DEODATUS BALILE: The walter mitty character & new face of supermarket journalism in TZ

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,552
774
IMGP0224.jpg


Balile akionyesha "degree" yake aliyochukua Hull

Bellow ni article aliyoandika Balile in 2007 na majibu aliyopewa:
NIKIWA na matumaini chungu wa tele kuwa mpendwa msomaji wangu hujambo, leo nimeona ni vyema nitupie macho sekta mpya inayoibukia hapo nchini kwetu, ambayo kimsingi ni fursa na ufunguo wa kukuza uchumi wetu

Balile, hujaonyesha umefikia vipi conclusion kuwa conflict resolution ni sekta mpya inayoibuka nchini kwetu hebu fafanua zaidi.Kwani kwa upande wangu sidhani kama ni sekta mpya kwa nchi kama Tanzania ambayo imekuwa imekuwa ikimediate tangu tulipopata uhuru na mpaka leo hii inaendelea. Na kama ilivyo International Relations, conflict resoluton inaevolve tuu na tunaona roles za Non-State actors zikiwa zinatiliwa mkazo zaidi kutokana na wao kuwa na know how zaidi katika speciality fulani fulani...lakini unayo fursa ya kufafanua.

Sekta hii ni tawi jipya la huduma katika usuluhishi wa migogoro (conflict resolution). Nikijaribu kuangaza katika mitandao mbalimbali, kwa sasa jina la Tanzania linakuja juu kwa kiwango cha kutisha katika sekta hii ya usuluhishi wa migogoro. Yapo mataifa magwiji kama Uswisi, yenye kuaminika kuwa ni eneo salama kwa mazungumzo na mikataba mizito, na ndiyo maana leo ukiangalia mikutano inayofanyika Geneva, Uswisi, ni mingi kuliko maelezo. Geneva imekuwa nyumbani kwa mikataba mingi ya kimataifa, kuanzia sekta ya diplomasia, uchumi (ikiwamo Shirika la Biashara la Kimataifa – WTO), biashara na usuluhishi. Kwa bahati mbaya nchi hii haina maliasili kwa kiwango kikubwa. Viongozi wa taifa hili walilifahamu hilo na kuamua kuwekeza katika huduma. Uchumi wa Uswisi unategemea au unajiendesha kutokana na mapato yatokanayo na sekta huduma kwa asilimia 98.

Yah, ni kweli mji wa Geneva umekuwa ukiplay a very huge role kama sehemu ya kusaini mikataba mbali mbali ya kimataifa lakini jambo ambalo ni la muhimu zaidi ni kuwa umesahau kufahamisha watu kuwa moja kati ya sababu kuu ya Geneva kuwa na status hiyo ni kihistoria Geneva ilikuwa makao makuu ya League of Nations pale Palais Wilson kabla ya kuhamishiwa Palais des Nations na vile vile wao kuwa neutral wakati wa World War 2 ilipelekea kuwa favourite destination ya mayahudi wengi ambao walikua walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha na assets mbali mbali walikuwa wanauliwa katika nchi zingine za Ulaya na Uswisi pamoja na United States ndizo zilikuwa kimbilio lao of course secret banking system ya Uswisi ilikuwa inawahakikishia amana zao so in a way uko sawa ila ulitakiwa ufafanue zaidi role ya League of Nations and impact ya WW2 ambayo imeifanya uswisi kuwa ilivyo leo not only Geneva lakini miji kama Zurich na Berne.


Taifa hili lina benki kubwa na zenye fedha nyingi kuliko mataifa karibu yote duniani

Naomba kupingana na wewe kwenye hili na hata sijui data umezitoa wapi lakini naweka kukufahamisha kuwa hoja yako hapo juu iko very simplistic kwani hujafafanua au kuweka wazi..sasa naweza kukuweka sawa kwa kukupa data zifuatazo:


Top 4 Banking groups in the world ambazo ziko ranked by Shareholder equity ni:
CITI GROUP-United States
JP MORGAN-United States
BANK OF AMERICA-United States
HSBC-United Kingdom

Top 4 Banks in the world ambazo ranked by market capitalisation ni:

1 CITY GROUP- United States
2 ICBS-China China ICBC
3 BANK OF AMERICA- United States
4 HSBC- United Kingdom

Top 4 bank holding companies in the world ambazo ziko ranked by profit ni:

1 CITYGROUP- United States Citigroup
2 BANK OF AMERICA- United States Bank of America
3 HSBC- United Kingdom HSBC
4 JP MORGAN CHASE - United States

Bwana balile source ya data zangu ni hii hapa:

EURO MONEY: http://www.euromoney.com/page.asp?PageID=2050
ECONOMIST: Thinking big | The Economistsasa wewe umetumia vigezo vipi na reference zipi ku substantiate hoja yako?


na lilijiingiza katika biashara ya usiri wa kumbukumbu za fedha, ambapo viongozi wengi wa dunia hii hupora fedha katika mataifa yao na kuzihifadhi Uswisi. Nieleweke hapa, sisemi kuhifadhi fedha za wahalifu ni mchezo mzuri, lakini nataka kujenga hoja yenye kuonyesha walivyojipanga kuhakikisha sekta ya huduma inakuwa nguzo ya uchumi wao.sawa basi nami nitaendelea kusoma hoja yako ambayo umendelea kwa kudai hivi:


Taifa kama Uingereza ambalo ni visiwa vidogo vyenye ukubwa sawa na mkoa kama wa Morogoro vikichanganywa, lina uchumi mkubwa ajabu. Taifa hili la Uingereza limewekeza katika sekta ya huduma. Kama Uswisi, nao mikataba mikubwa mingi hutiwa saini hapa. Leo ukitafuta kampuni kubwa 10 za masuala ya uhasibu, zote zina makao makuu hapa London.


sawa sasa naomba source ya hii hoja

Kati ya kampuni 10 kubwa za masuala ya kisheria duniani, 6 zipo hapa Uingereza, tatu zipo Marekani na moja ina makao makuu ya umiliki wake Uholanzi na Uingereza (kwa wakati mmoja).

I beg to diiffer bwana Balile zijui unatumia data za mwaka gani na umefikia conclusion hii kivipi lakini naweza kukupa listi ambayo ni sawa na utaona katika top 10 UK ina law firms 4 tu .

CLIFFORD CHANCE- UK
LINKLATERS-UK

SKADDEN,ARPS,SLATE,MEAGHER & FLOM -USA
FRESFIELS BRUCKHAUS DERRINGER-UK
LATHAM &WATKINS-USA
BAKER McKENZIE-USA
ALLEN & OVERY-UK
JONES DAY-USA
SIDLEY AUSTIN-USA
WHITE &CASE-USAsource yangu bwana Balile ni hii:http://www.thelawyer.com/global100/Naomba utoe source ya namna ulivyofikia conclusion hii je hizo 4 nilizokutajia ni za UK au USA?

Mataifa haya sasa yanafunga viwanda na kuvihamishia India na China, huku yenyewe yakibaki kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa.


Blame it on Milton Keynes, Adam smith and Milton Friedman...au tuseme ni Laissez-faire economics ...GLOBALIZATION

Nimeyasema haya, yanisaidie kujenga hoja juu ya fursa tuliyonayo Watanzania katika usuluhishi wa migogoro ya kimataifa. Kazi anayoifanya Dk. Salim Ahmed Salim, ya kusuluhisha mgogoro wa Darfur, nchini Sudan, inalitangaza taifa letu kwa kiwango cha ajabu.Kwa vipi? inatusaidia nini? Je salim alipokuwa kule OAU tulifaidika na nini? argument yako iko shallow hapo hebu fafa nua zaidi

Habari nyingi zinazochapishwa zinaitaja Arusha kama kituo cha usuluhishi wa migogoro kilichobobea, ambapo wanarejea mgogoro wa Burundi na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari iliyopo Arusha. Leo mataifa mbalimbali yameanza kuamini kuwa ikiwa Afrika Kusini, inayoonekana kuwa mshindani mkubwa wa Tanzania katika sekta hii ya usuluhishi ikishindwa kusuluhisha mgogoro wa Zimbabwe, basi ikabidhiwe Tanzania, itauweza.


Jibu la hili ni kuwa kuwa msuluhishi kunahitaji fedha na je unajua tunapewa kiasi gani kuwa wasuluhishi wa migogoro hii? Je unajua kuwa wasuluhishi kumetitia umasikini kwa kiasi gani? kama serikali yetu haipati pesa za kutosha ili kufanikisha hii mikutano je unategemea sisi tutafanya miracle gani? Sisi kwa sasa kusuluhisha migogoro hii ya Great Lakes region ni sawa kwani matatizo yanayoendelea huko huwa yana spill kwetu hivyo its in our interest kufanya hivyo na kama kutangaza nchi then hilo ni jukumu la wizara ya Utalii ana akina Mwenguo. Uchumi wa South Africa unawaruhusu na hizo gharama kwao si tatizo. Je unahabari kama kuna proposal kuwa watanzania waishio nje watatozwa pesa za kuendesha balozi zetu kutokana na budget restrains? sasa hebu tupe data ni kiasi gani kinatumika kwa mwaka katika masuala haya ya conflict kama hiyo ya burundi na sisi pesa tunatoa wapi?? Je EU au UN wanatupa kiasi gani? lete supporting data..after all wewe ni graduate wa University huko UK

Imani hii kwa taifa letu, ni nguzo kubwa na chimbuko la maendeleo. Kwa nchi zinazotokea kupata fursa kama hizo, huo ndiyo mwanzo wa kutimua vumbi kuelekea mji wa maendeleo.
sawa
Najua yapo mataifa mengi yangependa kupata fursa hii ila kutokana na misingi fasaha aliyoijenga muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, taifa letu linayo fursa ya ziada; amani, utulivu na utengamano wa kisiasa.Sawa wakati wa Nyerere na sasa ni tofauti kwani Mwalimu alikuwa ni idealist na alikuwa yuko tayari kusacrifise maisha ya MTZ ili Mzimbabwe au Mu Angola aishi huru na salama lakini kama nilivyosema hapo awali mamabo yamebadilika na tusiwe tunafanya haya mambo for the sake of doing it especially kama hayana NATIONAL INTEREST kwetu.

