Desemba 1, 2021: Siku ya UKIMWI Duniani

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,701
Leo trh 1/12 ni maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani, kwa Tanzania maadhimisho hayo yatafanyika katika Mkoa wa Mbeya.

Zaidi ya miaka 40 sasa tangu ugonjwa huu hatari uibuke, hadi sasa Ukimwi hauna dawa wala kinga.

UKIMWI umeendelea kuwa ugonjwa hatari zaidi duniani kuliko ugonjwa wowote ule.

Kundi ambalo limeathirika na Ukimwi ni rika la vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 49, wasichana ndio kundi lililo athirika zaidi.

Mikoa hatari ambayo inamaambukizi makubwa ya Virusi vya Ukimwi ni;

Njombe, Iringa, Mbeya, Mwanza, Kagera, Katavi, Shinyanga, Songwe, Ruvuma, Pwani, Tabora, Tanga, Dodoma na Geita.

hiyo ndio Mikoa inayo ongoza kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya UKIMWI.

wanao ishi kwenye mikoa hiyo chukueni tahadhari ili kuepuka Maradhi haya hatari.

Tuchukue tahadhari Ukimwi unauwa.

Twendeni TUKAPIME tujue hali zetu.
 
Kuwa makini sana unapo tembelea mikoa hii,
ukimwi upo nje nje ;
wataalamu wanasema Virusi vilivyopo ktk mikoa hii ni hatari zaidi kuliko.
Njombe, Iringa, Mbeya, Mwanza, Kagera, Katavi, Shinyanga, Songwe, Ruvuma, Pwani, Tabora, Tanga, Dodoma na Geita.
 
kwa nini VIONGOZI wetu Hawataki kupima VVU HADHARANI? ili kuonyesha mfano mzuri kwa wananchi.
 
Kuwa makini sana unapo tembelea mikoa hii,
ukimwi upo nje nje ;
wataalamu wanasema Virusi vilivyopo ktk mikoa hii ni hatari zaidi kuliko.
Njombe, Iringa, Mbeya, Mwanza, Kagera, Katavi, Shinyanga, Songwe, Ruvuma, Pwani, Tabora, Tanga, Dodoma na Geita.
Bila shaka utakuwa Dar.
Ukimwi uko popote hata ndani mwako.
 
ARV zinachangia zaidi maambukizi ya UKIMWI...ni bora hali ingebakia vilevile ili kila muathirika atambulike ili kupunguza maambukizi mapya.
 
Mama LETICIA MAURENCE KAPELA ambaye ni Mwenyekiti wa wanao ishi na Ukimwi ni mfano mzuri sana kwa wanawake Majasiri.
Safi sana mama Leticia....wanawake wwngine fuateni nyayo.
 
sijui nikapime leo.
Jumamosi nilitaka kwenda kupima pale hospital ya parestina.nikaambiwa wale wa kupima bure hawajaja nilishukuru.
Akaniambia nikapime kwa dokta.nikaona ujinga huu.yaani nitoe hela kupima ukimwi hela yangu alafu nikutwe nao
Mi sipimi ng'o
 
Back
Top Bottom