Deo Filikunjombe kupambana na Pindi Chana 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Deo Filikunjombe kupambana na Pindi Chana 2015?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JF2050, Oct 2, 2012.

 1. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Vuta nikuvute na pilika pilika wilayani Ludewa zinaonyesha wazi kwamba kutakuwa na mchuano mtamu sana kati ya Deo na mama aliyetokea kupendwa ndani ya chama na serikali ya JK.

  Na yasemekana Pindi Vhana yumo kwenye mtandao wa EL na majuzi kati wakati wa pilika za uchaguzi hata yule waziri wa hela aliyepigwa chini alikuwa kule kumpasapoti.

  Yetu macho, tusubiri.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Unajua hawezi kugombea ndani ya CCM; JINA LAKE LITAFUTWA... Hatakiwi CCM...
   
 3. C

  Concrete JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Filikunjombe jina lake lilikatwa na kamati kuu, vipi tena awe mgombea?
   
 4. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Azipa 14:19 26th September 2012
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Huyo mama ana jina kubwa kwa viongozi wa CCM, lakini sidhani kama anaubavu wa kupambana na Deogratias Filikunjombe ambaye jimboni kwake ni chanda cha dhahabu ndani ya kisahani.

  Zilipoanza kashkashi za sintofahamu alipoangusha wino kuafiki Waziri Mkuu kusulubiwa kwa udhaifu wake, aliporudi jimboni mwake walimpandisha kwenye punda na kuimba "anapanda punda, mwana wa ...." maana yake kwao ni nabii, ni masiha. Alipokelewa na vyama vyote vya siasa bila kujali itikadi zao, maana yake Filikunjome amewaunganisha Wanaludewa kuwa kitu kimoja. Ni wale vibaraka tu wa CCM ndio wako kivyao.

  Katika hafla ya Filikunjombe kupanda punda wananchi walitamka kwamba wako pamoja naye ko kote aendako hata kama atahama chama cha CCM na kujiunga na chama kingine. Je, huyu Chana Pindi anaoubavu wa kupambana na mpambanaji Filikunjombe? Wanaweza kumwengua jina lake lisipitishwe na chama lakini hawana ubavu wa kushindana naye akisimama kivyake kupitia Chama kingine. Walai nahisi jimbo hilo la Deo filikunjombe limeshakombolewa toka CCM, vinginevyo CCM ifanye kila liwezekanalo Filikunjombe aendee kuipeperusha bendere ya CCM, vinginevyo majuto ni mjukuu.

  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
   
 6. C

  Concrete JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hivi mnaijua CCM kweli au mnatania?

  Kama mpango wa CCM ni kumpa Pindi Chana ubunge mwaka 2015 basi huo ndio utakuwa mwisho wa Filikonjombe.

  Halafu kwanini Pro-Chadema mnapenda sana kupata makapi kutoka CCM ili myape uongozi ndani ya Chadema?

  Kweli Chadema wanashindwa kujenga mtandao wa chama Ludewa na kulichukua jimbo pasipo kusubiri haya makapi ya CCM na kuja kuyapa ubunge?
   
 7. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  - Anaetoka CCM mara nyingi huwa ni yule mzalendo wa kweli ambae ndani ya CCM huonekana adui, walianzisha operation Vua gamba imewashinda na hayo unayosema ni makapi ndo yamebaki ndani ya chama na ndo yenye kutoa maamuzi ya vikao vya CC ya CCM
  - CDM huwa wanapokea mwanachama yeyote anayetoka katika chama chochote au asiye na chama, lakini inapofikia hatua ya kumpa uongozi au uteuzi wa nafasi za kugombea uongozi hapa ufanyika ubembuzi yakinifu na hili litazingatiwa sana 2015 ili isije tokea kama yale ya SHIBUDA.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nisingeafikiana nawe kwa asilimia mia moja kwa mchango wako kwa sababu wanaoenguliwa walio wengi kutoka CCM ni kutokana na uadilifu, uwazi na utetezi wao kwa umma dhidi ya kudhulumiwa na serikali kupitia viongozi wake wenye kubeba dhama ya kuwatumikia. CCM dhamiri zinawasuta kubaki na waadilifu hawa kwa vile hawa watu hawako tayari kula visivyo halali vilivyowekwa kwenye bakuli la mafisadi. Hivyo kuonekana wasaliti wa ufisadi watoswe.

  Ukiongea kuhusu viongozi wa vyama vya siasa hutakosa kugusa CCM ambako walijiengua. Vyama vyote vikubwa vya upinzania vimetokana na watu waliojiengua au kuenguliwa toka CCM.

  Chadema


  • [*=2]Edwin Mtei Mwanzilishi wa Chadema alikuwa Waziri wa Fedha kipindi cha uongozi wa Nyerere, walipishana na Nyerere kuhusu mfumo bora wa uchumi unaotakiwa wa mashirika ya fedha ya umoja wa mataifa.

   [*=2]Dr Slaa alienguliwa katika na vikao vya juu baada ya kupeta kwa kura nyingi jimboni mwake Karatu. CCM walisema Dr. Slaa si mwenzao.


  CUF


  • [*=2]Lipumba alikuwa mshauri mkuu wa uchumi wa Rais Alhasan Mwinyi.
   [*=2]Katibu Mkuu Maalim Seif alikuwa waziri kiogozi wa Zanzibar, CCM hawakumpa nafasi za kugombea Urais visiwani kwa sababu ni Mpemba kama ilivyo kwa Salim.

  NCCR Mageuzi

  • [*=2]Iliakuja pata nguvu kutokana na Mzee wa Kiraracha, Augustino Lyatonga Mrema baada ya kutofautiana na Rais Mwinyi kwa vile Mrema hakuwa tayari kufunika madhambi ya serikali ya CCM na hivyo Mwinyi kumwona Mrema kakosa uwajibikaji wa pamoja.

  Kwa dondoo hizo za vyama vitatu vikuu vya upinzani nchini unaweza kukubaliana nami kwamba kauli yako ya kusema makapi ya CCM kama ingekuwa kauli ya mdomoni ningesema ulimi umeteleza, kwa vile umetumia key board ni dhahiri vidole vyako hukuviweka vizuri kwenye home keys na hivyo kubofya visivyo.
   
 9. cooper

  cooper JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 394
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kwa hiyo Deo, Lugola Mpina, Mkono,Lembeli,Sumaye ni makapi CCM? Chenge,Ngeleja,Nagu,Kapuya and the like ndo pure siyo? Kama ndivyo basi bora makapi mara mia
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa hata akigombea kupitia chama chochote ama mgombea binafsi atashinda tu. Hata mimi nitampa kura yangu. CCM wanachezea shilingi chooni.
   
 11. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unamwita Deo makapi kwa kipimo gani? Yaani wewe unafahamu ubora wa utendaji wake kuliko wananchi wanaoonyesha kumuunga mkono? Pamoja na hayo kama CCM hawamtaki je hana haki ya kujiunga na chama kingine cha siasa akipendacho ikiwa ni pamoja na CDM? Mtazamo wa namna hii kwa kweli unashangaza sana kutoka kwa great thinker!!!!
   
 12. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Samahani mkuu...kweli watu ni wengi lakini ukiangalia kwa makini...unagundua ni WATOTO AMBAO HAWARUHUSIWI KUPIGA KURA......
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Watoto huangulia mbele kufuata kupigwa picha na wenye camera, wakubwa huwa nyuma yao, kwani we hujaona hilo? Ina maana bado hujajua jamaa anavyokubalika Ludewa kila kona? Mpaka kwa hayati Kolimba kando ya ziwa unakoona yupe kwenye mtumbwi. Pindi Chana anabebeka kwa wakubwa wake lakini si kwa wapiga kura.
   
 14. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya mkuu ngoja tuwe na subira maana mapema sana....kutabiri. Hofu yangu kama huyu mama anasapotiwa na mafisadi basi Njombe kazi anayo mkuu. Pia kumbuka hizi kura zina pigwa na wajumbe na sio wananchi. So nguvu ya hawa mafisadi naiogopa sana. Ngoja tumuombe dua jembe Njombe.
   
 15. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ili jembe mimi nalikubari....Anapita alipokanya Tuntemeke Sanga
   
 16. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bure yako filikujombe ni muadilifu kitu ambacho hakitakiwi ccm, pole naona umeshikwa na hofu kama watamtema na yeye kuhama chama, kinachohitajika hata awe kapi ni kulikomboa taifa toka kwenye utawala dhaifu wa mafisadi, kama alivyofanya bungeni kwa kuweka saini ya kutokuwa na imani na yule aka mtoto wa mkulima.
   
 17. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Deo ni jembe but kwa Shibuda yule kweli ni kapi.
   
 18. Kyakukanwa

  Kyakukanwa Member

  #18
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni kweli kabisa! kwanini mnamnyemelea Deo atemwe ccm ndio agombee cdm badala ya kujipanga kivyenu? huo ni udhaifu kwenu cdm
   
 19. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  umesahau kuwa Umri haugandi..acha kuangalia future kwa macho ya ki shibudashibuda
   
 20. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Dah wangeligawa tena hilo jimbo...mbona pesa ya kuendeshea siasa ipo nyingi tu :frusty:
   
Loading...