Dickson Ng'hily
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 451
- 485
MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato mkoani Kagera imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja dereva wa gari dogo la kusafirisha abiria maarufu kama vipanya, baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi 600,000 baada ya kupatikana na hatia ya kubeba abiria wengi na kuwatoza nauli kubwa zaidi ya kiwango kinachotakiwa kisheria.
Akisoma mashikata mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Chato, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Mathias Maduhu, alidai kuwa Mei 26, mwaka huu mshitakiwa Boniphas Suka alikamatwa eneo la Kijiji cha Muungano majira ya saa sita na dakika 30 mchana akiwa na abiria 12 kwenye gari alilokuwa akiliendesha kinyume cha sheria za usafirishaji wakati gari lake likiwa na uwezo wa kubeba abiria watano.
Akisoma mashitaka dhidi ya mshitakiwa alisema alikuwa akiwatoza nauli abiria kati ya shilingi 4,000 hadi shilingi 5,000 katika umbali wa kilometa 80 wakati nauli halali iliyopangwa na Sumatra ni shilingi 2,500 .
Mshitakiwa alikiri kosa na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 600,000 na aliposhindwa kulipa faini hiyo mahakama ilimhukumu kifugo cha mwaka mmoja jela
Source: Tanzania Daima