Dereva Trekta Kanipora mpenzi

jrmlaurence

Member
Dec 2, 2010
80
57
NAWAHAKIKISHIENI duniani hakuna jambo jipya, mambo yanajirudia rudia kwa staili tofautitofauti tu. Kuna jambo limenitokea na baada ya kutafakari nimekubali kuwa hakuna jipya duniani nawaambieni.

Kuna binti mmoja hapa kijijini kwetu nilimpenda sana, kwa kweli nilikuwa nimeshapanga lazima nimuoe. Na yeye mwenyewe analijua hilo maana tumeshaongea mara nyingi sana pale kisimani tulipokuwa tukikutana wakati akija kufua au kuteka maji. Najua alikuwa akijua kuwa nampenda sana maana nilikuwa najitahidi kumpa vizawadi mbalimbali.
Nikipata elfu mbili nampa, siku moja nilikwenda mjini nikamnunulia Sketi na kitop, hata nyimbo nilikuwa siku nyingine namuimbia wakati anafua, kwa kweli ilikuwa raha sana, hata wenzie wote kijijini nao walijua kuwa tunapendana.

Mwezi uliopita nimeshangaa nimeenda kisimani kumngojea, kweli kaja, lakini salamu yenyewe kajibu kwa shida. Nimejitahidi kumuuliza tatizo hakujibu lolote la maana, kakataa hata nisimtwishe ndoo ya maji kichwani jambo ambalo tulikuwa tukilifanya kila mara kwa mapenzi makubwa.
Ghafla wakati najitahidi kumbembeleza aniambie tatizo ni nini, akafika jamaa mmoja ambaye ni mgeni kijijini maana sijawahi kumuona, alipomuita jina mpenzi wangu sura ya mpenzi wangu ikalipuka kwa furaha, wakaendelea na salamu zao utadhani mimi sipo, sikuamini. Nikaondoka polepole machozi yakinilengalenga.

Nikamfuata rafiki yake wa karibu na kumuuliza kinaendelea nini? Jibu alikuwa nalo, kumbe yule jamaa mgeni pale kijijini ni dereva wa trekta, kaja kijijini kulima mashamba kwa wanaoweza kukodisha trekta, halafu ana redio kaseti ambayo kampa mpenzi, kwa hiyo mimi nimefutwa sina kitu. Iliniuma sana, maana ni kweli nisingeweza kushindana na mtu ambaye kila siku anaingiza hela akikodishwa kulima shamba na kwa vile ni msimu wa kilimo trekta linatakiwa kila siku.

Mimi hata baiskeli sina. Nikakata tamaa, machozi yakinidondoka. Wakati nawaza haya nikakumbuka kuwa hii ni mara ya pili jambo kama hili linanitokea. Nikakumbuka wakati niko darasa la tatu kulikuwa na msichana mmoja darasani nilikuwa nampenda kweli, kila asubuhi nikifika tu shule, nilikuwa nampelekea kiazi cha kuchoma au siku nyingine andazi.
Nikikaa darasani ilikuwa lazima nimwangalie mara kwa mara, katika akili yangu ya kitoto nilijua huyo ndiye nitakayemuoa nikiwa mkubwa. Najua naye alikuwa akinipenda maana naye akipewa kashata au pipi kwao alikuwa akiniletea, mambo yalikuwa matamu, hata shule nilikuwa nawahi ili tu nimuone anapoingia kwenye geti la shule.

Siku moja tukiwa darasani akaingia mwanafunzi mpya. Kitu ambacho kilikuwa wazi kwanza alikuwa kavaa nguo safi na mpya, pia alivaa viatu vyeusi vya ngozi vinang’aa kwa upya, kitu ambacho kwa shule yetu ya kijiji ilikuwa nadra sana, pili alikuwa kavaa miwani, hakuna hata mwalimu mmoja aliyekuwa na miwani, niliwahi kumuona mzee mmoja toka mjini siku moja ndiye alikuwa amevaa miwani.

Basi wote tukabaki tunamshangaa huyu mwanafunzi mpya baadaye tukaja kuambiwa alikuwa anasoma mjini sasa kaja kuishi kwa bibi yake, kwa kuwa baba yake kapata kazi Dar es Salaam. Kiukweli huyu jamaa aliuteka moyo wa shule nzima. Lakini kubwa zaidi si akauteka na moyo wa mpenzi wangu, nikawa mimi sina maana tena, kashata analetewa yule mtoto mpya mwenye miwani, kimsingi nikaachwa kwa sababu ya miwani.

Sasa ukubwani nimenyang’anywa mpenzi na dereva wa trekta, kweli duniani hakuna jipya.

 
Kastori katamu kweli... kwama vipi uza smart phone inayokufanya uingie humu ili na wewe ununue cha juu zaidi ya dereva wa trekta LOL :smiling::smiling::smiling::smiling::smiling:
 
acha uzinzi wewe ungemuoa asingebabaika hivyo
lakini usife moyao huyo jamaa uapandaji mbegu ukianza tu na yeye hana chake atarudi mjini ww Papuchi ni lako
Kipya kinyemi wanasema waswahili (New Taste at a New Genaration)
 
Mwenye kisu kikali ndo hula nyama, huenda ulikuwa husomeki, mwenzio huenda alishachana na marinda wakati wewe ukisubiri ndoa.
 
Urefu na mpangilio wa aya ni mzuri.Dhamira ya mwandishi iko wazi.Zaidi ongeza misamiati ya lugha adhim ya Kiswahili mvuto uongezeke.Tumia tanakali za sauti ikibidi,methali na hata misemo.

BTW:Karibu MMU...Natumai jukwaa lako pendwa hujaondoka mazima.
 
"................nilikuwa nampelekea kiazi cha kuchoma au siku nyingine andazi"

teh teh teh teh utakua ww kweli ni kiazi mkuu! Natania tu .....pole mkuu!
 
NAWAHAKIKISHIENI

duniani hakuna jambo jipya, mambo yanajirudia rudia kwa staili
tofautitofauti tu. Kuna jambo limenitokea na baada ya kutafakari
nimekubali kuwa hakuna jipya duniani nawaambieni.

Kuna binti mmoja hapa kijijini kwetu nilimpenda sana, kwa kweli nilikuwa
nimeshapanga lazima nimuoe. Na yeye mwenyewe analijua hilo maana
tumeshaongea mara nyingi sana pale kisimani tulipokuwa tukikutana wakati
akija kufua au kuteka maji. Najua alikuwa akijua kuwa nampenda sana
maana nilikuwa najitahidi kumpa vizawadi mbalimbali.
Nikipata elfu mbili nampa, siku moja nilikwenda mjini
nikamnunulia Sketi na kitop, hata nyimbo nilikuwa siku nyingine
namuimbia wakati anafua, kwa kweli ilikuwa raha sana, hata wenzie wote
kijijini nao walijua kuwa tunapendana.

Mwezi uliopita nimeshangaa nimeenda kisimani kumngojea, kweli
kaja, lakini salamu yenyewe kajibu kwa shida. Nimejitahidi kumuuliza
tatizo hakujibu lolote la maana, kakataa hata nisimtwishe ndoo ya maji
kichwani jambo ambalo tulikuwa tukilifanya kila mara kwa mapenzi
makubwa.

Ghafla wakati najitahidi kumbembeleza aniambie tatizo ni nini,
akafika jamaa mmoja ambaye ni mgeni kijijini maana sijawahi kumuona,
alipomuita jina mpenzi wangu sura ya mpenzi wangu ikalipuka kwa furaha,
wakaendelea na salamu zao utadhani mimi sipo, sikuamini. Nikaondoka
polepole machozi yakinilengalenga.

Nikamfuata rafiki yake wa karibu na kumuuliza kinaendelea nini?
Jibu alikuwa nalo, kumbe yule jamaa mgeni pale kijijini ni dereva wa
trekta, kaja kijijini kulima mashamba kwa wanaoweza kukodisha trekta,
halafu ana redio kaseti ambayo kampa mpenzi, kwa hiyo mimi nimefutwa
sina kitu. Iliniuma sana, maana ni kweli nisingeweza kushindana na mtu
ambaye kila siku anaingiza hela akikodishwa kulima shamba na kwa vile ni
msimu wa kilimo trekta linatakiwa kila siku.

Mimi hata baiskeli sina. Nikakata tamaa, machozi yakinidondoka.
Wakati nawaza haya nikakumbuka kuwa hii ni mara ya pili jambo kama hili
linanitokea. Nikakumbuka wakati niko darasa la tatu kulikuwa na msichana
mmoja darasani nilikuwa nampenda kweli, kila asubuhi nikifika tu shule,
nilikuwa nampelekea kiazi cha kuchoma au siku nyingine andazi.

Nikikaa darasani ilikuwa lazima nimwangalie mara kwa mara,
katika akili yangu ya kitoto nilijua huyo ndiye nitakayemuoa nikiwa
mkubwa. Najua naye alikuwa akinipenda maana naye akipewa kashata au pipi
kwao alikuwa akiniletea, mambo yalikuwa matamu, hata shule nilikuwa
nawahi ili tu nimuone anapoingia kwenye geti la shule.

Siku moja tukiwa darasani akaingia mwanafunzi mpya. Kitu ambacho
kilikuwa wazi kwanza alikuwa kavaa nguo safi na mpya, pia alivaa viatu
vyeusi vya ngozi vinang’aa kwa upya, kitu ambacho kwa shule yetu ya
kijiji ilikuwa nadra sana, pili alikuwa kavaa miwani, hakuna hata
mwalimu mmoja aliyekuwa na miwani, niliwahi kumuona mzee mmoja toka
mjini siku moja ndiye alikuwa amevaa miwani.

Basi wote tukabaki tunamshangaa huyu mwanafunzi mpya baadaye
tukaja kuambiwa alikuwa anasoma mjini sasa kaja kuishi kwa bibi yake,
kwa kuwa baba yake kapata kazi Dar es Salaam. Kiukweli huyu jamaa
aliuteka moyo wa shule nzima. Lakini kubwa zaidi si akauteka na moyo wa
mpenzi wangu, nikawa mimi sina maana tena, kashata analetewa yule mtoto
mpya mwenye miwani, kimsingi nikaachwa kwa sababu ya miwani.

Sasa ukubwani nimenyang’anywa mpenzi na dereva wa trekta,
kweli duniani hakuna jipya.


ahaaaaa kwi kwi nimecheka sana ivi mkuu std 3 kumbe wew ulishakuwa na
mawazo hayo.?? ebu nambie watu wasikuskie ivi dadudu kako enzi izo kalikuwa kana sence iyo
kitu? dah umenivunja mbavuuuu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom