Deogratias Nsokolo, Rais UTPC na kada wa CCM ni "kirusi"kwa waandishi wa habari nchini

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Deogratias Nsokolo, Rais UTPC na kada wa CCM ni "kirusi"kwa waandishi wa habari nchini

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratias Nsokolo ni kirusi kinachowauwa waandishi wa habari katika mapambano ya kudai haki na ukuaji wa tasnia hiyo kwa ujumla.

Rais wa UTPC ni kada wa CCM ambae ameshindwa kupambana na kushirikiana na waandishi wenzake katika kudai haki zao pindi Mwandishi wa habari anapopata mkasa.

Nsokolo ni kiongozi wa Klabu za waandishi wa habari zinazotetea na kuongoza wanahabari, siku chache zilizopita alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Nsimbo mkoani Katavi, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais huyu alitangaza nia hiyo akiwa bado ni Rais wa UTPC na Mwandishi wa habari mkoa wa kigoma akiiwakilisha ITV Tanzania.

Watu wengi wanajiuliza Rais huyu anatangaza vipi nia ya kugombea ubunge wakati bado ni kiongozi wa waandishi wa habari?

Hali hiyo, inasababisha wananchi kushindwa kumwamini na kuwaamini baadhi ya waandishi ambao hawafungamani na chama chochote cha siasa?.

Huyu Rais wa UTPC kabla ya kwenda kutangaza nia ya ubunge angetakiwa atangaze kuachana na nafasi zake za uongozi kwanza kama walivyofanya watu wengine.

Waandishi wengi ambao wamekuwa wakitangaza nia ya kugombea uongozi ndani ya vyama vya siasa ama ubunge mara nyingine wamekuwa wakiachia nafasi zao.

Miongoni mwa watu waliofanya hivyo, ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa ubungo Said Kubenea ambaye miezi miwili kabla aliachana na uandishi wa habari na kuingia kwenye siasa.

Kutokana na Nsokolo ambaye ndiye kiongozi wa waandishi nchini anapaswa kuona aibu na kujiuzuru nafasi ya urais wa UTPC kwa maslahi yake na ya waandishi wenzake.

Pia haitaleta taswira nzuri kwenye jamii kuongozwa na kada wa chama cha siasa ambaye ameonesha wazi itikadi yake.

Hata hivyo inaelezwa kwamba, katika uongozi wa Nsokolo wa miaka mitano akiwa Rais wa UTPC ameshindwa kusaidia waandishi wa habari nchini ambao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali.

Nsokolo miaka mitano, ameshindwa kuiongozo UTPC na tangu aingie madaraka hakuna kitu ama mabadiliko yanayonekana kwa macho.

Miaka mitano waandishi wamepitia misukosuko na kesi nyingi lakini Nsokolo hajawahi kushirikiana na wenzake katika kuhakikisha wanapata haki zao.

Nsokolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kigoma, UCCM wake umesababisha ashindwe kushirikiana na wenzake kupaza sauti kukabiliana na misukosuko wanayopitia.

..................................................................
 

Attachments

  • IMG_20200724_191455.jpg
    IMG_20200724_191455.jpg
    45.4 KB · Views: 1
  • IMG_20200724_191521.jpg
    IMG_20200724_191521.jpg
    32.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom