Dereva amlipua risasi mwenzake wakigombea abiria

M

MegaPyne

Guest
Na Daniel Mjema, Moshi,

Mfanyabiashara wa mabasi yanayofanya safari kati ya Moshi na Kilema, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga risasi dereva wa basi la Flora Coach kwa madai ya ugomvi wa kugombea abiria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko, jana aliliambia Mwananchi kuwa mfanyabiashara huyo ametiwa mbaroni tangu amjeruhi kwa kumpiga risasi mguuni dereva huyo, Rodgers Lyimo, Jumamosi iliyopita.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:30 jioni katika maeneo ya Kilema, Wilaya ya Moshi Vijijini, baada ya basi la mfanyabiashara huyo na lile linaloendeshwa na Rodgers aina ya Toyota DCM kufika mwisho wa safari.

"Ni kweli tunaye huyo mfanyabiashara tangu Jumamosi. Walizozana na huyo dereva basi akaamua kuchukua bastola yake na kumpiga risasi ya mguu. Tunaweza endelea kumhoji," alisema Ng'hoboko.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu kutoka katika Hospitali ya Kilema alikolazwa kwa matibabu, Rodgers alidai kuwa chanzo cha tukio hilo ni kitendo cha abiria kuteremka kwenye basi la mfanyabiashara huyo na kuingia katika basi analoendesha.

Dereva huyo alidai kuwa Ijumaa iliyopita majira ya 10:30 jioni, wakiwa katika stendi kuu ya mabasi Moshi, abiria waliingia katika basi lake na kuliacha lile la mfanyabiashara ambalo lilikuwa limepanga foleni mbele yake.

Alisema malalamiko yao yalifikishwa kwa Meneja wa kituo hicho na kuwasuluhisha kwa kumuagiza dereva huyo kuwasihi abiria watelemke na kupanda kwenye basi lililokuwa mbele.

"Abiria waliteremka lakini wengi hawakwenda kupanda hilo basi wakasubiri la kwangu, kwa hiyo tukajikuta tumepata abiria mapema na kumpita njiani akiwa bado anatafuta abiria, kitendo ambacho naamini hakikumfurahisha," alidai.

Dereva huyo alidai Jumamosi baada ya kumaliza safari, alimkuta mfanyabiashara huyo katika baa moja iliyopo Kilema na kumsalimia, lakini alikataa kuitikia, akisema alikuwa akimtafuta kwa siku nyingi.

Alidai baadaye mfanyabiashara huyo alimfuata na kumnyang'anya kofia kisha kumpiga dereva huyo kwa ubao mgongoni na kuanguka na kwamba wakati akiwa katika harakati za kujitetea alimsukuma mfanyabiashara huyo na kuanguka.

"Niliamua kuondoka na kurudi mahali nilipoegesha basi, lakini akanifuata na kuchomoa bastola huku akisema lazima anivunje mguu ili nisimkoroge tena katika kupakia abiria," alidai.

Dereva huyo aliongeza kuwa baada ya kuchomoa bastola, baadhi ya wananchi waliojitokeza kuamua ugomvi lakini walikimbia, ndipo mfanyabiashara huyo alimpiga risasi na kutiwa mbaroni baada ya tukio hilo kuripotiwa polisi.
 
Sasa hapa tunakwenda pabaya; huyu bwana should be put away for a very looooong time!

WHY? (siyo kwamba namtetea lakini na wala simjui)

Mbona Ditto alifanya worse than that na akakaa ndani for only 3 months na sasa anapeta na magari ya Govt of TZ?

Samaki huoza kuanzia kichwani .............
 
Tumeshaanza kuwa Johannesburg ambako ugomvi wa ruti na abiria umalizika kwa risasi. Stori hii inaonyesha kuwa silaha zimetapakaa sana TZ na kuwa any Tom, Dick and Harry anaweza kuwa nayo bila proper scrutiny.
 
Nilitaka kujua je hiyo silaha anaimiliki kihalali? Nafikiri kuwepo na sheria maalum kwamba kabla mtu hajamilikishwa silaha, akapimwe akili kama hana kasoro, kwani ukiangalia issue kama hii ni kasoro ya akili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom