Dereva wa muda (temporary driver)

Zainab Tamim

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,293
578
Tunatafuta driver wa muda.

Kazi zitahusu kwenda kibaha (Misugusugu na kurudi) na hapa hapa mjini Dar kwenda huku na kule.

Awe muaminifu, gari zipo ndogo na Hilux 2.8 pickup iliyo choka choka (ya kuendea shamba).

Na akifanya vizuri kwa baadae anaweza pia kuhamia kwenye Fuso crane (permanent) kama ataweza na itapokamilika matengenezo yake (inafanyiwa repair) kwa mapatano mengine.

Malipo 10,000/= kwa siku.

Kama yupo aliye tayari ampigie Mzee Abdul 0756803528.

Hii kazi ni ya muda (temporary work).

Update 16-11-2015:

Wote mliotupigia simu asanteni sana.

Tumepata dereva tayari ni kati ya waliopiga simu.

Poleni kwa usumbufu tulikuwa tunahitaji dereva mmoja tu.

Asante, tunataka watu wanaoweka mambo wazi kama wewe ili mtu ajipime sio wengine wanakuja na mbwembwe za kiingereza huku.
 
Asante, tunataka watu wanaoweka mambo wazi kama wewe ili mtu ajipime sio wengine wanakuja na mbwembwe za kiingereza huku.

Asante kaka. Nimeona nikiweka wazi itaondoa usumbufu na itaokoa muda kwa anaehitaji kazi na kwangu.

Na kama kuna yeyote ana swali lolote aniulize tu hapa nitakuwa muwazi na mkweli.
 
Samahani. Atakae kazi awe na leseni iliyo hai. Maana kuna mtu kapiga simu anasema yeye anataka hiyo kazi lakini leseni yake inataka ihuishwe, akopeshwe pesa kwanza akatengeneze leseni.

Naomba samahani sana hatuwezi kufanya hivyo. Kama hauna leseni hai usijisumbue kutupigia hatutoi mkopo wa kutengenezea leseni au mwengine wowote.

Ukiajiriwa unafanya kazi, ikifika muda wa kazi umekwisha unachukwa chako siku hiyo hiyo. Hii ni kazi a kibarua na ya muda tu.
 
Kwa wale wanaotaka kujuwa kazi inaanza lini, napenda kuwajulisha kuwa ni sasa. hata leo ukiweza kuanza, njoo.
 
Mimi Mgeni wa hayo Mazingira ata kibaha siijui iko wapi na nipo Shinyanga cjawah kuishi dar
 
Wote mliotupigia simu asanteni sana.

Tumepata dereva tayari ni kati ya waliopiga simu.

Poleni kwa usumbufu tulikuwa tunahitaji dereva mmoja tu.
 
Napenda kuwajulisha ndugu zangu wote.

Wale wenye matatizo ya ngozi aina zote, vidonda sugu, gas, ulcers, chunusi, vidonda ndugu, fungus na hawana uwezo wa kulipia, ninawaomba waje wachukuwe bure hii tiba yetu mbadala bila kulipia hata senti moja.

Hii ni tiba pekee ambayo ukinunua na kukusaidia basi umelipia na tiba kwa wengine wasio na uwezo wa kununua.​

Naitaji hiyo dawa nitaipataje?
 
Back
Top Bottom