Deo Mwanambilimbi, Allain Mulumba Kashama mbaroni kwa uhamiaji haramu

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Deo M.jpg

Deo Mwanambilimbi
Alain Mulumba.jpg

Alain Mulumba Kashama

IDARA ya Uhamiaji imewatia mbaroni wanamuziki mashuhuri Deogratius ‘Deo’ Mwanambilimbi, rapa maarufu Alain Mulumba Kashama na Mwenabantu Kibyabya Michel wakihusishwa na uhamiaji haramu katika kutekeleza kauli mbiu ya Rais John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Mbali ya kuwakamata wanamuziki hao, Uhamiaji pia imemtia mbaroni Abdulahi Suleiman Mberwa kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha binadamu kuwapeleka nje ya Tanzania.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji nchini, John Mfumule. Zaidi HAPA
 
Nimeshangaa kuona wasanii wanasema hawana vibali vya kuishi sababu hawana pesa za kulipia
 
'Siwezi sema kwaniniii.. Niliachana na yeye..
Siwezi taja sababu.. Ya kutengana na yeye..
Mapenzi yangu naye yalikuwa ya hadithi.. Mapenzi yangu naye yalikuwa ya hadithi ooh!
 
Khaaaaa wale Wachina,Wahindi na Wazungu wanaozurura tu mitaani vipi nao bora hata bana Congo wanatupagha mandombolo.
 
Deo mwanambilimbi ni mtanzania unless amekutwa amewahifadhi wahamiaji haramu. Baba yake alikuwa mkuu wa wilaya au mkoa enzi ya Nyerere sasa sijui wamemkamata kivipi
 
Deo ni mbongo mie nimesoma na mdogo wake tena baba yao alikuwa kigogo serikalini enzi za mwalimu
 
Back
Top Bottom