Dereva bajaji mwenye shahada ya uzamili

Mbikiboy

Member
Feb 15, 2019
90
86
Hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa vyombo vya habari kutoa habari vikielezea watu mbalimbali ambao wamesoma mpaka ngazi za shahada au uzamili wakifanya shughuli ambazo hata darasa la saba anafanya.

Tunadhani wadogo zetu watahamasika kusoma mpaka katika level hizi kwa mazingira haya au itawakatisha tamaa?? Binafsi naona kama kutakuwa na changamoto kubwa mbeleni kuhusiana na watu kuhamasika na elimu!

IMG-20201227-WA0004.jpg
 
Wakubwa hawana cha kuwashtua maana watoto wao wana ajira za vimemo

Utashangaa wanamsifia kinafiki kwa kujiajiri.
 
Hii biashara ya Bajaj siyo ya kuidharau kama mtu akakubali kuweka cheti pembeni akaingia humo anatusua,kuna siku nilipanda Bajaj Mbezi jamaa akaniambia ana masters.

Nina Bajaj nimempa jamaa mmoja mkataba miaka miwili iwe yake kila baada ya siku 10 aniingizie 200K hajawahi kupitisha siku na yeye anafanya hivi hivi kuokota miatano mia tano pale Ubungo external,na service ni juu yake kasoro vibali na bima tu na anamudu vyote hivyo kwa usahihi.Tanzania elimu ni ya kuondoa ujinga tu kichwani ila ukiiweka mbele kwamba itakutoa utafeli vibaya sana!
 
Mkuu kwa Hali ya sasa,vyeti inabidi uweke pembeni upambane kiume na degree yangu mojaa Ila Ni chingaa na tembeza viatu na maisha poa kabisa,familia inakula na kwenda chooni.wasomi wengi wanalia Lia niwale wanaotaka kazi za maofisini.mfungwaa achagui gerezaaa
 
Mkuu kwa Hali ya sasa,vyeti inabidi uweke pembeni upambane kiume na degree yangu mojaa Ila Ni chingaa na tembeza viatu na maisha poa kabisa,familia inakula na kwenda chooni.wasomi wengi wanalia Lia niwale wanaotaka kazi za maofisini.mfungwaa achagui gerezaaa
Yale yale ubunifu wa survival mode...wacha wadhungu watutawale tuu
 
Hakuna tatizo biashara ukikua hiyo masters ataitumia ku manage hiyo kampuni
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom