Dereva wa pikipiki, abiria wake wawili wauawa kwa gari

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Watu watatu wamekufa na mwingine kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari wakiwa wamebebwa kwenye pikipiki mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 9:00 alasiri baada ya gari hiyo kuigonga pikipiki ilikuwa imebeba watu wanne eneo la Changa, barabara ya Msata wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda Mwakyoma alisema pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 132 BDV aina ya Sanlg ikiendeshwa na Ally Ramadhani (26), ilikuwa ikitokea Msata kuelekea Bagamoyo.

Alisema pikipiki hiyo iligongwa na gari aina ya Prado yenye namba za usajili T 470 AVH likiendeshwa na raia wa Uingereza, Nevile Bissett (44), mfanyakazi wa kampuni ya NITS kitengo cha kontena, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mwakyoma aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Emile Msagama (26), mfanyabiashara wa Kwa Mathias mjini Kibaha mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jiana moja la Kulwa (26), mkazi wa Maili Moja, Kibaha na dereva wa pikipiki hiyo, Ally Ramadhani (26).

Aidha, alisema katika ajali hiyo, abiria mmoja kati ya wanne waliopanda pikipiki hiyo, Dingo Rakika (26), mkazi wa Fukayose, Bagamoyo alijeruhiwa vibaya na kulazwa katika hosptali maalum ya Tumbi kwa matibabu zaidi.

Kamanda alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hosptali hiyo kwa ajili ya kusubiri ndugu kwa mazishi.

Wakati huo huo, watu wawili ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, wamekufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuligonga gari lingine ambalo lilikuwa limesimama pembeni mwa barabara baada ya kuharibika.

Kamanda Mwakyoma alisema tukio hilo lilitokea Februari 15, mwaka huu saa 4:30 usiku eneo la Mlandizi wilayani Kibaha barabara kuu ya Dar es Salaam -Morogoro.

Alisema ajali hiyo ilihusisha gari namba T347 AXY aina ya Mitsubish Fuso na kuwa dereva hakujulikana jina lake mara moja na kuwa likuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro na kwamba liligonga lori lingine aina ya Scania lenye namba za usajili T 368 AJG lililokuwa limeharibika na kuegeshwa kando kando ya barabara.

Alisema madereva wawili wote wa magari hayo walikimbia baada ya ajali hiyo na wanatafutwa na polisi na kuwa, Seif Walii (24), ambaye ni fundi wa magari, alijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo.

Kamanda Mwakyoma alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari lililoharibika kwa kutoweka alama za kuonyesha kuwa ni bovu.
 
Hii mambo ya pikipiki kubeba mishikaki ipigwe marufuku kabisa.
Polisi wanaangalia tu jinsi sheria za usalama barabarani zikivunjwa na uhai wa wananchi ukihatarishwa bila ya kuchukua hatua zozote.
Serikali i haramishe matumizi ya pikipiki kama chombo cha biashara cha kusafirisha abiria.
 
Pikipiki inabeba watu 4 duh hii balaaaaaa

Mkuu,

Those pikipiki na Bajaj are the new KILLING MACHINES on Dar es Salaam Roads!

Madereva wa hizi pikipiki na Bajaj ni kama wehu vile - wanasahau kuwa chombo wanachoendesha (ni 1/2 Tyre less ya Gari) equilbrium yake inategemea MZIGO zaidi wanaendesha kama vile ni Corolla Limited!

 
Back
Top Bottom