Desecration of the Dead: A criminal offense in our law

Is it possible that more Tanzanians have died at the hand of the State up to this time than during Mkapa's twIo terms.?


Wanasheria watusaidie katika hili jamani halifai kufumbia macho kwani nchi nzima itaonekana hakuna watu au kuonekana hatujui kitu.
Akina Kiwanga na rafiki yangu Harold Sungusia ondoeni hii aibu kwa kuitolea tamko la sivyo mipaka na miiko na utu umekiukwa kwa kiwango kisichotamkika.

Polisi siyo tu wamejiweka juu ya kila sheria lakini wamedharau watanzania kwa kufanya uhalifu ambao haujawahi fanywa mahali popote duniani.

Mbona ndugu wa marehemu katika nchi zenye vurugu kama Libya, yemeni, Syria, Bahrain n.k huruhusiwa kuchukua miili ya ndugu zao iweje hapo Tarime Polisi waingilie hili zoezi nyeti kwa wafiwa?
 
Hivi kweli nyie ndio GREAT THINKERS? Inafurahisha sana. Non sense.
 
Kikwete akifa kama nipo hai maiti yake nitaitemea mate na kama jeneza lake litapelekwa kwao kwa gari nitalipiga manati jeneza lake. Hii ni yamini yangu dhidi ya kikwete kwa kile alichowafanyia ndugu zangu wa mara

Non sense.
 
It is totaly true, Mwanakijiji it is now a high time for Tanzanian to rise their voices so the afforementioned official should step down and walk away from Public offices. Enough you have killed our brothers and sister! Imetosha
 
Hii nchi haitawliki tena,KIKWETE na jeshi lake hawawezi kutupa miili ya watu,kikwete kaonyesha waziwazi kuwa hawapendi wakristo,NCHI HAITAWALIKI TENA.
 
Kikwete akifa kama nipo hai maiti yake nitaitemea mate na kama jeneza lake litapelekwa kwao kwa gari nitalipiga manati jeneza lake. Hii ni yamini yangu dhidi ya kikwete kwa kile alichowafanyia ndugu zangu wa mara

Hawa ndugu zako walivyovamiana na kuua watu 17 wa familia tatu ndugu kule Buhare Musoma nayo ilikuwa order ya Kikwete? Au dini yenu inaruhusu watu kuuana kwa kuchinjana?
 
For whatever happened in Tarime overnight calls for condemnation for the police force lacking the sense of irony by expressing that some people were preventing the relatives to pick up the bodies of their loved ones only for them, police, to throw away the same bodies. The Tarime/Rorya special zone commander making cogent remarks that seem favorable to the helmsman who allowed himself to commit ethico-intellectual suicide.
 
Hii nchi haitawliki tena,KIKWETE na jeshi lake hawawezi kutupa miili ya watu,kikwete kaonyesha waziwazi kuwa hawapendi wakristo,NCHI HAITAWALIKI TENA.
 
Mimi sijaona point ya kuleta uhusiano kati ya urais wa kikwete na udini kwa hao maiti.kama una chuki binafsi sema.
 
poleni wapiganaji wenzetu wana tarime kwa janga hili tuliloletewa na kiongozi wetu mk were.Ila iko siku inakuja atasema maneno haya mbele ya Ocampo kiboko ya hawa viongozi wa afrca wavivu wa kufikiri
 
Something gotta give, thats all i can say to this creature calling themselves humans. Even though wameonesha kidogo ITV the images of the coffins by the side of the road are very strong and sad, Watanzania tumeona na inatia uchungu aise. Something gotta give

Mungu awabariki
 
Kikwete akifa kama nipo hai maiti yake nitaitemea mate na kama jeneza lake litapelekwa kwao kwa gari nitalipiga manati jeneza lake. Hii ni yamini yangu dhidi ya kikwete kwa kile alichowafanyia ndugu zangu wa mara

Kwani jk ndiye aliyeamuru maiti zikatolewe mortuary? Cha msingi hapa awawajibishe walioamuru maiti zitolewe na sio kumtupia rais hata lawama za wengine.
 
Ehud;Kikwete akifa kama nipo hai maiti yake nitaitemea mate na kama jeneza lake litapelekwa kwao kwa gari nitalipiga "4"]manati jeneza lake. Hii ni yamini yangu dhidi ya kikwete kwa kile alichowafanyia ndugu zangu wa mara
MPG;2013225]Hii nchi haitawliki tena,KIKWETE na jeshi lake hawawezi kutupa miili ya watu,kikwete kaonyesha waziwazi kuwa hawapendi wakristo,NCHI HAITAWALIKI TENA
Busara na hekima zitangulizwe ili zitusaidie kuelekea kwenye ukweli ili tofauti kati ya busara na kukosekana ionekane. The above kind of interjections is uncalled for, please don't adulterate this thread,personalize or take it out of context.

Kilichotokea ni mwendelezo wa yale mauaji yasiohojika.
Kifo cha raia hufanyiwa inquest lakini ni nadra kwa Tanzania. Ni mazoea hayo yanayopelekea viongozi kutoogopa maisha ya wanadamu. Gongola mboto, mbagala yamekwisha bila mtu kuwajibika na inaonekana kama ndio utamaduni. Wananchi wafike mahali na kusema hapana, tushinikize utamaduni wa kujiuzulu.

Bila kujali sababu za kifo, marehemu anastahili heshima zake bila kujali cheo,wadhifa au utajiri.
Kutupa maiti kwa yoyote yule afanyaye ni 'moral decay' ya hali ya juu.
Viongozi wanapokuwa mstari wa mbele kwenye mazishi na kudharau mazishi ya raia wengine ni ubaguzi, unafiki na dharau. Tuwaambie tumechoka!
 
Which prophets have been killed?



Redemption Song lyrics

Old pirates, yes, they rob I
Sold I to the merchant ships
Minutes after they took I
From the bottomless pit
But my hand was made strong
By the hand of the almighty
We forward in this generation
Triumphantly
Won't you help to sing
These songs of freedom?
'Cause all I ever have
Redemption songs
Redemption songs
Emancipate yourselves from mental slavery
None but ourselves can free our minds
Have no fear for atomic energy
'Cause none of them can stop the time
How long shall they kill our prophets
While we stand aside and look? Ooh
Some say it's just a part of it
We've got to fullfil the book

Won't you help to sing
These songs of freedom?
'Cause all I ever have
Redemption songs
Redemption songs
Redemption songs
Emancipate yourselves from mental slavery
None but ourselves can free our mind
Woh, have no fear for atomic energy
'Cause none of them-a can-a stop-a the time
How long shall they kill our prophets
While we stand aside and look?
Yes, some say it's just a part of it
We've got to fullfill the book
Won't you help to sing
These songs of freedom?
'Cause all I ever had
Redemption songs
All I ever had
Redemption songs
These songs of freedom
Songs of freedom
 
Hii nchi haitawliki tena,KIKWETE na jeshi lake hawawezi kutupa miili ya watu,kikwete kaonyesha waziwazi kuwa hawapendi wakristo,NCHI HAITAWALIKI TENA.

Mbona wakistro ni wengi sana katika ofisi za serikali na inawezekana walirusha risasi kuuwa hao ndugu zetu ni pia Wakistro! hata RPC wa Tarime Bwana Massawe ni Jambazi sugu ni Mkistro.

Sidhani kama hili swala ni la udini Bwana mdogo husichanganye mada hapa. Waziri Mkuu ni Mkistro amechukua hatua gani kulingana na hayo mawazo yako!
 
Kitendo cha kuiba maiti na kuzitupa bara barani kilichofanywa na jeshi la polisi ni cha KISHENZI na kilaaniwe na watanzania woote waliostaarabika na wenye kuheshimu haki za binadamu.Inasikitisha kuwa baadhi ya wachangiaji wanaleta hoja za udini jambo ambalo ni sumu kwa umoja wa kitaifa na faraja kwa watawala dhalimu kama JK na genge lake.JK alaumiwe kwa madaraka yake kama rais na amiri jeshi mku kwa kushindwa kuwawajibi makamanda wake wanaotoa amri za kishenzi kama hizi kwa askari wao.JAMANI TUSISHABIKIE UDINI ULIOASISIWA NA JK ILI CCM IENDELEE KUTUTAWALA NA KUTUUA KAMA ILIVYOTOKEA NYAMONGO.ALAANIWE JK,ILAANIWE CCM NA LILAANIWE JESHI LA POLISI.
 


Polisi wadaiwa kupora maiti Tarime


* WADAIWA KUVAMIA MOCHWARI USIKU
Waandishi Wetu

POLISI Kanda Maalumu ya Tarime, wanadaiwa kuvamia chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Mara kuchukua maiti za watu wanne waliouawa katika tukio la uvamizi wa Mgodi wa Nyamongo na kuziweka chini ya ulinzi.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa tukio hilo lilikwenda sambamba na kukamatwa kwa watu 12 wakiwemo wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Waliokamatwa katika tukio hilo ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Matiko. Wengine ni kada wa Chadema, Waitara Mwita na wakazi wengine sita wa Tarime ambao majina yao hayakupatikana mara moja.

