Deo Filikunjombe: Mbunge anayefanya makubwa jimboni mwake

Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.
Kweli tena Used la mwaka 1989. That is nothing comparing to what they are getting from us!
 
Tanzania tunahulka ya kuchagua chama na rangi yake bila kuangalia uwezo wa mtu. Mbunge kijana Deo Filikunjombe Haule wa Ludewa anafanya makubwa jimboni mwake na hivyo kuwafunika wabunge wote waliomtangulia na wamekiri hivyo. Hayo ndiyo maendeleo tunayotaka kama alivyofanya Godbless Lema wa Arusha. Kama posho wanazolilia wabunge zingekuwa zinafanya kazi kama hiyo ingeeleweka.

DSCF7201.JPG
DSCF7109.JPG
  • Picha ya 1: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akikabidhi gari ya wagonjwa kata ya Mlangali kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa gari lalilonunua kwa posho yake milioni 90
  • Picha ya 2: Wabunge wa zamani waliomtangulia Filikunjombe Bibi Baraka, Simalenga, Mathias Kihaule na Kolimba.

DSCF7122.JPG
DSCF7167.JPG

  • Picha ya tatu: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akisakata dansi na paroko wa parokia ya Kifumbe Mwamengele Ngole
  • Picha ya nne: Mbunge mstaafu Matias Kihaule ambaye alishawahi kuwa naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
DSCF7044.JPG
DSCF7018.JPG

  • Picha ya 5: Paroko Mwamengele Ngole akimkaribisha mbunge Filikunjombe na babake mzazi kusalimia
  • Picha ya 6: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akishiriki ibada

DSCF7025.JPG
DSCF7073.JPG

  • Picha ya 7: Waumini wa kanisa la RC Ludewa wakimpongeza mbunge wao Filikunjombe kwa mchango wake wa maendeleo jimbo la Ludewa leo
  • Picha ya 8: Wadau wa wilaya ya Ludewa Bw.Nkwera na wenzake wakiwa nje ya kanisa la RC leo

Akiwahutubia wananchi hao Filikunjombe alisema kuwa mkakati wake katika jimbo hilo ni kuhakikisha anaendelea kupigania maendeleo ya jimbo hilo na katika kuanza amepania kuanza na ujenzi wa lami katika wilaya hiyo ya Ludewa lami ambayo itaanza Ludewa mjini kwenda wilaya ya Njombe.

Hata hivyo Mbunge huyo amesema kuwa ,katika kulipa fidia kwa wananchi wake amelazimika kuzitumia kiasi cha shilingi milioni 90 alizopata bungeni kununua gari ya wagonjwa katika jimbo hilo.

Alisema kuwa hadi sasa amepata kukabidhi gari la wagonnjwa katika kata ya manda ,Rupingu na sasa katikata ya Mlangali ambako pia rais Jakaya Kikwete amepata kuahidi gari katika kata hiyo ya Mlangali .

Filikujombe alisema kuwa Rais Kikwete alipata kuahidi gari katika kata hiyo na kuwa iwapo itafika gari hilo la Rais basi wao wataangalia matumizi ya gari hii ya sasa.

MMM??????? Milioni 90??? garli hili. Mbona naona kam ni used hilo gari. Si bora tu angewanunulia land cruiser ambalo lingehimili ubovu wa barabara za huko Ludewa??? Kama wananchi wameambiwa ni bei hiyo basi imekula kwao
 
aangalie sana hawa magamba hawaaminiki... watamchakachua huyo dogo, ushauri wangu ambao ni wa bure kabisa ahamie CDM...
 
Mwaka mmoja mtu tayari katengeneza milioni 90,hapo bado nyingine alizotumia kwa mambo mengine ndani ya mwaka. Mwalimu anafundisha miaka 30 kiinua mgongo milioni 35 au 25. Kweli hapa kuna usawa wajameni? Nahisi kizunguzungu, hawa magamba kuna haja ya kuchinja mmoja mmoja.
 
Mnanshangaza sana kukubali kuipokea hiyo ambulance. Rushwa haitoisha Tanzania kwa mpango huu.

jamani ni wewe faiza foxy au nimekosea? Ni wewe original au mwingine feki? Mbona kama commets zako now day zimebadilika? Imekuwaje tena? Hawajakulipa au tayari nawe umeingia kwenye siasa za makundi? all in all hongera kwa kuanza kuongea ukweli kwa kile unachoamini ni sahihi au sio sahihi.
 
mhhhhhhhhhhhhhhhhh

Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.
 
MMM??????? Milioni 90??? garli hili. Mbona naona kam ni used hilo gari. Si bora tu angewanunulia land cruiser ambalo lingehimili ubovu wa barabara za huko Ludewa??? Kama wananchi wameambiwa ni bei hiyo basi imekula kwao
Kwenye hotuba yake Filikunjombe alisema ametumia sehemu ya tshs 90 mil alizopewa kama posho ya gari lake kama mbunge kuwanunulia hiyo ambulance.
 
Candid!!,
Anakupa Tshs ngapi kumpigia debe namna hii?
Gamba ni Gamba tu,
Labda tofauti iwe kuna Gamba kubwa na Gamba ndogo!!!

Shark nakupa pole sana. Ninyi ndo wale minyoo ndani ya chama cha magamba. Wasio na uchungu wala huruma kwa nchi yao ila kujineemesha tokana na wavuja jasho wanaoachwa wamening'inizwa njia panda kwa njaa na taabu wasijui wapi wakapate ahueni.

Wengi wanaopinga hapa ni wale wa magamba waliozoea kukamua tu bila kuachia, na sasa wengine wanapowaonyesha njia wanaaibika na kuibua hoja ya kisanii kukandia kwamba ni rushwa. Hakuna kitu chema utakachofanya magamba wakaona umefanya cha maana ila ukitaka wakuone wa maana ingia kwenye system yao ya ulaji hapo watasema huyu mwenzetu.

Toeni tafsiri zo zote lakini sisi wanaharakati katu haturudi nyuma. Mbunge au mtumishi ye yote wa umma anayefanya makubwa kwa nchi yetu hatujali anatoka chama gani tunamwenzi kwa nguvu zetu zote bila woga, maana watanzania tumeshaamka na hakuna kulala tena hadi kieleweke.

Akijitangaza asijitangaze, mbunge si mfadhili wala haina mafundisho kujidai kutowa chochote, hii ni rushwa. Kwanini asipeleke sadaka za Msikitini au Kanisani? huko watajuwa wazifanyie nini, wao ndio kazi zao hizo kuhalalisha pesa chafu.

DSCF7044.JPG
DSCF7025.JPG

FaizaFox, kuna watu hapa wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, wana ufahamu lakini hawafahamu. Huko misikitini na makanisani unamaanisha nini? Akiwa kanisani kama unavyoona kuna sadaka anayotoa na ni nafasi yake kufanya hivyo. Lakini kumbuka sadaka ya kanisani au msikitini ina limit level ya matumizi kutokana na nafasi ya wanaothibiti sadaka hiyo. Lakini kwenye umma haitachagua kwamba tukiajengee msikiti fulani au tukajengee kanisa fulani, kila kutoa huduma kwa wote wananchi wa itikadi zote na hawa wapita njia mradi wapo ndani ya eneo la huduma hiyo.

FaizaFox jaribu kuelewa maana ya aya hii ya maandiko ya Injili takatifu katika Biblia:
"Mpeni kaisari yaliyo ya kaisari na mpeni Mungu yaliyo ya Mungu."
 
Kweli tena Used la mwaka 1989. That is nothing comparing to what they are getting from us!

DSCF7201.JPG

Well, kukosa kabisa na kupata used nini bora? Unapotoa hoja kupinga msaada huo ungetuletea mfano wa aliyeleta ambulance brand new. Nakumbuka siku za nyuma hata mashirika ya umma yalikuwa na utaratibu wa kununua magari mitumba mpaka uwezo ulipowaruhudu ndipo wakaanza kununua mapya. Tena nilishuhudia shirila la bima la taifa tawi la (jina la mkoa nalihifadhi) miaka kadhaa iliyopita ilinunua gari aina ya landrover lililotumika kutoka shirika la kidini nchini kwa vile shirika hilo la dini halikupenda kutumia gari hiyo ambayo ilitumia petrol, wao walipenda magari yanayotumia diesel.
 
Wakuu just for brainstorming, hivi kazi za mbunge ni zipi???????????

MPs must not concede to the demands of their constituents to provide personal financial assistance, as that is not the nature of their representative role in a democratic society.

"Inside his constituency, the MP is expected to carry out the normal duties of meeting and talking to constituents regularly...But again there have
developed certain unscheduled expectations of treating their MP as a provider of financial assistance. This can and has created problems for those MPs who are unable to respond adequately to such expectations.

For as the old adage goes, ‘members of parliament are men and women of high rank, [but] they have nothing in the bank!'" – Pius Msekwa, Former Speaker of the National Assembly of the Tanzania Parliament.
 
akijitangaza asijitangaze, mbunge si mfadhili wala haina mafundisho kujidai kutowa chochote, hii ni rushwa. Kwanini asipeleke sadaka za msikitini au kanisani? Huko watajuwa wazifanyie nini, wao ndio kazi zao hizo kuhalalisha pesa chafu.

swali la kujiuliza kwa nini filikunjombe alikuwa akipinga hoja ya kuondolewa kwa posho za wabunge kama kweli yeye ni mpenda mageuzi?
 
Hilo gari sidhani kama litamaliza mwaka tayari lipo juu ya mawe
 
Shark nakupa pole sana. Ninyi ndo wale minyoo ndani ya chama cha magamba. Wasio na uchungu wala huruma kwa nchi yao ila kujineemesha tokana na wavuja jasho wanaoachwa wamening'inizwa njia panda kwa njaa na taabu wasijui wapi wakapate ahueni.

Wengi wanaopinga hapa ni wale wa magamba waliozoea kukamua tu bila kuachia, na sasa wengine wanapowaonyesha njia wanaaibika na kuibua hoja ya kisanii kukandia kwamba ni rushwa. Hakuna kitu chema utakachofanya magamba wakaona umefanya cha maana ila ukitaka wakuone wa maana ingia kwenye system yao ya ulaji hapo watasema huyu mwenzetu.

Toeni tafsiri zo zote lakini sisi wanaharakati katu haturudi nyuma. Mbunge au mtumishi ye yote wa umma anayefanya makubwa kwa nchi yetu hatujali anatoka chama gani tunamwenzi kwa nguvu zetu zote bila woga, maana watanzania tumeshaamka na hakuna kulala tena hadi kieleweke.

Dah,
Mkuu umenitusi sana kwa kweli!!
bora hata ungenitukania Mama yangu kuliko kunihusisha na magamba!!
Kwa sifa unazommwagia huyo Deo wako from Magamba Camp nahisi wewe ndio member wa hiyo Camp.
Anyway, Deo katumia tu posho kununua hilo gari ambapo Cdm wakiziondoa hizo posho, gari zingenunuliwa nyingi tu kuptia mfuko unaojulikana.
Pili hiyo hiace unaijua bei yake kiasi cha kukubaliana na hiyo 90Mil anayoisema Deo??
 
Usijali mwanamapinduzi, tuko kwenye jukwaa hapa kila mmoja anajitahidi kutetea hoja ila mwishoni tutapata nafasi ya summary na tunapoeremka chini ya jukwaa tunapeana mikono na kwenda pata lunch together. Sorry kama umekwazika ndio mchezo ukiwa uwanjani unaweza shtukia umemkwatua mchezaji two times kushuhudia ukizawadiwa yellow card.
 
Dah,
Mkuu umenitusi sana kwa kweli!!
bora hata ungenitukania Mama yangu kuliko kunihusisha na magamba!!
Kwa sifa unazommwagia huyo Deo wako from Magamba Camp nahisi wewe ndio member wa hiyo Camp.
Anyway, Deo katumia tu posho kununua hilo gari ambapo Cdm wakiziondoa hizo posho, gari zingenunuliwa nyingi tu kuptia mfuko unaojulikana.
Pili hiyo hiace unaijua bei yake kiasi cha kukubaliana na hiyo 90Mil anayoisema Deo??

Tatizo la watanzania wenzangu hatutumii zaidi akili, ila tunaendekeza vionjo. Falsafa ya kijamii ni hii; hatumchukii mtu ila tunachukia matendo mabaya. Mtu anaweza kubadilika kuwa mwema au kuwa mbaya.

Katika siasa hatuchukii watu waliomo ndani ya chama la hasha ila tunachukia itikadi mbaya. Hatupendi chama fulani kwa sababu ya mambo na taratibu zao zinavyopotosha malengo ya maisha bora tunayotazamia. Ndani ya chama hicho kuna walio na mwelekeo mzuri tunaotaka, hakuna sababu ya kuwaweka kando. Bora kutangaza mazuri yanayofanywa na hao ili kuwapa funzo wengine.

Mwanaharakati mzuri ni yule anayejali utu wa watu, si kuchukia watu, maana chuki huzaa machafuko. Na utakuta watu katika familia moja wamegawanyika kiitikadi, sasa chuki ikijengeka si wataanza kufumuana na majambia ndani ya familia kabla ya kuingia kueneza machafuko mitaani? Na si wote waliomo ndani ya Magamba wanaofurahia kinachoendelea, ila wanahitaji msaada wetu kuwaunga mkono, kuwapa moyo na upendo wetu ni silaha kubwa zaidi kuliko chuki ambayo inazidisha ufa. Tukomae, na tukomaze demokrasi kwa manufaa ya nchi yetu, kizazi cha leo na kijacho.

We owe to create better future for next generations
otherwise they will face the worst situation ever.
 
kuna haja ya kuwafundisha watanzania namna ya kushukuru, pia namna ya kufikiri. hilo gari naamini likitumika vema litaokoa maisha ya wengi hasa akina mama na watoto. ni upuuzi kupuuza msaada kama huu. hata kama humpendi huyu dogo, kutoa msaada wa ambulance amefanya jambo la maana sana. binafsi, kwakuwa najua mateso ya wagonjwa wa vijijini, nampongeza katika hili. endelea na moyo huohuo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom