Deo Filikunjombe: Serikali ni sawa na saa mbovu iliyosimama

amezitaja nchi zinazoongoza kwa kukopa ni Afghanistani, Irak na Tanzania

mkuu! Afghanistan na Iraq ni nchi ambazo zimepita katika vita sio ishu hata zikiwa omba omba sio hii tanzia ina miaka 51 ipo huru inaomba mpaka vyandarua na raisi anahongwa suti na waarabu hii ni aibu sana
 
Huyu ndie mbunge makini kuzidi wote CCM katika bunge la sasa, hapendi unafiki wala uzandiki kama walivyo wengine vinyonga wanabadirika kila mara pasi na sababu wala hoja ya maana. Wamalizie kipindi chao hiki ili 2015 wakalime waone kuwa sera ya kilimo kwanza haitekelezeki kwa vitendo ila ni kiini macho.
 
Deo ni Jembe namkubali.Tz ya tatu kwa omba omba duh! Kumbe hatutakiwi kuwalaumu akina matonya na washikaji wake na unga mkono akina matonya waendelee kuomba
 
Hop wapo wanao'm'beza

Tena wengi sana!

Zakia Meghji alikuwa amekaa nyuma Deo Filikunjombe na wakati wote alipokuwa anaongea, alionekana mwenye hasira sana!!

Hata hivyo, naamini maisha yake ndani ya chama chao ni mafupi sana (i.e his days are numbered)!!
 
Fikirikunjombe ni mbunge makini. Kama wakimzingua ni bora aje Chadema tutampokea. CCM hawapo tayari kupokea challenge za namna hii.
 
amezitaja nchi zinazoongoza kwa kukopa ni Afghanistani, Irak na Tanzania

Iraq and Afganistan inajulikana ni kutokana na vita vya muda mrefu na tawala za kiimla kwa muda mrefu kwenye nchi hizo sisi je?? Unajua mafisadi wanatumaliza tukiwa tuinaona maana pesa ambazo wanakopa nakuingiza kwenye mifuko yao zinageuka kuwa deni la taifa ambalo sisi watanzania wafanyakazi, wafanyabiashara hata wakulima kupitia kodi tunalipa deni hilo pesa amabazo mafisadi wamechukua! ndio maana unaona deni linatanuka hakuna maendeleo pesa inatunisha mifuko ya mafisadi!!
 
Sio kuwa wabunge wengine wa CCM sio makini, tatizo lao ni kuangalia matumbo yao kwanza na sio nchi kwa ujumla wake. Huwezi kuniambia kuwa wabunge wa CCM hawajui kuwa nchi inaangamia kiuchumi na hawajui kuwa hakuna hela iliyotengwa kwa ajili ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano, au hawajui kuwa bajeti ile ni kiini macho tu kama ile ya mwaka jana ambapo wizara zimepata pungufu ya zile walizoahidiwa. Unafiki ndio umewazidi ndio mana wanachumia matumbo yao tu
 
Fikirikunjombe ni mbunge makini. Kama wakimzingua ni bora aje Chadema tutampokea. CCM hawapo tayari kupokea challenge za namna hii.

Mmeesahau kipindi kile anasutwa na wabunge wa kike wa chadema? hivi alikuwa amekosea nini kipindi hicho? Na ni kwa nini siku hizo alikuwa adui wa wana Chadema humu Jf na sasa anaonekana kipenzi cha wanachadema humu jamvini?. Tanzania yetu hii, mambo huja na hupita watu wakasahau.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu.
 
Huyu ndie mbunge makini kuzidi wote CCM katika bunge la sasa, hapendi unafiki wala uzandiki kama walivyo wengine vinyonga wanabadirika kila mara pasi na sababu wala hoja ya maana. Wamalizie kipindi chao hiki ili 2015 wakalime waone kuwa sera ya kilimo kwanza haitekelezeki kwa vitendo ila ni kiini macho.

kweli bwana umeongea poinT.. NAMUOMBEA MAISHA MAREFU DEO ABLIKIWE
 
Mbona hiyo kauli haina tofauti na ya yule aliyesema rais ni dhaifu!!!?
 
Tupo hapa tulipo kwa sababu ya UDHAIFU wa Rais Kikwete, Bunge legelege na upuuzi wa CCM- J J Mnyika - Mbunge Ubungo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom