Dereva wa Lissu isiwe kisingizio cha kuacha uchunguzi

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
934
1,000
Hivi karibuni kumekuwa na visingizio eti Dereva wa Lissu amekimbia kwahiyo imechangia kukwamisha uchunguzi wa kushambuliwa Lissu. Sioni kama kutokuwepo dereva wa Lissu iwe ni tatizo na nitaelezea bi kwanini.

Kwanza, dereva wa Lissu amekimbia kuokoa maisha yake. Huwezi kumlaumu kwa hilo hasa ukifikiria matukio mengine ya watu kutoweka kama akina Ben Saanane.

Pili, wachunguzi wa tukio hilo wana uwezo wa kumuhoji dereva na Lissu mwenyewe kwa kutumia video call. Hii njia si ngeni na pia inatumiwa na nchi nyingine.

Tatu, kwenye mahojiano yake na VOA Tundu Lissu alisema kwamba wachunguzi wa shambulio lake waliahidi kwenda Nairobi kufanya mahojiano naye na dereva lakini hawakwenda.

Nne, wachunguzi wanaweza kutumia msaada wa Interpol kufanya mahojiano.

Kwa kuhitimisha ningependa kusikia wachunguzi wakitoa maelezo kuhusu mambo haya.

1. Waelezee walichokiona kwenye recordings za CCTV cameras.

2. Waelezee kwanini CCTV cameras ziliondolewa baada ya shambulio. Nilifikiri wangeongeza CCTV cameras nyingine kuongeza ulinzi lakini badala yake waliziondoa.

3. Kwanini hakukuwa na walinzi kwenye siku ya shambulio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom