Deo filikunjombe mtu msafi je petrol station yako kwanini uliuza wakati wa kampeni??

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
477
120
Kama Haumjui Deo filikunjombe nenda ludewa.

Jamaa ameshajua safari yake na Magamba imekuwa nzito baada ya kutambua miguu haina nguvu tena ya kukimbia. Deo amejikuta akiwa na ugomvi kila mara na watendaji wa halmashauri kwakuwa hawakufanya kile alichokitaka wakati wa uchaguzi "Ushindi wa Kishindo" ile nae aonwe walau apewe kawizara aka "ulaji" Deo alishiriki katika hila mbali mbali ikiwa ni kumnunua mwenyekiti wa chadema Ludewa na kumtangaza Mpinzani ambaye hakuwa anakubalika.......wakati CC ilimtaka mwingine.... Deo ndio amelobby Mradi wa Umeme na Maji uwe katika Kata ya wazazi wake kwa kutumia influence yake na ukaribu na wazungu.....Deo toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzako......
 
Sungura kuruka ruka, mtini akasogea...
akayaona matunda, mtini yameenea...

......Sizitaki mbichi hizi.
aha ha ha!! lo! aka kanyimbo/kashairi katamu kweli, nakapenda.
 
Baada ya kuenda against na Magamba leo mnamuona hafai na ana bonge la Boriti?
 
I know the place huko ni kutapatapa kwa wafa maji tuuu! Kwanini haya yaje baada ya mheshimiwa kusaidi form ya Zito?
 
sasa kuuza stesheni yake si alikuwa anatafuta fedha za kampeni? Na huo mradi wa maji si bora ye aliyevutia kwa wazazi wake na wananchi wengine wa karibu wanafaidi? Si kuna wengine dar wameyeyuka na mabilioni ya bucha na haipo kabisa? Au amejenga bomba moja kwao tu? Umesahau kwamba kuna miradi mingi ya maji imeishia njiani na fedha hazipo? Nani tumuone anafaa? Kumnunua mwenyekiti wa cdm una ushahidi? Kuna sehemu nyingi tulisikia mambo hayo mf ismani,musoma lakini kumbuka tunaenda na ushahidi vinginevyo kila kinachosemwa kingekuwa kinafunga watu.
 
Sasa ulitaka mradi wa umeme aupeleke kwa wazazi wa nani kama sio wake? Mbona Magufuli alipindisha barabara kupitia Chato na bado tunamuita mchapa kazi? Charity starts at home.

Na kama aliuza petrol station, hilo si kosa kwani kimfaacho mtu chake. Mbona serikali iliuza viwanda vya Watanzania na watu hatuongei?
 
Mleta mada maji ya shingo yamemfika.anatafuta pa kumpa ahueni ndo kaamua ajishike kwa bw.filikunjombe.
 
Kama Haumjui Deo filikunjombe nenda ludewa........jamaa ameshajua safari yake na Magamba imekuwa nzito baada ya kutambua miguu haina nguvu tena ya kukimbia. Deo amejikuta akiwa na ugomvi kila mara na watendaji wa halmashauri kwakuwa hawakufanya kile alichokitaka wakati wa uchaguzi "Ushindi wa Kishindo" ile nae aonwe walau apewe kawizara aka "ulaji" Deo alishiriki katika hila mbali mbali ikiwa ni kumnunua mwenyekiti wa chadema Ludewa na kumtangaza Mpinzani ambaye hakuwa anakubalika.......wakati CC ilimtaka mwingine.... Deo ndio amelobby Mradi wa Umeme na Maji uwe katika Kata ya wazazi wake kwa kutumia influence yake na ukaribu na wazungu.....Deo toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzako......

Hiyo kata ya wazazi wake iliyo pelekewa mradi wa maji na umeme iko jimbo lingine au ni hilo hilo jimbo lake....!?Na kwenye hiyo kata wanaishi wazazi wake pekee au kuna raia wengine...!? Mtu akiwa mbunge inamaanisha kuwahudumia wapiga kura wake wote isipokuwa wazazi wake na watu walio kwenye kata ya wazazi wake au ni wananchi wa jimbo zima!?.....Kuna mambo mengine ukitaka kulalamika fikiria kwanza sio kukurupuka...
 
Kama Haumjui Deo filikunjombe nenda ludewa........jamaa ameshajua safari yake na Magamba imekuwa nzito baada ya kutambua miguu haina nguvu tena ya kukimbia. Deo amejikuta akiwa na ugomvi kila mara na watendaji wa halmashauri kwakuwa hawakufanya kile alichokitaka wakati wa uchaguzi "Ushindi wa Kishindo" ile nae aonwe walau apewe kawizara aka "ulaji" Deo alishiriki katika hila mbali mbali ikiwa ni kumnunua mwenyekiti wa chadema Ludewa na kumtangaza Mpinzani ambaye hakuwa anakubalika.......wakati CC ilimtaka mwingine.... Deo ndio amelobby Mradi wa Umeme na Maji uwe katika Kata ya wazazi wake kwa kutumia influence yake na ukaribu na wazungu.....Deo toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzako......

mwenzetu umeyajuaje hayo? na umeyajua lini hebu tujuze maana waswahili bwana mhhhhhhhh
 
Kama Haumjui Deo filikunjombe nenda ludewa... Deo amejikuta akiwa na ugomvi kila mara na watendaji wa halmashauri kwakuwa hawakufanya kile alichokitaka wakati wa uchaguzi "Ushindi wa Kishindo"......

Kaka,nenda ukajipange upya. Filikunjombe angeshindaje kwa kishindo wakati hakuwa na mpinzani? Mwanaharakati, FYI, this time, Ludewa hawakufanya uchanguzi wa Mbunge. The guy went unopposed.
 
Join Date : 21st March 2012
Posts : 16
Rep Power : 310
Likes Received7
Likes Given2
Vip deo kasababsha mrija wa mijihera ukatwe kwako au kwa watu wako wa karibu nini?
Pole ila hoja za apo juu hazina uzito jipange
 
Utakua umetumwa na magamba ili umchafue Deo,after kusign form ya zitto! Mwanzo ulikua wapi kuleda mada? Kwanza unajichanganya mada yako ni kuuzwa kwa shell yake na hii tena ya mradi wa maji imetoka wapi tena?
 
Hivi mtu mzima unatumwa kama jini hujishtukii tu.Nenda kalime hiyo kazi dunia ya leo unaweza ukachomwa moto.
 
Back
Top Bottom