Chanzo kimoja cha habari kilisema jana kwamba watu hao walikamatwa majira ya saa 3:23 juzi usiku baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi eneo la chumba cha kuhifadhia maiti kuwatawanya watu waliojitokeza kuzuia polisi kuchukua miili ya marehemu usiku huo.

Taarifa zilisema kuwa mbali na watu hao kukamatwa juzi, jana majira ya saa 4:30 asubuhi waandishi wa habari watatu; Anthony Mayunga (Mwananchi), Beldina Nyakeke (The Citizen) na Anna Mroso (Nipashe), walikamatwa.

Waandishi hao walikamatwa jana na mbunge huyo wa viti maalumu wa Chadema katika Kijiji cha Nyakunguru na kuhojiwa kwa muda katika Kituo cha Polisi Nyamwaga kabla ya kupelekwa kwa Kamanda wa Operesheni Maalumu, Paul Chagonja. Waliachiwa kwa kujidhamini wenyewe saa 9:30 jioni.

Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema alipotafutwa kuzungumzia suala hilo simu yake ya mkononi ilipokewa na msaidizi wake ambaye alisema anayeweza kulitolea ufafanuzi ni msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso.

Senso alipotafutwa naye alisema hawezi kulizungumzia akimtupia mpira Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime, Constantine Massawe.

Hata hivyo, Massawe alikanusha madai hayo ya kupora maiti akisema kwamba walipata taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu kwamba kuna baadhi ya watu waliokuwa wakiwazuia kuchukua miili ya ndugu zao.

"Jana baada ya kufanyika uchunguzi kama walivyotaka, miili yote ilikuwa chini ya familia. Sasa uamuzi wa kuzika ulikuwa juu yao, lakini majira ya saa mbili usiku tulipata taarifa kuwa kuna watu wako mochwari wamezuia ndugu wanaotaka kuzika wasichukue miili ya jamaa zao," alisema Kamanda Massawe na kuongeza:

"Tulipofika tulikuta wapo watu wanane, wanne walikuwa ni wakazi wa Singida na wengine wanne wakiwa ni wakazi wa Tarime. Tuliwakamata na kusimamia ulinzi wa ndugu waliotaka kuchukua miili ya jamaa zao wakachukua."

Alisema baada ya miili hiyo kuchukuliwa, polisi ililitoa msaada wa kuwasafirishia ndugu hao hadi majumbani kwao na walikuwa wanaishusha kadri walivyokuwa wameambiwa na ndugu hao.

‘Sasa asubuhi hii (jana), tumeelezwa kuwa kuna kundi la watu wengine lilikuwa likipita nyumba hadi nyumba kuwahamasisha wafiwa kutokubali kuzika maiti za ndugu zao baada ya kufuatilia tuliwakamata na hawa waandishi wakiwa wanapiga picha jeneza," alisema Kamanda Massawe.

Awali, Katibu wa Chadema Tarime Mjini, Paschal Warioba alidai kuwa polisi walipora maiti hizo na kwamba viongozi wa chama chake walikamatwa juzi usiku majira ya saa nne.

"Lissu yuko 'lockup' (rumande) hapa Nyamongo, walikuwa wakifuatilia maiti za watu waliouawa katika vurugu mgodini ili leo (jana) ziende kuzikwa, lakini kabla ya kufanikisha zoezi hilo jana (juzi), polisi walizipora maiti hizo kwa kuwadanganya baadhi ya ndugu kwa kuwapa fedha ili waende kuzizika," alisema.

Warioba alidai kuwa baadhi ya maiti tayari wamezikwa, lakini wengine wameonekana katika maeneo karibu na walipokuwa wakiishi.

Juzi alasiri, maiti hao walifanyiwa uchunguzi wa mwisho tayari kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana chini ya uratibu wa Chadema kabla ya vurugu kubwa kuibuka katika chumba cha maiti baada ya polisi kufika na kukuta umati wa watu uliokuwa tayari umekusanyika kuanzia saa 1:30 jioni ili kuchukua miili hiyo kwa ajili ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo.

Hata hivyo, Chadema kinadai kwamba baadhi ya ndugu wa wafiwa waliona maofisa wa polisi wakinunua majeneza manne na kuyapakia katika gari lao kabla ya kufika hospitali hapo kuchukua miili hiyo.

Kutokana na taarifa hiyo, Lissu, Waitara na makada wengine wa Chadema wakiwa na wananchi wengine waliamua kufika katika eneo la mochwari na muda mfupi baadaye, idadi ya watu iliongezeka kwa lengo la kuzuia Polisi kubeba miili hiyo.

"Wakati tukio hilo hapo mochwari polisi walifika majira ya saa mbili usiku na kukuta timu kubwa ya watu ambao walikuwa wamejitolea kulinda maiti hao wasichukuliwe," alisema mkazi wa Tarime aliyejitambilisha kwa jina la Mwita Nyankaira na kuongeza:

"Walianza (polisi) kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu na ndipo walipowakamata kina Lissu na wengine. Sisi tulifanikiwa kukimbia."

Alisema baada ya polisi kuwasambaratisha wananchi, walirudi hospitalini hapo na kuchukua maiti hao na kuanza kuwapeleka usiku huohuo kwenye familia za wafiwa.

Habari zimeeleza maiti ya Chawali Bhoke ilipelekwa katika Kijiji cha Bonchugu, wilayani Serengeti na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mwikwabe Makena alisema kulikuwa na vurugu kubwa jana asubuhi kijijini hapo baada ya polisi kuwalazimisha ndugu kupokea mwili huo kwa ajili ya kuuzika.

"Kumekuwa na vurugu kubwa iliyoambatana na polisi kurusha mabomu ya machozi," alisema mwenyekiti huyo.

Maiti nyingine ilipelekwa katika Kijiji cha Nyakunguru, Kata ya Kibasuka. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyamanche kilichoko kwenye kijiji hicho, Isaack Marara alisema jana saa 12:00 asubuhi, alifuatwa na mkazi wa eneo hilo, Kisabo Ghati na kumweleza kuwa kuna jeneza limewekwa barabarani lakini hawajui kuna nini ndani yake.

"Watu walishtuka sana kwani hawajawahi kuona tukio hilo. Baba mdogo wa marehemu Emmanuel Magige, Ambrose Nyabwanya alidai kuwa saa 6:00 usiku wa juzi, magari mawili ya polisi yalisimama na kushusha jeneza mita 200 kutoka nyumbani kwao kisha magari hayo yakaondoa haraka.”

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando alisema kitendo cha polisi kuchukua kinguvu miili ya watu hao wanne kwa lengo la kwenda kuizika ni kinyume na walivyokubaliana.

Marando alisema walikubaliana na polisi pamoja na ndugu wa marehemu Jumapili iliyopita kwamba shughuli za mazishi zifanyike leo katika Uwanja wa Sabasaba.

“Chadema siyo kama tumeshikilia kidedea msiba huu. Tunafanya hivi kwa kuwa waliouawa ni makada wa Chadema na hiyo ndiyo siasa."

Ripoti ya uchunguzi wa miili yawekwa hadharani

Uchunguzi wa miili ya maiti wanne waliopigwa risasi na askari polisi katika Mgodi wa African Barrick North Mara uliofanywa na daktari bingwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Makatta imebaini kuwa marehemu wote walipigwa risasi maeneo ambayo hayakulenga kujeruhi, bali kuua.

Uchunguzi huo uliochukua saa 4:27 ulianza saa 5.20 asubuhi hadi saa 9.47 alasiri. Upande wa familia za wafiwa ulisimamiwa na Dk Greyson Nyakarungu kutoka Hospitali ya Wilaya ya Tarime na askari wawili. Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa hospitali

Dk Nyakarungu alisema Emmanuel Magige mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari namba za PM1/5/2011 (TGH), alipigwa risasi katika nyonga ya kushoto ambako kulikuwa na tundu la duara llilokuwa na upana wa sentimita 0.5 ilipoingilia na sentimita 2.5 ilipotokea.

“Mishipa ya damu iliharibiwa, kibofu cha mkojo, mishipa ya fahamu, mfupa wa nyonga ulisagika, damu ikavia ndani ya tumbo, lakini chini ya mgongo karibu na risasi ilipotokea kulikuwa na tundu linaloonyesha kuwa alichomwa na kitu chenye ncha kali kama singa ya bunduki,” alisema na kuongeza:

“Tumebishana sana kwa hilo wenzangu wakidai huenda aliangukia kitu kikamchoma, ikumbukwe kuwa alipigwa kwa nyuma akikimbia hivyo asingeweza kuanguka chali zaidi ya kifudifudi,” alisema.

Kuhusu Chacha Ngoka mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM 2/5/11 (TGH), uchunguzi ulibaini kuwa alipigwa risasi mgongoni karibu na kiuno na kutokea katikati ya mbavu chini ya titi, tundu la kuingilia likiwa ni sentimita za duara 0.3 na ukubwa wa tundu pa kutokea ikiwa ni sentimita tano.

Mishipa mikubwa ya damu iliharibiwa, ini likasagwasagwa, damu iligandia kwenye mfumo wa upumuaji hali ambayo inadhihirisha kuwa alipumua kwa nguvu, damu ilikwisha mwilini na kuwa alipigiwa risasi kwa mbali.

Alisema marehemu Bhoke mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM/3/5/11(TGH) alipigwa risasi ya kichwani karibu na sikio na kidonda chake pakuingilia ni sentimita za duara 0.2 ,pa kutokea sentimita tano za duara kwenye paji la uso hivyo kuharibu ubongo, fuvu na mifupa yote kubomolewa.

Kuhusu uchunguzi wa Mwikwabe Marwa Mwita mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM/4/11 (TGH) alisema alipigwa risasi karibu na nyonga na kuacha tundu la sentimita za duara 3,5 na risasi haikutoka nje na kuharibu mifupa yote ya nyonga, misuli ikawa imeharibiwa na kipande cha risasi kilikutwa katikati ya misuli (PSOAS), damu ikiwa imevia tumboni.

“Kilichoonekana hapo ni kuwa walipigwa risasi kwa mbali tena kwa nyuma maana wote zimeingilia kwa nyuma na maeneo waliyopigwa risasi ni yale ya kuua si kuwapunguza nguvu kama walikuwa wamegoma kusalimu amri,” alisema daktari huyo.

Kuzuiwa kwa maziko ya pamoja

Awali, Chadema kilipanga kuendesha ibada ya maziko katika Uwanja wa Sabasaba leo kuanzia saa 2:00 asubuhi kabla ya kupelekwa katika vijiji vyao kwa ajili ya mazishi ya kifamilia.

Lissu alisema juzi usiku kuwa licha ya kukubaliana na wanafamilia na Kamishina wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, jeshi la polisi lilibatilisha kibali hicho baadaye.

"Tumekuwa katika maandalizi ya mazishi hayo tangu jana jioni. Hata hivyo, jioni hii tumeletewa barua ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tarime kututaarifu kwamba haturuhusiwi tena kuwaaga marehemu wetu kama ilivyokubaliwa jana," alieleza Lissu.

Waandishi waeleza walivyokamatwa

Baadhi ya waandishi waliokamatwa katika sakata hilo walieleza kuwa walikuwa kazini kutekeleza majukumu yao.

Mmoja wa waandishi waliokamatwa, alisema baada ya kusikia taarifa juzi usiku juu ya polisi kupiga mabomu na kuchukua miili ya marehemu aliamua kuingia kazini kufuatilia tukio hilo.

“Tulipofika hapo kijijini tulikuta pia kuna mbunge wa viti maalum wa Chadema, sasa wakati tukiwa tunamhoji, polisi wakafika na kutukamata wakieleza kuwa tumekuwa tukichochea ndugu wasizike miili ya marehemu," alisema

Alisema kitendo cha polisi kuwahoji jana kuanzia saa 5:10 asubuhi hadi saa 6:20 mchana kimewafanya washindwe kuwajibika ipasavyo jambo ambalo linapaswa kulaaniwa na wadau wote wa habari.

“Tulihojiwa hapa kwa zaidi ya saa moja na ilipofika saa 6:20 mchana walituambia tusubiri maelekezo kutoka kwa kamanda wa polisi…" alisema.

Mei 16, mwaka huu polisi wilayani Tarime iliwaua kwa kuwapiga risasi watu wanne kati ya zaidi ya watu 1,000 waliovamia mgodi wa Nyamongo wilayani humo kwa lengo la kupora mchanga wa dhahabu.

Tukio hilo lililotokea katika Kijiji cha Matongo, lilizua msuguano baina ya polisi, Chadema na wananchi wa eneo hilo ambao juzi waligoma kuzika miili ya marehemu hao na kukataa rambirambi ya polisi.

Chanzo: Mwananchi
 
The american star has a story on it google it.
Totally agree with you!....Itgdt's so sickening,and why aren't we getting the images? or even an article with quotes from the families,neighbours,the cops......can somebody please take a photo or video with your phone and send it to a friend or any human rights office nearby for uploading?We don't really need the media,we can post pictures and videos easily,it's very very easy!
We get pics and vids from syria,yemen,libya...uploaded from phones,can't we do it?.....can we get the news from our point of view?Anybody?
 
Back
Top Bottom