Dereva afunguka maajabu ya njiani: Kukutana na watu hawana vichwa na wengine watupu

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,520
2,000

Kutana na Allen Sherukinga ambaye yeye ni dereva magari makubwa na mabasi ya abiria mwenye uzoefu wa miaka 45 barabarani.

Anakuambia yeye hajawahi kupata ajali akiwa anaendesha gari kwa miaka yote hiyo lakini jambo ambalo leo anatueleza ni kuhusu matukio ambayo amekutana nayo barabarani wakati anaendesha gari.

Kwasasa Mzee Sherukinga ameshastaafu kuendesha magari makubwa yupo nyumbani kwake Lushoto Tanga akiendelea na bishara zake.

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,034
2,000
Mbona mambo ya kawaida,Usiku wa wsaa tisa nakaribia Nakaribiaa mlima Saranda...mwanzo nilifikitmri ni kiroba kimedondoka kutoka kwenye gari.

Kusogea zaidi nakaona sio kiroba kumbe ni mtu yuko ndani ya Sanda halafu anafurukuta
Mara akakaa ...wakati huo mimi nikajua ni mchezo ili nishangae wezi wadandie .

Mimi huwa muda wote natembea na Silaha nikashuka nikaenda nyuma ya tela sikuona mtu nyuma yagari nikarudi mbele sikumkuta yule kiumbe nikamuomba mungu nitatia gia Nikapanda Saranda mpaka Singida.

Visa vipo tena vingi wewe tembea drive usiku.
 
Hawachi

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
12,120
2,000
Mboma mambo ya kawaida,Usiku wa wsaa tisa nakaribia Nakaribiaa mlima Saranda...mwanzo nilifikitmri ni kiroba kimedondoka kutoka kwenye gari.

Duh huna uwoga mkuu hongera.
 
Ndumbusi

Member
Jan 28, 2019
10
45
Mboma mambo ya kawaida,Usiku wa wsaa tisa nakaribia Nakaribiaa mlima Saranda...mwanzo nilifikitmri ni kiroba kimedondoka kutoka kwenye gari.

Kusogea zaidi nakaona sio kiroba kumbe ni mtu yuko ndani ya Sanda halafu anafurukuta
Mara akakaa ...wakati huo mimi nikajua ni mchezo ili nishangae wezi wadandie .

Mimi huwa muda wote natembea na Silaha nikashuka nikaenda nyuma ya tela sikuona mtu nyuma yagari nikarudi mbele sikumkuta yule kiumbe nikamuomba mungu nitatia gia Nikapanda Saranda mpaka Singida.

Visa vipo tena vingi wewe tembea drive usiku.
Una huruma sana ungempitia tu na tairi kumaliza biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,034
2,000
Ukikutana na maiti au mtu wa ajabu usiku barabarani, usimkwepe, mgonge tu ndio usalama wako. Hata hivyo, kuepusha majanga, sali kwa jina la Yesu kabla hujaanza safari
Ni imani tu mimi kipindi cha miaka 90 ilikua ukitoka Manyoni kwenda Singida lazima upitie Itigi na barabara ilikuwa ni mbovu kwelikweli na haswa kwa gari la mizigo.

Nikia natembea polepole uziku wa saa Nne kama na nusu hakuna vijiji wala nyumba sehemu ile nikamuona mtoto wa kike kachakaa vumbi utasema hajaoga mwezi mzima nilikuwa nimepakia abiria tukaanza kuulizana huyu mtoto ametoka wapi?!

Mimi lile eneo nalijua nilishaona Simba nikasimamisha Gari nikamsogelea yule mtoto nikawa najari kumuuliza ...nyumbani kwenu ni wapi akawa ananiangalia tu.kila nikimsogelea na yeye anarudi nyuma..nikarudi kwenye gari nikaendelea na Safari wale abiria walikuwa wawili wakaanza kusema hao ni watoto waliogeuzwa kichawi

Kwa hiyo familia zao zinajua kuwa alishakufa...daaah!!!....nikasikitika sana kufika Itigi wale abiria na tandiboi wangu wakaanza kujisikia vibaya mara homa mara wanasikia harufu mbaya..lakini mimi sisikii chochote wakapendekeza tulale mpaka kesho yake mimi nikawa nasema hawa wanaogopa tu tukaamua kulala.
 
CHIEF WINGIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2013
1,029
2,000
Mishale ya saa 8 hivi tuligonga mtu pande za mkenge mkuranga tukasimama na kukagua gari ila hakukua na damu wala mbonyeo wowote kwenye body na hata asubuhi tukiwa tunarudi tulisimama na kuliza wenyeji wa pale kama kuna msiba au ajili iliyoua usiku wa jana walidai hakuna
Mwaka jana napo msata to bagamoyo road ilitupasa kusimamisha gari kabsa kupisha msafara wa watu ukivuka barabara walikua wengi aysee
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,351
2,000
Mboma mambo ya kawaida,Usiku wa wsaa tisa nakaribia Nakaribiaa mlima Saranda...mwanzo nilifikitmri ni kiroba kimedondoka kutoka kwenye gari.

Kusogea zaidi nakaona sio kiroba kumbe ni mtu yuko ndani ya Sanda halafu anafurukuta
Mara akakaa ...wakati huo mimi nikajua ni mchezo ili nishangae wezi wadandie .

Mimi huwa muda wote natembea na Silaha nikashuka nikaenda nyuma ya tela sikuona mtu nyuma yagari nikarudi mbele sikumkuta yule kiumbe nikamuomba mungu nitatia gia Nikapanda Saranda mpaka Singida.

Visa vipo tena vingi wewe tembea drive usiku.

Yaani mtu anafurukuta yupo kwenye sanda...akakaa.

Wewe ukasimamisha gari ukashuka ukaenda nyuma ya gari....okay!
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,034
2,000
Yaani mtu anafurukuta yupo kwenye sanda...akakaa.

Wewe ukasimamisha gari ukashuka ukaenda nyuma ya gari....okay!
Ninavyokwambia ndio hivyo,pili mimi natembea na chuma kwa kuongezea tu sanda imufungwa kwa nje .ni mimi nimempiga full light na kama mita thathini.
 
Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
2,662
2,000
Ni imani tu mimi kipindi cha miaka 90 ilikua ukitoka Manyoni kwenda Singida lazima upitie Itigi na barabara ilikuwa ni mbovu kwelikweli na haswa kwa gari la mizigo.

Nikia natembea polepole uziku wa saa Nne kama na nusu hakuna vijiji wala nyumba sehemu ile nikamuona mtoto wa kike kachakaa vumbi utasema hajaoga mwezi mzima nilikuwa nimepakia abiria tukaanza kuulizana huyu mtoto ametoka wapi?!

Mimi lile eneo nalijua nilishaona Simba nikasimamisha Gari nikamsogelea yule mtoto nikawa najari kumuuliza ...nyumbani kwenu ni wapi akawa ananiangalia tu.kila nikimsogelea na yeye anarudi nyuma..nikarudi kwenye gari nikaendelea na Safari wale abiria walikuwa wawili wakaanza kusema hao ni watoto waliogeuzwa kichawi

Kwa hiyo familia zao zinajua kuwa alishakufa...daaah!!!....nikasikitika sana kufika Itigi wale abiria na tandiboi wangu wakaanza kujisikia vibaya mara homa mara wanasikia harufu mbaya..lakini mimi sisikii chochote wakapendekeza tulale mpaka kesho yake mimi nikawa nasema hawa wanaogopa tu tukaamua kulala.
Nmesikitika sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
2,662
2,000
Mishale ya saa 8 hivi tuligonga mtu pande za mkenge mkuranga tukasimama na kukagua gari ila hakukua na damu wala mbonyeo wowote kwenye body na hata asubuhi tukiwa tunarudi tulisimama na kuliza wenyeji wa pale kama kuna msiba au ajili iliyoua usiku wa jana walidai hakuna
Mwaka jana napo msata to bagamoyo road ilitupasa kusimamisha gari kabsa kupisha msafara wa watu ukivuka barabara walikua wengi aysee
dooh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
5,517
2,000
Nimekumbuka mida ya saa nane usiku ndiyo kwanza tu nimeachana na Singida na kwenye gari niko mimi na rafiki yangu mmoja, ghafla hata bila mimi kujua nikajikuta nimehama upande na kuanza kupita upande wangu wa kulia huku gari linasoma 120 Km/hr na mbele yangu mita chache kuna Noah iko speed kama yangu nayo imekaa upande wa kulia, nahisi nilihamia huko baada ya ile Noah kuhamia kulia, mara ghafla kwa mbali( On the left hand side) naona mtu kalazwa Barabarani kwa haraka haraka ni kama kagogwa mda mchache uliyopita ajabu kafunikwa mwili mzima, dah nilipata vibrations mwili mzima lakini nikajikaza na bahati nzuri nilikuwa upande wa kulia so nikaongeza speed huku niko kimya ila navibrate hatari. Baada kama ya dakika tano navunja ukimya na kumuuliza mshikaji wangu, “ Oya dah umemwona yule mtu pale barabarani? Aisee kama tusingekuwa tumehamia kulia si ingekuwa hatari mwana? “
Jamaa yangu akanijibu
“ Oya mtu gani wewe? Acha kuzingua etii, kama umechoka tutafute mji karibu tulale mwana”.
Jamani usike ni noma jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
604
1,000
Mida ya saa tano usiku napandisha arusha,niko na mshikaji mmoja,kufika maeneo ya maimoria bums la kwanza kabisa kabla hujakata kona kuelekea sauti ya injili nikamwona mtu anavuka barabara,mwembamba mrefu kiasii,kavaa shati ya draft,kwa kua hatukua speed tukapunguza mwendo kumpisha avuke,ile amefika katikati akapotea,nikajua ni mimi mwenyewe nimemwona akipotea-yaani hakumalizia kile kipande cha bums kufika upande wa pili wa barabara, akavanish akiwa katikati ya barabara.
From there tukawa kimya hakuna aliemsemesha mwenzake,wakati tunajaza mafuta kituo cha panone,pale kimashuku,huku tukigonga serenget bariidii ndo jamaa akaniuliza Sonko vipi uliona mtu akivuka barabara alafu akapotea.Hapo ndo nikagundua haikua mbambaa jombaa !Ni kweli tulikutana na mtu wa ajabuu.

Sent using nokia ya torch
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom