Deo/Gidion Mlele Polisi mpelelezi tapeli, anafanya shughuli Ofisi ya M/Kiti Mtaa wa Mbondole Ilala

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,892
22,649
Kwanza niwape pole kwa kuondokewa na askari wetu 8 kule kibiti Mwenyezi Mungu awahifadhi mahara pema peponi ,ameen

Kuna kijana anajiita Deo lakini kwa uchuguzi wangu nimebaini anaitwa Gidion Mlele ,huyu amejipa upolisi mpelelezi na anafanya shughuli zake katika ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Mbondole Ilala jijini Dar.

1. Amewatapeli watu kuwa atawaunganisha JKT kwa kiasi cha 7 za kitanzania ,amechukua laki mbili za dada mmoja hivi eti atamuunganisha mdogo wake apate nafasi.Analichafua jeshi la polisi kwa watu kuamini kiwa yeye ni askari.

2. Amemtapeli mganga mmoja kuwa anaweza kumsaidia ndugu yake apate dhamana ya kesi ya silaha ambaye yupo Keko tangu akamatwe mwaka jana.Amelipwa 1.5 ikiwa ni malipo ya awali kwani alihitaji million 1.5 huku akijua kuwa kesi ya silaha haina dhamana

3. Anakamata watu na kuwashikilia katika ofisi ya mtaa mpaka apewe pesa ,nani amemruhusu huyu kama ni polisi kufanyia kazi za kipolisi kwenye ofisi ya mtaa?

4. Anakamata bangi na akipewa pesa anawaachia wakishindwa anakwenda kuuza kwingine ,nimemfuatilia na kujua mengi of course anajiamini sana ,ukimwuliza kitambulisho anakujibu eti kimepotea

5. Anafanya kazi hizi peke yake muda wote anakamata yeye,anashikilia yeye na kuhukumu yeye.

Waziri Mwigulu wewe na RC Makonda ni member humu tusaidiane kuondoa watu hawa wanachafua taswira ya jeshi letu adhimu mbele ya jamii.

Kwa taarifa zaidi, pm pls

cc
Mwigulu Nchemba
Paul Makonda
 
Ujumbe umefika na umeeleweka lakini jifunze matumizi ya "l" na"r"
 
Back
Top Bottom