Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
Tanzania tunahulka ya kuchagua chama na rangi yake bila kuangalia uwezo wa mtu. Mbunge kijana Deo Filikunjombe Haule wa Ludewa anafanya makubwa jimboni mwake na hivyo kuwafunika wabunge wote waliomtangulia na wamekiri hivyo. Hayo ndiyo maendeleo tunayotaka kama alivyofanya Godbless Lema wa Arusha. Kama posho wanazolilia wabunge zingekuwa zinafanya kazi kama hiyo ingeeleweka.
- Picha ya 1: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akikabidhi gari ya wagonjwa kata ya Mlangali kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa gari lalilonunua kwa posho yake milioni 90
- Picha ya 2: Wabunge wa zamani waliomtangulia Filikunjombe Bibi Baraka, Simalenga, Mathias Kihaule na Kolimba.
- Picha ya tatu: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akisakata dansi na paroko wa parokia ya Kifumbe Mwamengele Ngole
- Picha ya nne: Mbunge mstaafu Matias Kihaule ambaye alishawahi kuwa naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Picha ya 5: Paroko Mwamengele Ngole akimkaribisha mbunge Filikunjombe na babake mzazi kusalimia
- Picha ya 6: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akishiriki ibada
- Picha ya 7: Waumini wa kanisa la RC Ludewa wakimpongeza mbunge wao Filikunjombe kwa mchango wake wa maendeleo jimbo la Ludewa leo
- Picha ya 8: Wadau wa wilaya ya Ludewa Bw.Nkwera na wenzake wakiwa nje ya kanisa la RC leo
Akiwahutubia wananchi hao Filikunjombe alisema kuwa mkakati wake katika jimbo hilo ni kuhakikisha anaendelea kupigania maendeleo ya jimbo hilo na katika kuanza amepania kuanza na ujenzi wa lami katika wilaya hiyo ya Ludewa lami ambayo itaanza Ludewa mjini kwenda wilaya ya Njombe.
Hata hivyo Mbunge huyo amesema kuwa ,katika kulipa fidia kwa wananchi wake amelazimika kuzitumia kiasi cha shilingi milioni 90 alizopata bungeni kununua gari ya wagonjwa katika jimbo hilo.
Alisema kuwa hadi sasa amepata kukabidhi gari la wagonnjwa katika kata ya manda ,Rupingu na sasa katikata ya Mlangali ambako pia rais Jakaya Kikwete amepata kuahidi gari katika kata hiyo ya Mlangali .
Filikujombe alisema kuwa Rais Kikwete alipata kuahidi gari katika kata hiyo na kuwa iwapo itafika gari hilo la Rais basi wao wataangalia matumizi ya gari hii ya sasa.