Deo Mwanyika of Bulyanhulu convicted of Tax Evasion

deo alini inspire.

japo wengi waliofanyakazi nae wanamlaumu kwa kushiriki kuwanyanyasa vijana wazawa.(jamaa yangu alikuwa anamlaumu;kama bado hajamsamehe!?)

na hiyo hela ameshalipa kwa ukwasi aliojikusanyia..

bilioni 'is just a peanut' kwake,achilia mbali uwezo wa marafiki zake aliowainua kumchangia
 
Alikuwa anawalazimisha kwenda kufanya kazi? Hao walioenda, hawakuwahi kusikia kuwa wenzoa wamefia migodini?
Nyumbu wanafanya uamuzi gani kuvuka mto wenye mamba? WANA TARGET NA WANAJITOSA MTONI. Wengine wanadakwa na wengine wanaendeleza lengo. Pia corona hivo hivo tufanye kazi.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu leo imewahukumu aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara Exploration na Bulyanhulu, Deodatus Mwanyika na wenzake wawili, kulipa fidia ya TSh1.5 bilioni baada ya kupatikana na hati ya kukwepa kodi.

Imetoka wapi? Soma TAKUKURU yawakamata aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya Acacia, Deo Mwanyika na Alex Lugendo

===

The Kisutu Resident Magistrate Court has today ordered the Pangea, North Mara Exploration and Bulyanhulu Gold Mines President Deodatus Mwanyika (56) and his co-accused to pay compesation of Sh 1.5billion after they were found guilty of tax evasion.

The court also ordered the trio to pay an additional fine of Sh1.5 million fines or serve a jail term of four months.

The Resident magistrate Godfrey Isaya arrived at the decision after the accused pleaded guilty through a plea bargain arrangement at the office of the DPP.

Others also convicted alongside Mr Mwanyika on economic crimes charges number 37 of 2018 included Bulyanhulu Corporate affairs manager, Alex Lugendo (43) and the managing director of Pangea, North Mara and Bulyanhulu mines, Assa Mwaipopo (57).

Before the judgment was reach the state led by Paul Kadushi , Shadrack Kimaro and Wankyo Simon, claimed the case had come for judgment after the accused entered a guilty plea with the Director of Public Prosecution.

Out of the 39 charges, the accused faced one charge of not paying taxes worth $9,309,600 to the Tanzania Revenue authority

Source: The Citizen
Mission accomplished! TRA cum Kisutu Branch has of late become a major revenue collector.
 
Alikuwa anawalazimisha kwenda kufanya kazi? Hao walioenda, hawakuwahi kusikia kuwa wenzoa wamefia migodini?
Roho zetu waswahili huzijui??
Watu tuliomba kazi wenyewe kisha tukaridhia mikataba tukasaini sisi mwenyewe tukiridhia vigezo na masharti, leo tunamlaumu Deo, kisa tu, alikuwa boss kama mabeberu na mshahara wa kibeberu.

Nilifanya kazi migodini na sub contractors sijawahi kuwa na shida na hao mabeberu. Ndiyo walitupa mishahara ikatupa heshima mjini ati!

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
Sijui kwa nini Watanzania wengi huwa wana roho za ajabu ajabu. Wengi wanafurahia aliyefanikiwa, tena kwa njia halali, akipatwa na mabaya.

Deo alipoanza kazi Barrick, alikuwa Legal Manager. Kama Legal Manager, jukumu lake kubwa ilikuwa ni kutetea maslahi ya kampuni. Wewe mfanyakazi ukiishtaki kampuni, idara yake ndiyo ilikuwa na jukumu la kwenda kutoa defence kwa kampuni. Akifanya hivyo, wafanyakazi wale wasio na uelewa, chuki kwa Deo na wanasheria wake. Wao walitegemea mtu aliyeajiriwa kwaajili ya kuitetea kampuni, afike mahakamani aanze kumtetea aliyeishtaki Kampuni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi walikuwa na mob mentality, walijiingiza kwenye makundi ya kihalifu, wizi wa mafuta, ulevi kazini, kutokutii kanuni za afya na usalama, walivunja cardinal rules, kwa makusudi!

Walitaka Deo awatetee, ilhali naye ni muajiriwa kama wao na ana job description na score-card ya key performance indicators!
Inasikitisha mno, watz tu wavivu sana, tukitaka upendeleo hata kwenye vitu visivyo na tija!

Deo Mungu atamlipia...binafsi nimeyaishi maisha ya mgodini! Wanasiasa siyo watu wazuri kabisa!

Everyday is Saturday.......................... :cool:
 
Kiuhalisia, wamemtesa sana kwa kumweka mahabusu bila hatia.

Walisema anatuhumiwa kwa makosa 39, mojawapo uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Mishowe wameishia kwenye kosa moja la kukwepa kodi. Hivi tuhuma ya kukwepa kodi haina dhamana? Au yale makosa 39 yote yalikuwa ya kumbambikia ili ateseke?

Najua Deo hana hiyo pesa. Wala hana nyumba au rasilimali nyingine yoyote nje ya nchi. Alicho nacho chote kipo nchini, na kikubwa kuliko vyote ni hotel ya pale Njombe. Watu kwa dhamira chafu, wanataka kuwaaminisha watu kuwa Deo ni tajiri sana, jambo ambalo ni uwongo mkubwa. Hata huko bank, wamefuatilia sana, hana pesa yoyote. Wala hana hela yoyote nje ya nchi. Na wala hakuna ndugu au rafiki yake yeyote wa karibu aliyethibitika labda kutumika na Deo kumhifadhia hela. TISS wamefanya kazi miaka 3 kumfuatilia, hakuna pesa yoyote ya maana waliyomkuta nayo.

Lakini kwa vile dhahama zote dhidi yake ilikuwa kuwaadibisha ACACIA baada ya kupeleka notice ya kutaka kuishtaki Serikali, ACACIA/Barrick watalazimika kuilipa hiyo fine.

Watanzania tuache chuki zisizo na msingi wowote.

Barrick wamlipie hiyo fine, maana ameteseka kwa sababu yao. Angalao baada ya mateso ya zaidi ya mwaka mzima, akaungane na famikia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hela anayo au anajua nani atamlipia,vinginevyo asingeingia mkataba huo na mwanasheria wa serikali AG,anajua analofanya huwezi peleka maombi hayo kama unajua huna hela
 
Aise nimesoma comments hapa. Kama ni kweli, huyu jamaa hafai. Ndio kielelezo kikuu kwanini Afrika inafeli na kuwa ngumu- ni watu kama hawa. They dont care about their own people busy to impress the white people who dont care about him and his kind .
 
VIONGOZI WA ZAMANI WA ACCACIA WAHUKUMIWA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu aliyekuwa makamu wa Rais wa Kampuni ya Acacia, Deodatus Mwanyika na wenzake kulipa fidia ya shilingi bilioni 1.5 na faini ya shilingi milioni 1.5 au kifungo jela cha miezi minne baada ya kukiri mashitaka ya kukwepa kodi.
 
Back
Top Bottom