wetu.

Habari hizi za wakovu tunazipata kwa wale wachungaji waliotokewa na malaika wa Mungu na kuwaambia kwamba:
"...leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana." - Luka 2:11.


Yesu ni Mwokozi wetu; Wokovu huu maana yake ni UTAKATIFU, UZIMA, USHINDI, AFYA, UTAJIRI, MAFANIKIO, NGUVU, UTAWALA, na kila jema litokalo kwa Bwana Mungu ni letu kupitia utakaso wa damu ya Yesu Kristo. Amekuja kutuokoa na kutupatia uzima wa milele. Kama wewe haujampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako; kamwe usiache nafasi hii ikupite bure. Tamka maneno haya machache yanayobadirisha maisha yako tangu utakapoyakiri kwa kinywa chako kwa imani.

Sema;
"Bwana Yesu, nakuhitaji katika maisha yangu. Pekeyangu mimi pasipo Wewe siwezi kuishi maisha yampedezayo Mungu. Yesu naomba tangu sasa uwe Bwana na Mwokozi wangu, nisamehe dhambi zote nilizozitenda, naomba unitumie kwa ajili ya utukufu Wako; tangu sasa na siku zote daima. Asante Yesu kwa kuniokoa. Amina."


Sala hiyo fupi imekufanya uwe mwana wa Mungu. Kwako wewe uliyeamini na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako tangu sasa katika jina la Yesu Kristo. Amen.

Nakutakia sikukuu njema ya Krismasi, Yesu azaliwe ndani yako na mapenzi ya Mungu yatimie kwako, katika jina la Yesu Kristo.

Amina
 
ismase

ismase

Senior Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
116
Likes
1
Points
33
ismase

ismase

Senior Member
Joined Feb 12, 2010
116 1 33
Chrismas haina maana yeyote. kwanza Yesu hakuzaliwa tar 25 kihistoria wala kimaandiko. kama mtu ana ushahidi alete hapa jukwani.
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,395
Likes
38,573
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,395 38,573 280
Pear.... nakuaminia mwana wane.
Nimekuchapa na MULULU wa thanks hapo juu.
 
Pearl

Pearl

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2009
Messages
3,042
Likes
46
Points
135
Pearl

Pearl

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2009
3,042 46 135
yanini malumbano ya nini maneno?tuelimishane na kufundishana
Chrismas haina maana yeyote. kwanza Yesu hakuzaliwa tar 25 kihistoria wala kimaandiko. kama mtu ana ushahidi alete hapa jukwani.
 
J

J Lee

Member
Joined
Dec 14, 2010
Messages
60
Likes
1
Points
0
J

J Lee

Member
Joined Dec 14, 2010
60 1 0
historia haionesh kwamba yesu alizaliwa 25 Dec bblia ndo ktabu cha iman ya kikristo kakin haielekez kuwepo kwa christmas, inasikitisha sana kuona jins tunavyo fuata mkumbo ktk hli suala.
 
msomi_wa_zamani

msomi_wa_zamani

Member
Joined
Nov 27, 2010
Messages
17
Likes
0
Points
0
msomi_wa_zamani

msomi_wa_zamani

Member
Joined Nov 27, 2010
17 0 0
Christmas Day[is a holiday observed generally on December 25th to commemorate the birth of Jesus, the central figure of Christianity.The date is not known to be the actual birthday of Jesus, and may have initially been chosen to correspond with either the day exactly nine months after some early Christians believed Jesus had been conceived,[9] the date of the winter solstice on the ancient Roman calendar,[10] or one of various ancient winter festivals.

notes: Lying is modus operandi of any religion,then why do we celebrate Christmas on December the 25th.


The History of Christmas
Christmas on the Net - The History of Christmas
Christmas - Wikipedia, the free encyclopedia
 
K

Kivia

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
278
Likes
8
Points
35
K

Kivia

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
278 8 35
Je X-mass ni sherehe za kuzaliwa yesu kristo ? Nielewavyo gregorian calenda ilianza pale yesu alipozaliwa yaani tareh 01-januari - 01. Sasa ninapoambiwa tunasherehekea kuzaliwa yesu tar 25 -Dec, inachanganya kidogo.[au tarehe kamili ya kuzaliwa yesu haifahamiki ?] Wapendwa naomba msaada hapo na bwana asifiwe.
 
Good Guy

Good Guy

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
4,547
Likes
126
Points
160
Good Guy

Good Guy

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
4,547 126 160
This is a joke forum and i dont c anything funny right there!
 
hashycool

hashycool

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2010
Messages
6,347
Likes
1,303
Points
280
hashycool

hashycool

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2010
6,347 1,303 280
Je X-mass ni sherehe za kuzaliwa yesu kristo ? Nielewavyo gregorian calenda ilianza pale yesu alipozaliwa yaani tareh 01-januari - 01. Sasa ninapoambiwa tunasherehekea kuzaliwa yesu tar 25 -Dec, inachanganya kidogo.[au tarehe kamili ya kuzaliwa yesu haifahamiki ?] Wapendwa naomba msaada hapo na bwana asifiwe.
is this suppose to be a joke?........its in the jokes forum dude!
 
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,816
Likes
139
Points
160
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,816 139 160
Je X-mass ni sherehe za kuzaliwa yesu kristo ? Nielewavyo gregorian calenda ilianza pale yesu alipozaliwa yaani tareh 01-januari - 01. Sasa ninapoambiwa tunasherehekea kuzaliwa yesu tar 25 -Dec, inachanganya kidogo.[au tarehe kamili ya kuzaliwa yesu haifahamiki ?] Wapendwa naomba msaada hapo na bwana asifiwe.

Very poor question. When was this calendar started? Why is this year 2010?

Kama wewe ni wale wafuasi wa Allah kiumbe,

Je, Issa bin Mariam aliye ndani ya kolani, na kutokana na Kolani ya Allah wa Isilamu, huyu Issa bin Mariam alizaliwa tarehe gani? Naomba aya kutoka Kolani yenu.
 
Omukuru

Omukuru

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
244
Likes
2
Points
35
Omukuru

Omukuru

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
244 2 35
Je X-mass ni sherehe za kuzaliwa yesu kristo ? Nielewavyo gregorian calenda ilianza pale yesu alipozaliwa yaani tareh 01-januari - 01. Sasa ninapoambiwa tunasherehekea kuzaliwa yesu tar 25 -Dec, inachanganya kidogo.[au tarehe kamili ya kuzaliwa yesu haifahamiki ?] Wapendwa naomba msaada hapo na bwana asifiwe.
The post is in the wrong place, but I'll try to answer in a very short way.
Christmas is not Jesus' birthday. It is the Christian feast to celebrate and commemorate the event of the birth of Jesus Christ, the date, just like any calender is conventional.
Revise your history, you will see that the gregorian calender doesn't begin when "Jesus was born" (do your homework especially about the error margin). [Just for curiousity, as a msabato, which "Bwana" do you refer to when you write "Bwana asifiwe"?]
 
X-PASTER

X-PASTER

Moderator
Joined
Feb 12, 2007
Messages
11,649
Likes
133
Points
160
X-PASTER

X-PASTER

Moderator
Joined Feb 12, 2007
11,649 133 160
Je X-mass ni sherehe za kuzaliwa yesu kristo ? Nielewavyo gregorian calenda ilianza pale yesu alipozaliwa yaani tareh 01-januari - 01. Sasa ninapoambiwa tunasherehekea kuzaliwa yesu tar 25 -Dec, inachanganya kidogo.[au tarehe kamili ya kuzaliwa yesu haifahamiki ?] Wapendwa naomba msaada hapo na bwana asifiwe.
Kyonda, kwa faida yako hapa huta pata majibu ya kiistarabu, kama ulivyo ona hapo juu... ! Kuhusu hii sherehe si sikukuu ya kuzaliwa Yesu wala Yeheshua, wahusikia waliipanga tu, wala huwezi kuipata kwenye Biblia.
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Kyonda, kwa faida yako hapa huta pata majibu ya kiistarabu, kama ulivyo ona hapo juu... ! Kuhusu hii sherehe si sikukuu ya kuzaliwa Yesu wala Yeheshua, wahusikia waliipanga tu, wala huwezi kuipata kwenye Biblia.
Kwenye Quran nabii wenu Issa imeandikwa amezaliwa lini?
 
Kipala

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Messages
3,562
Likes
98
Points
145
Kipala

Kipala

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2009
3,562 98 145
Xmas ni sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu si siku ya kuzaliwa kwake - sawa na sikuukuu ya kuzaliwa kwake Malkia wa Uingereza (Queens birthday) inayosheherekewa tarehe iliyochaguliwa - kwa hiyo si tukio la ajabu kusheherekea siku tofauti.

Kwa malkia siku nyingine ilichaguliwa kwa sababu kwenye hali ya hewa ya Uingereza sherehe na maandamano ni afadhali kuwa mwezi usio na mvua nyingi (June).

Kwa Yesu sababu yake ni hakuna anayejua tarehe ya kuzaliwa kwake. Katika utamaduni wake watu hawakujalitarehe ya kuzaliwa na hakuna aliyekumbuka. Yesu hakuwana sherehe ya aina hii. Lakini Wakristo wa baadaye waliona ni mhimu kusherekea siku ya kuzaliwa kwake walichagua tarehe.

Si desturi katika Ukristo pekee. Waislamu wengi duniani wanasheherekea maulidi ya nabii Muhamad - lakini hakuna anayejua tarehe ya kuzaliwa kwake. Tarehe hii ilichaguliwa pia.
Hakuna ubaya - tusheherekee!
Heri za Krismasi!
 
Kipala

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Messages
3,562
Likes
98
Points
145
Kipala

Kipala

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2009
3,562 98 145
Kwa wote wanaosikitika mada hii kujadiliwa wenye uwanja wa mizaha basi hapa faraja kidogo naleta k/p kutoka Christmas eve Jokes


What did Adam say on the day before Christmas ?
It's Christmas, Eve !
How do you make an idiot laugh on boxing day ? Tell him a joke on Christmas Eve !

What do you have in December that you don't have in any other month ?

The letter "D" !

What does Father Christmas suffer from if he gets stuck in a chimney ?
Santa Claustrophobia !

What do you call a letter sent up the chimney on Christmas Eve ?
Black mail !

Who delievers cat's Christmas presents ?
Santa Paws !
Why does Father Christmas go down the chimney ?
Because it soots him !

Who delievers elephants's Christmas presents?
Elephanta Claus !
 
X-PASTER

X-PASTER

Moderator
Joined
Feb 12, 2007
Messages
11,649
Likes
133
Points
160
X-PASTER

X-PASTER

Moderator
Joined Feb 12, 2007
11,649 133 160

Very poor question. When was this calendar started? Why is this year 2010?

Kama wewe ni wale wafuasi wa Allah kiumbe,

Je, Issa bin Mariam aliye ndani ya kolani, na kutokana na Kolani ya Allah wa Isilamu, huyu Issa bin Mariam alizaliwa tarehe gani? Naomba aya kutoka Kolani yenu.
Mkristo mwezio anakuuliza unakwenda kuutukana Uislam, wapi na wapi...!
 

Forum statistics

Threads 1,235,630
Members 474,678
Posts 29,229,177