Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,254
- 21,275
Kwanza pole kwa kazi nzito ya kulenga madaraja na kupambana na full and sports lights, vicheche na madereva wanaosinzia njiani. Kiukweli hii Ni Kazi nzito Sana, na Mimi kama turnboy Wako najua jinsi shughuli hii ilivyo pevu, na hizo kelele za hao jamaa wa kwenye Trailer huko nyuma zisikutishe.
Lakini nilitaka nikukumbushe kua hii Ni Scania 113H/310, kwa kifupi hii gari Ina Pulling moja matata Sana achilia mbali turbo inavyoimba hapo kwenye through-pipe, hii gari huwezi kuendesha kama unaendesha Scania Series za P, R na G. Wala huwezi kuendesha kama Benz Actros au DAF XF 480 new model macho ya panzi kwa juu. Huku unatakiwa utulize akili, mambo ya high na low na sprinter gears yasikuvuruge, magneto iliyofungwa hapo kwenye gearbox sio ghali Sana lakini inahitaji matunzo tusije kulala porini. Jambo kubwa zaidi nilililoliona kwako na ambalo unahitahiji kufanyia kazi Ni hili, kwanza unavaa Sana headphones kwahiyo huwezi kusikia namna chombo kinavyoitikia uki-engage gear au hata diff ikianza kuvuma hutosikia mpaka ikate msalaba au itafune meno. Kwahiyo jitahidi usivae hizo headphone kila Mara maana itatugharimu, sina maana uvue headphone usikilize kelele za hao jamaa wa huko nyuma au hawa tulionao humu kwenye cabin, Ila nataka usikilize chombo chako kinaendaje, usisubiri mpaka gari isizi ndio ubadirishe gear, unaichosha Sana.
Jambo lingine Ni kwamba unapenda Sana mambo ya Retarder as if tupo kwenye VOLVO FH 12, Retarder Ni nzuri kweli ila sio Kila sehemu Tu, Kuna miteremko mingine tushuke Tu na stop engine na MGUU KATI inatosha Sana, halafu sasa Retarder yenyewe sometimes unaiset kwenye 60kph, sasa kwa speed hiyo Kuna kona hatutozimaliza tukiwa na mwendo mkali hivyo, balance Mguu Kati, ngoja nikuulize swali, unafikiri kwanini magari mengi ya kisasa Hua yanashindwa pale kwenye kona ya mwisho kutoka darajani pale sekenke kama unatokea upande wa huku misigiri? Au pale mwisho kabisa wami darajani? Jibu Ni Retarder!!! Kama unataka kuset Retarder bora uweiweke kwenye 30kph au 20kph kabisa! Tukishuka mteremko kama K-9 au kitonga au hata hiyo wami kwa Retarder ya 70kph na hiyo Dundu huko kwenye Trailer wallah hautookotwa hata mfupa kule chini.
Lakini pia sina maana uendeshe Lori letu kama FIAT Mbaula zile za wasomali, huku hamna mambo ya Mkasi Juu/Mkasi chini, Ila pia usiendeshe kama modern truck Sana, Tutakufa Kiongozi halafu mwenzio wanangu bado wadogo Sana sitaki kumuachia majanga Mke wangu. Wewe twende mdogo mdogo Tu tutafika Tu, kwani tunamuwahi nani?
Halafu pia wakati mwengine hao jamaa huko nyuma kwenye Trailer wanatusaidia, imagine pale mlima Nyoka tunapandisha kina Tenende wakianza kuiba mali za watu utawasikia bila kuambiwa? So watch it, wakaushie ila not to that extent.
Haya bwana Mimi napanda kitanda cha juu hapo kupumzika kidogo, ila ado ado.. Hii Ni Scania 113, sio 90 wala hayo madude mengine ya kichina kama Howo na Faw.
Bon Voyage.