Deo Filikunjombe: Serikali ni sawa na saa mbovu iliyosimama

Wakuu, nimeshangazwa na alichokisema Mh. Deo Filikunjombe, mbunge wa Ludewa, kwamba Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa ombaomba Duniani. Na ametia mkazo kwamba tunaomba bila sababu za msingi, moja ya saba kuu ni kwamba serikali ya Magamba haina nidhamu katika tutumia fedha tulizonazo, hali ambayo amesema hatutaendelea hata kama mapato yataongezeka mpaka wapi. Kwa hali hii, maoni yangu ni kwamba hii serikali imepoteza uhalali wa kuongoza.[/QUOTE]

ver good we need changes now!!!!!!!!!!!!!!!!!111111
 
kuwa mbunge wa ccm lazima uwe na uthubutu, kwa kauli hii lazima aitwe na kamati mitusi ya kina Lusinde, Komba na yule mchumi nambari one nchini tanzania aka mzee wa kuzoa mizigo ya watu ili akajibu tuhuma kabla ya kupelekwa kwenye kamati ya maadili na baadaye wamfukuze uanachama.
 
Ukweli utabaki pale pale rais ni dhaifu na ccm ni wapuuzi wasipo ondoa upuuzi itakuwa ngonjera tu
 
katika wabunge wa CCM ambao sio wanafiki huyu mheshimiwa anaongoza...keep it up Deo Filikunjombe..
 
Anasaka uwaziri huyo, Simbachawene yuko wapi? na huyo MR Masifa a.k.a machemba Mbunge mpotoshaji wa Msimu wote wanausaka wakiupata maneno yao ya ovyo utayakuta kwenye wall zao fb kama wapambe wengine waliokabidhiwa unaibu waziri januari mikamba, MAGAMBA NI MAGAMBA Haijalishi nila KOBE au La NUNGUNUNGU kama Shibuda. Namshukuru Mh. Mbowe kutangaza kuinyima Vyeo CHADEMA. Nawachukia wabunge Dhaifu wa sisiemu na ya Chukia Magamba wote
 
Iraq and Afganistan inajulikana ni kutokana na vita vya muda mrefu na tawala za kiimla kwa muda mrefu kwenye nchi hizo thats why wana alocate pesa nyingi kwenye hili na hakuna suala la uwekeza wa maana wala uzalishaji n.k kitu kinachowafanya hata mapato yao ya ndani kuwa ya kusuasua sasa sisi na mirasili mali yetu yooote tuliojaliwa.. kweli nafasi ya tatu (3) kwa kuomba omba duniani mmhmh hainingii akilini
 
Amemchana RAISI kiaina kwa kuwaambia wabunge kuwa "tunamwaibisha raisi wetu kwa kumfanya ombaomba kwa vile kila siku anasafiri kwenda kuomba misaada wakati serikali haiwezi kusimamia hata kile kidogo tulichonacho. Nadhani Lukuvi alipaswa kumwombea mwongozo huyu mheshimiwa kuliko Mh. Mnyika!
 
Kwa hiyo Jk naye siku moja Mnyika anaweza akafuta kauli yake ya Rais ni Dhaifu endapo Jk atamridhisha?.
The unseen is illustrated by the seen.

Akawaridhishe magamba wenzie na sio watu ambao wanathubutu kusema ukweli uliowashinda kusema hadharani. Mnabaki kumfurahisha Mr. Dhaifu huku mnaugulia maumivu.
 
Ni vigumu sana kupambana na adui unayeishi nyumbani kwake. Walijaribu akina Kilango wakaishia kulamba miguu ya watawala, kijana kama yuko serious avae gwanda

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Dk. Slaa aliwahi kusema Anne Kilango ni mnafiki.
 
Mimi natoka Ludewa nafurahia sana sana Mbunge wangu anafanya vizuri mambo yake ila tuu ninaweza nikamyima kura kwa vile ni CCM kwa hoja ya msingi atakapopiga kampeni atasifia CCM, halafu kumchagua mbunge wa CCM ni kujenga CCM kwa litafanya nisimchague? cha msingi nitamuomba aje upinzani ili mwaka 2015 awe waziri wa Chama tawala CHADEMA.
 
Kuifananisha ccm na saa mbovu ni kuipandisha chati. Maana walau saa mbovu huwa sahihi mara mbili kwa siku. Lakini ccm tuliyonayo sasa haina usahihi hata wa sekunde moja!
 
Maskini Tanzania nchi yangu. Ni moja kati ya nchi zenye utajiri mkubwa wa raslimali lakini tumo kwenye "tatu bora" ya ombaomba duniani !!!!!!!!
Viongozi wetu wakiambiwa ni dhaifu wanafura kama Nyati aliyejeruhiwa.
 
Mimi natoka Ludewa nafurahia sana sana Mbunge wangu anafanya vizuri mambo yake ila tuu ninaweza nikamyima kura kwa vile ni CCM kwa hoja ya msingi atakapopiga kampeni atasifia CCM, halafu kumchagua mbunge wa CCM ni kujenga CCM kwa litafanya nisimchague? cha msingi nitamuomba aje upinzani ili mwaka 2015 awe waziri wa Chama tawala CHADEMA.

hv wakhunyumba...
mbona waludewa na njombe wanaipenda sana ccm ingawa jamaa amefanya angalau ludewa kwetu kujulikane
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom