Deo Kamugisha kiongozi wa mtaa mfano wa kuigwa

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,404
Nimefurahishwa na kitendo cha mwenyekiti wa mtaa Deo Kamugisha kuhamasisha wakazi kusafisha eneo la makaburi na hatimae kuhamasisha watu kujenga uzio. Ukweli hakuna sehemu ya hovyo na chafu kama maeneo ya makaburi, mambo ya kishenzi na ya kishetani hufanyika huko.

Cha kushangaza msiba ukitokea sie ndio wa kwanza kuwapeleka mashehe mapadri na wachungaji kwenda kuombea dua wapendwa wetu. Hebu tujitume angalau kuyafanyia usafi kwa kufyeka vichaka na kung'oa mbigili.
 
Back
Top Bottom