Kimsingi kazi ya usuluhishi wa migogoro ni biashara kubwa.


enhe

Nasema ni biashara kwa misingi kuwa watu wetu watakaokuwa wanafanya kazi katika mabaraza au mahakama za usuluhishi, ni wazi watakuwa hawajitolei. Hawa watakuwa wanalipwa, kumbi za mikutano na hoteli wanapolala wahusika wakati wa mikutano vinalipiwa, bila kutaja chakula na matumizi ya ziada wanayofanya washiriki wa mikutano hii wanapokuwa hapo nchini.


Kabla hujaendelea narudia tena swali nililokuomba hapo awali, lete cost analysis iliyopelekea kwa ARUSHA ACCORD 1 & 2 then tuambiane local staff wanalipwa kiasi gani and so on then itakuwa launchpad nzuri ya kujengea hoja otherwise utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.

Hata hivyo, lipo jambo moja linalonitia wasiwasi kwa sasa. Jambo hili ni umahiri wa watu wetu hasa katika fani hii ya usuluhishi wa migogoro.enhe,

Kipo kizazi kilichofanya kazi Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miongo kadhaa na kupitia uzoefu au shule walizopata wakapata utalaamu unaotumika kushawishi na hatimaye kutatua migogoro hii.


Mimi sijakuelewa, hivi balile unataka tuendeleze vijana wengi katika fani hii ya conflict resolution wakati hujatoa mchanganuo jinsi gani tutanufaika vipi na hiyo kozi. Kama utasoma nakala zangu za nyuma nimekuwa ni critic mkubwa tuu humu ndani wa Bwana Membe na Foreign kwa ujumla lakini hii yako ni kali zaidi. Kwani hujaja na hoja thabiti juu ya hili na kama unhetaka then bora uje na data kamili ili kusupport argument yako. Kama ni revamp then naweza kukuambia kuwa civil service yetu nzima inatakiwa ifanyiwe revamp au reforms na kama issue ni MOFA then njoo na data mzee

Kwa kuwa wizara hii iliyopo chini ya Membe inayo dhamana ya usuluhishi wa migogoro, nimsihi aliangalie suala hili na kujaribu kutafuta hata vyanzo mbadala vya mapato, vijana wetu wanaoibukia wenye umri wa miaka 19 hadi 30, wapelekwe shule katika fani hii tuwe na wataalamu wa kutosha.


Yaani unataka Membe aangalie hila kwa kupropose AGE DISCRIMINATION, vipi mzee balile mbona hivi? je mtu akiwa na iaka 32 ndio hana nafasi au tumnyime?

Napendekeza umri huu kwa sababu hawa wakipata utalaamu kwa umri wao wataweza kulitumikia taifa kwa miaka 30 na zaidi, badala ya kupeleka shule kwa kiwango cha uzamivu mtu mwenye miaka 48, akirejea kutoka masomoni anatumikia miaka minne anastaafu kwa hiari au anaongeza miaka mitano na kulazimika kustaafu kwa mujibu wa sheria.sawa lakini usisahau kuwa experience ya wazee nayo inahitajika japo kwa mbali hoja yako inaelekea kufanana na ya Yakubu kuhusu kuwapa nafasi wazee na majibu yani ni kuwa Public sector yetu inatakiwa ifanyiwe reforms za hali yajuuu kama nilivyoshauri hapo awali

Itakuwa ni aibu kwa taifa letu kuwa na sifa ya usuluhishi wa migogoro, lakini watendaji wa mabaraza au mahakama husika wanatoka mataifa mengine na hakuna Watanzania wenye kufanya kazi hii.


Kweli kabisa lakini hujaeleza kwa nini hili hotokeaChonde chonde Membe lifikirie hili, na ikiwezekana ulitafutie ufumbuzi. Tukisuasua, fursa hii tutaipoteza. Mungu Ibariki Tanzania.
deobalile@yahoo.com – 0007904159144


Once again kama nilivyokuambia kuwa Membe budget yake ni ndogo sana na kama ni proposal basi nadhani ungeomba serikali iipatie wizara hii pesa zaidi lakini sidhani kama kuna haja ya kumwaga mapesa mengi kwenye conflict reslution huko Burundi na Congo ili hali tunashindwa kufanya hivyo kwenye mgogowa ZANZIBAR ambao uko ndani ya uwezo wetu nashangaa hujaliongelea hili

Natumai utarejea kujibu hoja zangu.


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom