WAKATI polisi wakiendelea kukalia jalada la Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kubaka na kutishia kuua binti wa miaka 16, sasa suala hilo limefikishwa katika ubalozi wa Marekani. Mbali na hatua hiyo, binti huyo pia amelifikisha jambo hilo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amiri Manento akitaka msaada zaidi.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumatano, binti huyo na dada yake, walisema wameamua kuomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani kwa madai ya kuhofia usalama wao kutokana na vitisho wanavyozidi kuvipata kila kukicha.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, binti huyo alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DDP), hawataki kulifikisha suala lao mahakamani wanakoamini haki yao itapatikana.
Alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakisikia kuwa Marekani ni vinara wa utawala bora na demokrasia, hivyo aliamua kwenda ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini wasaidiwe.
"Kapuya inaonekana anatisha au analindwa sana, lakini sisi tutahakikisha haki yetu tunaipata kwa njia zozote," alisema.
Aliongeza kusema kuwa serikali imeshindwa kuwapa hifadhi kutokana na vitisho wanavyovipata, na wanahofia kuuawa hali inayowafanya wawe waangalifu zaidi.
Tanzania Daima Jumatano limedokezwa kuwa mabinti hao walikwenda ubalozi wa Uingereza kuomba hifadhi hiyo ambako walielekezwa kuwa wakienda katika ubalozi wa Marekani shida yao itatatuliwa.
Source: Tanzania Daima