Deo Mwanyika of Bulyanhulu convicted of Tax Evasion

Deo na alaaniwe Milele na kizazi chake!

Dhulumati kubwa na jitu lililonyanyasa sana watz wenzalo pale Acacia.
Wewe una matatizo yako. Namfahamu huyu bwana na nilifanya kazi Bulyanhulu. Unaweza kutoa mfano japo mmoja wa namna alivyowanyanyasa wafanyakazi? Nijuavyo hakuwa na direct contact na wafanyakazi. Kazi zake zaidi zilikuwa kwenye corporate, wewe alikunyanyasaje?

Sina shaka, yawezekana ulikuwa na matatizo ya kiutendaji. Siku zote utabakia kulaumu watu wengine wakati matatizo yapo upabde wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu deo ametajirika kwa jasho la watanzania maskini...

Watu wamekufa sana migodini.. huku huyu deo anashirikiana na wazungu kufunika vifo..

Mtu kama huyu ni wa kufilisiwa .. na kufungwa jiwe kubwa na kutoswa baharini
Hapana unamwonea kusema hivyo eti kwa jasho la waTz. Serikali ndiyo iliyoingia mikataba na mwajiri wa DEO. SERIKALI ndiyo iliyo ona iwape mabeberu aridhi ili ipate kodi. Juzi kati may serikal imepokea pesa toka kwa haohao waajiri wa DEO why Deo aonekane anamakosa?
 
Alikuwa anawalazimisha kwenda kufanya kazi? Hao walioenda, hawakuwahi kusikia kuwa wenzoa wamefia migodini?
Mkuu, huyu Deo alishiriki kupindisha sheria na kuwakandamiza waTanzania walio kuwa wakifanya kazi na wengine walikufia pamoja na kujeruhiwa wakiwa kazini.
 
Hivi huyu nwanyika si alipata kuwa waziri enzi za mkapa au nafananisha jina?
 
Hiyo hukumu haina mabadala wa kufungwa? maana ni heri kumalizia maisha kifungoni kuliko kuwaacha watoto maskini wa kupindikia
Hiyo hela Mwanyika analipa bila shaka
TZS 1.5 billion ilipwe BILA SHAKA? unless kama ACACIA ndo wanalipa
Akilipa hiyo fine atakuwa tajiri sana, 1.5b kwa individual person sio jambo dogo, au asaidiwe na kampuni.
Jamaa atalipa, namfahamu Deo vizuri
 
Toka maktaba :

17 Oct 2018
Aliyekuwa rais wa Migodi ya Pangea, Mwanyika asomewa mashtaka 39 Kisutu.

Rais wa Migodi kizimbani Dar kwa kukwepa kodi ya dola milioni 112.

More info :

Machi 30, 2019
Tanzania : Upelelezi kesi ya Barrick unaendelea, Mwanyika, Lugendo warudishwa rumande

Waendesha mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na wenzake, wamedai mahakamani upelelezi bado ungali unaendelea chini ya usaidizi wa nje ya nchi.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Aprili 11, 2008 na Juni 30,2007, katika sehemu tofauti za Jiji la Dar es Salaam, na mikoa ya Kahama, Shinyanga, Tarime (Mara) na (Biharamulo) Kagera maeneo ambayo yako katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maeneo mengine ambayo washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo ni katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto (Canada) na Uingereza.

Aidha, Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutoa tamko la uongo kwa Kamishna Mkuu wa TRA huko Biharamulo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi Dola za Marekani, 9,309,600 ambayo ilipaswa kulipwa TRA.

Mwanyika na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 39, ikiwemo madai ya kutakatisha fedha na kukwepa kodi ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 112, gazeti la Nipashe limeripoti nchini Tanzania.

Katika shtaka la kutoa nyaraka ya uongo, Mwanyika anadaiwa kuwa Aprili 30, mwaka 2018, katika Benki Kuu ya Tanzania, Ilala jijini Dar es Salaam, inadaiwa kwa makusudi aliwasilisha nyaraka ya uongo ya mkopo baina ya kampuni mgodi wa Bulyanhulu na Barrick International Bank Corp kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, kati ya Juni 2001 na Desemba 13, 2007 Bulyanhulu walijipatia mkopo usio na faida wa Dola za Marekani, 416,100,000 kutoka Barrick.

Maelezo hayo yalitolewa Ijumaa na Wakili wa Serikali, Simon Wankyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kevini Mhina.

Washtakiwa wengine katika kesi hii ni Meneja Uhusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu, Alex Lugendo;Mkurugenzi Mtendaji wa Pangea, North Mara na Bulyanhuku, Assa Mwaipopo, kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba 17, mwaka 2018.

"Mheshimiwa Hakimu upelelezi wa kesi hii bado unaendelea chini ya usaidizi wa nje ya nchi. Tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa," alieleza Wankyo.

Hakimu alisema kesi hiyo itatajwa Aprili 12, mwaka 2019, na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kundi la pili wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, mashtaka saba ya kughushi, mashtaka 17 ya utakatishaji wa fedha, kuwasilisha nyarakaza uongokwaMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa shtaka moja, mashtaka manane ya kukwepa kodi na moja la kutoa rushwa.

Pia Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kuwa kati ya Desemba, 2009 na Desemba 31, mwaka 2018, katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi ya Tanzania, kwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani, walisaidia mgodi wa North Mara kuhamisha Dola za Marekani, 374,243,943,45, huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa ya kughushi na kukwepa kodi.

Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Novemba 2, 2012 na Novemba 27, 2015 huko Shinyanga walitoa rushwa ya Sh. 718,520,001.76 kwa Hussein Kashindye ambayeni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa (RCO) wa Shinyanga kwa lengo la kumshawishi ili aachane na uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyokuwa yametendwa na mgodi wa Bulyanhulu.

Katika shtaka la kughushi, washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai, wanadaiwa walighushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30, 2014 Kampuni ya Pangea Limited ilikubali kukopa USD 90,000,000 ikiwa na riba kutoka benki ya kimataifa ya Barrick, huku wakijua kuwa si kweli.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC
Source :
Tanzania : Upelelezi kesi ya Barrick unaendelea, Mwanyika, Lugendo warudishwa rumande
 
Hapana unamwonea kusema hivyo eti kwa jasho la waTz. Serikali ndiyo iliyoingia mikataba na mwajiri wa DEO. SERIKALI ndiyo iliyo ona iwape mabeberu aridhi ili ipate kodi. Juzi kati may serikal imepokea pesa toka kwa haohao waajiri wa DEO why Deo aonekane anamakosa?
Atakuwa labda alikwepa kodi kwenye biashara zake binafsi.
 
Hiyo hukumu haina mabadala wa kufungwa? maana ni heri kumalizia maisha kifungoni kuliko kuwaacha watoto maskini wa kupindikia
Barrick italipa hiyo faini lakini Deo Mwanyika atabaki kwenye kumbukumbu za wafanyakazi wengi wa migodi ya Barrick kwa kuminya haki za Watanzania na kukumbatia Mabeberu.
 
Kiuhalisia, wamemtesa sana kwa kumweka mahabusu bila hatia.

Walisema anatuhumiwa kwa makosa 39, mojawapo uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Mishowe wameishia kwenye kosa moja la kukwepa kodi. Hivi tuhuma ya kukwepa kodi haina dhamana? Au yale makosa 39 yote yalikuwa ya kumbambikia ili ateseke?

Najua Deo hana hiyo pesa. Wala hana nyumba au rasilimali nyingine yoyote nje ya nchi. Alicho nacho chote kipo nchini, na kikubwa kuliko vyote ni hotel ya pale Njombe. Watu kwa dhamira chafu, wanataka kuwaaminisha watu kuwa Deo ni tajiri sana, jambo ambalo ni uwongo mkubwa. Hata huko bank, wamefuatilia sana, hana pesa yoyote. Wala hana hela yoyote nje ya nchi. Na wala hakuna ndugu au rafiki yake yeyote wa karibu aliyethibitika labda kutumika na Deo kumhifadhia hela. TISS wamefanya kazi miaka 3 kumfuatilia, hakuna pesa yoyote ya maana waliyomkuta nayo.

Lakini kwa vile dhahama zote dhidi yake ilikuwa kuwaadibisha ACACIA baada ya kupeleka notice ya kutaka kuishtaki Serikali, ACACIA/Barrick watalazimika kuilipa hiyo fine.

Watanzania tuache chuki zisizo na msingi wowote.

Barrick wamlipie hiyo fine, maana ameteseka kwa sababu yao. Angalao baada ya mateso ya zaidi ya mwaka mzima, akaungane na famikia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa ana Mali nyingi alizovuna na wazungu alinyanyasa sana wafanyakazi wenzake mno
 
Bams umenena ukweli hakukuwa na haja ya kumtesa kiasi hicho kama kosa lilikuwa ni hilo ..

Kuhusu Mali labda tuseme hakunafaida ya kuzitaja kwani waupande wake nikushukuru wamembainisha kosa na adhabu yake. Ila no zaidi ya ile Hotel
 
Attachments

  • 2018-08-14.jpg
    2018-08-14.jpg
    12.4 KB · Views: 1
mkuu uliwahi kufanya kazi buly sasa hiv upo upande gani?
Wewe una matatizo yako. Namfahamu huyu bwana na nilifanya kazi Bulyanhulu. Unaweza kutoa mfano japo mmoja wa namna alivyowanyanyasa wafanyakazi? Nijuavyo hakuwa na direct contact na wafanyakazi. Kazi zake zaidi zilikuwa kwenye corporate, wewe alikunyanyasaje?

Sina shaka, yawezekana ulikuwa na matatizo ya kiutendaji. Siku zote utabakia kulaumu watu wengine wakati matatizo yapo upabde upo
 
Kiuhalisia, wamemtesa sana kwa kumweka mahabusu bila hatia.

Walisema anatuhumiwa kwa makosa 39, mojawapo uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Mishowe wameishia kwenye kosa moja la kukwepa kodi. Hivi tuhuma ya kukwepa kodi haina dhamana? Au yale makosa 39 yote yalikuwa ya kumbambikia ili ateseke?

Najua Deo hana hiyo pesa. Wala hana nyumba au rasilimali nyingine yoyote nje ya nchi. Alicho nacho chote kipo nchini, na kikubwa kuliko vyote ni hotel ya pale Njombe. Watu kwa dhamira chafu, wanataka kuwaaminisha watu kuwa Deo ni tajiri sana, jambo ambalo ni uwongo mkubwa. Hata huko bank, wamefuatilia sana, hana pesa yoyote. Wala hana hela yoyote nje ya nchi. Na wala hakuna ndugu au rafiki yake yeyote wa karibu aliyethibitika labda kutumika na Deo kumhifadhia hela. TISS wamefanya kazi miaka 3 kumfuatilia, hakuna pesa yoyote ya maana waliyomkuta nayo.

Lakini kwa vile dhahama zote dhidi yake ilikuwa kuwaadibisha ACACIA baada ya kupeleka notice ya kutaka kuishtaki Serikali, ACACIA/Barrick watalazimika kuilipa hiyo fine.

Watanzania tuache chuki zisizo na msingi wowote.

Barrick wamlipie hiyo fine, maana ameteseka kwa sababu yao. Angalao baada ya mateso ya zaidi ya mwaka mzima, akaungane na famikia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
R.i.P John Eliud
R.i.P. Kadelema
R.i.P. Majige Jr

Pole ziwafikie yule jamaa alie katika mkono, hapo walio katika vidole na wengi walio pata maumivu ya mgongo pamoja na walio poteza kusikia, na wenye matatizo ya mapafu.......
Dahhhh mkuu nimejikuta nakumbuka mengi sana aliyo yapindisha Deo ilkhali hakuwahi kuweza kukaa hata lisaa limoja pale 4820, 4700, 4480, 4440, Zone zero, zone three, deecline na kadhalika...
 
mkuu uliwahi kufanya kazi buly sasa hiv upo upande gani?
Huyu jamaa anadhani anayajua mengi wakati hakuna analo lijfahamu.
Deo aliwaumiza sana wafanyakazi wa Bullyanhulu.
Nakumbuka miaka flani ya 2000 mapema, aliwahi kutranslate English to Swahili kwa kutaka kuwatetea mabeberu, hali iliyo leta tafarani kubwa hadi Bwana Jery Magimila akaomba apewe mic ili aseme mwenyewe alichotaka kumwambia General Manager.
 
Back
Top Bottom