Kuyafanya Meno Yenye Rangi Kuwa Meupe (Teeth Whitening)

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Naomba msaada wenu, kama mtu anasafisha meno yake mara 3 kwa siku lakini bado yana rangi ya 'njano' na sio meupe!

teeth-whitening-review.jpg


UFAFANUZI NA MICHANGO KUTOKA KWA WADAU
Watu wengine wakiona rangi ya 'njano' wanahisi kwamba meno hayo ni 'machafu'. Je, kuna namna ya kuweza kuyasafisha ili yang'ae au yawe meupe?

Wakati wa muongo uliopita mahitaji ya kuboresha muonekano au kurembesha meno yameongezeka kwa kiwango kikubwa hasa katika nchi zilizoendelea. Hii imechochewa na kupatikana kemikali mpya za meno (dental

meterials) na vifaa kwa kasi ikiendana na kuboresha vile vya zamani. Sehemu nyingine iliyosababisha madaktari na mainjinia wa meno kuyafanya meno kuwa meupe ni sehemu ya fani ya taaluma ya meno chini ya urembeshaji wa meno, fani hii uhusika na kuboresha muonekano wa meno hasa yale yanayoonekana wakati

wa kutabasamu na kuongea. Inahusisha matibabu kama kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe, kunyoosha meno yaliyojipanga vibaya pamoja na kukarabati meno yaliyovunjika na yale yaliyoumbika visivyo (malformed teeth). Huko Uingereza na sehemu nyingine za magharibi wanawake walio wengi wanatumia maelfu ya paundi/euro kuboresha muonekano wa meno yao hali ambayo inaanza pia kuingia huku kwetu.

Nini husababisha meno kugeuka rangi?
Meno kugeuka rangi husababishwa na kimojwapo au muunganiko wa vitu vifutavyo: -


Vyakula na vinywaji kama vile vinyaji vyenye kaboni, wine na sigara.
Utumiaji wa maji yenye kiwango cha juu cha madini aina ya magadi (fluoride) na utumiaji wa magadi katika kulainisha vyakula wakati wa kuandaa vyakula vigumu kama maharage na makande. Utafiti uliofanywa na Prof.

Mabelya na wenzake nchini Tanzania umeonesha kuwa kubadilika kwa rangi ya meno kutokana na magadi kwa kiwango kikubwa husababishwa na matumizi ya magadi katika mapishi ya vyakula hasa makande kule maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro/Moshi kuliko inavosababishwa na matumizi ya maji.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ngumu za jino (enamel and dentine defects). Iwapo sehemu ngumu ya meno imeumbwa ikiwa laini ni rahisi kufyonza rangi na jino kuota likiwa limegeuka rangi au kubadilika baada ya kuota.

Matumizi ya madawa kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayajapata madini ya kutosha na hata watoto wachanga ambao meno yao hayajakomaa.
Kufa kwa kiini cha jino hasa kutoka na kujigonga wakati wa ajali au kupigana ngumi usoni (pulp necrosis), jino

likigongwa kwa nguvu damu huvuja ndani ya kiini cha jino na baadaye huchachuliwa na kutoa kemikali ambayo hupenya kwenye vitundu vidogo vidogo kwenye dentine na kujidhihirisha kama kijivu, zambarau au hata

nyeusi. Hali hii yaweza tokea mapema baada ya kupata ajali lakini wakati mwingine inaweza kuchukua miaka kadhaa hata arobaini kipindi ambapo mtu hakumbuki kuwa aliwahi kutwangwa ngumi.

Kuyafanya meno yenye rangi yasimpendeza mwenye nayo kuwa meupe
(Bleaching or teeth whitening)

Huku ni kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe au kuongeza weupe wa yale yenye rangi ya kawaida kufikia kiwango cha weupe atakacho muhitaji kwa kutumia kemikali maalum. Rangi ya kawaida ya meno kwa walio wengi ni uweupe kama wa maziwa (milky white). Rangi yeyote nje ya hiyo si ya kawaida (abnormal color or discoloration).


Kuwa na rangi isiyo ya kwaida hasa kwa meno ya mbele linaweza kuwa tatizo kubwa la urembo na kumsumbua mhusika kisaikolojia. Kuyafanya meno kuwa meupe kumelenga kuwaondolea wahusika tatizo hili japo mafanikio yake yanategemea kiwango cha rangi isiyo ya kawaida.


Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia kemikali, kunaweza kubadili yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kutoka yale yaliyoathirika kwa kiwango kidogo mpaka cha kati.


Kufanya meno yawe meupe kwa kutumia kemikali huunguza (oxidises) rangi ya jino na kuiondoa. Kemikali zinazotumika zina hydrogen peroxide 30%-35% na baadhi carbamide peroxide 10%. Kemikali hizi huweza kuondoa rangi zilizosababishwa na vyakula, vinywaji, dawa za tetracycline, rangi kidogo iliyotokana na utumiaji

wa madini ya magadi kwenye vyakula au kwenye maji (mild fluorosis) na meno yenye rangi ya njano au kijivu itokanayo na umri kuwa mkubwa. Inaweza pia kuondoa rangi itokanayo na uvutaji wa sigara na matumizi ya ugoro. Kwa wavutaji wa sigara sharti waache pindi watumiapo kemikali hizi kwani muunganiko wa hydrogen

peroxide na kemikali zilizopo kwenye moshi wa sigara unahisiwa kuongeza madhara zaidi ambayo tayari moshi wa sigara husababisha kwenye mwili wa binadamu. Haishauriwi kwa akina mama wanaonyonyesha kutumia dawa hizi pamoja na kwamba hakuna madhara yanayojulikana mpaka sasa.

Teeth%20Whitening%201.jpg

Kuboresha weupe kwa kutumia chemikali

Kupiga meno viraka (Veneering)
Hii hufanyika kwa kuondoa sehemu ndogo ya juu ya jino kwenye enamel kama 0.5-1mm na baadaye kupandika dawa yenye rangi nyeupe kulingana na mgonjwa anavyotaka mwenyewe. Picha inayonesha meno yaliyobadlika rangi kutokana na magadi kabla na baada ya kupigwa viraka

Teething%20Whitening%202.jpg

Kabla ya kiraka. Na Baada ya kupigwa kiraka(veneer)
Kumbuka: kuna rangi zaidi ya 26 nyeupe ambazo miongoni mwake mgonjwa anaweza kuchagua anayoitaka.

Kuyafanya Meno Yenye Rangi kuwa Meupe (Teeth Whitening)
---
Naomba nianze kwa kukushauri ni vema daktari wa meno akuangalie tatizo lako na ndo ushauri mzuri & kitaalamu waweza tolewa!

Mambo yanayoweza sababisha njano:

Meno ya mwanadamu huanza kutengenezwa km sikosei miezi 3 ya mwisho wa ujaozito wa Mama(last trimister)...kinachotokea siku za nyuma palikuwa na dawa iitwayo Tetracyline....ilikuwa maarufu sana enzi zile..si dawa zote zinaweza kupenya Placenta ila dawa hii ilikuwa na uwezo wa kupenya na kusababisha madhara hayo kwa meno ya mtoto.

Pia yaweza rangi hiyo ya jano ni madhara ya madini ya Fluoride.. tatizo hili lipo sana kwa watu toka shinyanga, singida, moshi...(along rift valley).

Ama pia ni uchafu wa meno umetengeneza tabaka gumu ambapo haliwezi kusafishika kwa kupiga mshwaki mpaka mtu afanyiwe matibabu ya kusafisha kinywa (scaling).

Ushauri
Tafuta daktari wa meno aliyekaribu nawe,Kama ni kusafisha atakufanyia Scaling na Kama yametokana na tetracycline au fluoride anweza kukufanyia toothwhitening and/orveneer.

Ukifanya hivyo guarantee 100% utaonekana smart ht umiss Tz mwakani waweza gombea (samahani sijajua jinsia yako!!!)
---
YAWE MEUPE NA MUONEKANO BOMBA
Meno ni kiungo cha ajabu sana ambapo kinapokua na muonekano mzuri hukufanya uwe na furaha na tabasamu zito mbele ya wenziwako. Na kinyume chake mtu hukosa kujiamini mbele za watu na tabasamu la dhati hutoweka. Hivyo nimeona ipo haja ya kukuainishia kwa mukhtasari njia anuai za Kung'arisha meno yako na kukufanya ujiamini katika mazungumzo.




Meno kuwa ya manjano(discolouration) huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya vyakula tulavyo, matumizi Ya vinywaji vya viwandani ambavyo huaribu kabisa meno yako. Lakini pia namna ya kupiga mswaki huchangia hilo, hivyo ni vema kuzingatia kanuni sahihi za upigaji wa mswaki.


Meno kuwa na rangi ya kahawiya hii husababishwa na aina ya maji kutokana na aina ya miamba ya sehemu husika .mfano uzoefu unaonesha maji yenye kiwango kikubwa cha madini ya fluoride huchangia meno kupoteza rangi yake ya asili , Matumizi ya sigara, tumbaku,unywaji wa kahawa kupita kiasi.



Hizi hapa ni njia mbadala za kufanya meno yako kuwa meupe na mvuto;



Baking soda .sodabiki,au maarifu kama unga wa soda. chukua nusu kijiko cha baking soda pigia mswaki, au weka pamoja na matone kadhaa ya limau, au maji ya limau ya vuguvugu. Pigia mswaki.hii husaidia sana Kung'arisha meno kutokana na Tahiti za wadau wa afya. Lakini ni vema kutumia kwa uangalifu, yaani mtu asizidishe zaidi ya Mara tatu kwa wiki,




Maganda ya ndizi za kuiva (banana peels). Unaweza kusugua meno yako kwa kutumia maganda ya ndizi, maganda ya ndizi yana madini kama magniziam, potasiam, na manganese, hivyo husaidia kutakatisha meno yako. Sugua meno yako kwa maganda ya ndizi kisha acha kwa dakika angalau Milo na uendelee kupiga mswaki wako kama kawaida .



Kutafuna karoti, jitahidi kutafuna karoti kwa wingi mno kwani husaidia kufanya meno yako yawe meupe na mvuto bomba.




Matumizi ya bizari (turmeric), bizari hutumiwa kama kiungo katika jamii nyingi za upwa wa afrika mashariki. Lakini pia tafiti zinaonesha kuwa hutakatisha meno yetu. Ni vizuri ukaongezea na juisi ya limau kidogo na kuutumia mchanganyiko huu .




Mafuta, unaweza pia kusugua meno yako kwa kutumia mafuta ya mzaituni (olive oil), au mafuta ya ufuta (sesame oil) au mafuta ya halizeti (sunflower oil) .namna ya kutumia chukua kijiko kimoja cha mafuta husika na sugua meno yako ,kisha piga mswaki wako kama ada ,pia unaweza kutumia mafuta ya nazi husaidia mno





Limau, unaweza kusugua meno yako kwa kutumia maganda ya limau, au kutumia maji ya limau au kutumia dawa za mswaki zenye limau ndani yake.




Matumizi ya karafuu(cloves), hii uboresha harufu ya kinywa, kuuwa vijidudu kinywani na kulinda vizi na meno kwa ujumla


Ahsanteni kwa kufuatilia makala zangu.
---
Mahitaji:
Vitu viwili, limau na baking soda au wengine huita bicardonate of soda nayo ni ile wamama huitumia wanapopika maandazi au mikate, inapatikana maduka ya kawaida hata kwa mangi hapo mje ipo.

Namna ya kuandaa;
Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja maji maji yake kisha changanya baking soda ya unga kijiko kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.

Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.

Muhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokarabia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini. Ukifanya hivi mara 2 au 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanaong’aa na kupendeza.

Vyakula kadhaa vifuatayo vinasaidia kung’arisha meno yako navyo ni pamoja na machungwa, stawrberry, mapeazi, maziwa na mtindi, maji ya kunywa, jibini, broccoil, celery. Tufaa, kitunguu maji, mbegu mbegu (kama karosho, karanga) nk.

Vyakula au kitu vinavyoharibu rangi ya meno ni pamoja na uvutaji tambaku/ sigara, chokoleti, chai iya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine baridi vyenye kaffeina.

===
PIA NI MUHIMU KUSOMA MADA HIZI:
1. Fahamu: Meno yaliyooza yanatibika - JamiiForums

2. Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya - JamiiForums
 
hi,
naomba msaada wenu, kama mtu anasafisha meno yake mara 3 kwa siku lakini bado yana rangi ya 'njano' na sio meupe! Watu wengine wakiona rangi ya 'njano' wanahisi kwamba meno hayo ni 'machafu', je kuna namna ya kuweza kuyasafisha ili yang'ae au yawe meupe?
labda ueleze uko eneo gani kani kila eneo lina madini ambayo pengine ndiyo yanasababisha hiyo rangi kwenye meno
 
Naomba nianze kwa kukushauri ni vema daktari wa meno akuangalie tatizo lako na ndo ushauri mzuri & kitaalamu waweza tolewa!

Mambo yanayoweza sababisha njano:

Meno ya mwanadamu huanza kutengenezwa km sikosei miezi 3 ya mwisho wa ujaozito wa Mama(last trimister)...kinachotokea siku za nyuma palikuwa na dawa iitwayo Tetracyline....ilikuwa maarufu sana enzi zile..si dawa zote zinaweza kupenya Placenta ila dawa hii ilikuwa na uwezo wa kupenya na kusababisha madhara hayo kwa meno ya mtoto.

Pia yaweza rangi hiyo ya jano ni madhara ya madini ya Fluoride.. tatizo hili lipo sana kwa watu toka shinyanga, singida, moshi...(along rift valley).

Ama pia ni uchafu wa meno umetengeneza tabaka gumu ambapo haliwezi kusafishika kwa kupiga mshwaki mpaka mtu afanyiwe matibabu ya kusafisha kinywa (scaling).

Ushauri
Tafuta daktari wa meno aliyekaribu nawe,Kama ni kusafisha atakufanyia Scaling na Kama yametokana na tetracycline au fluoride anweza kukufanyia toothwhitening and/orveneer.

Ukifanya hivyo guarantee 100% utaonekana smart ht umiss Tz mwakani waweza gombea (samahani sijajua jinsia yako!!!)
 
onana na dentist, mwambia unataka kufanya teeth whitening by zoom.
ukishafanyiwa iyo kitu, mtu akikucheki anaweza dhani una milk teeth.
hiyo ni treatment ni kiboko, kama si ya njano sana basi ukifanyiwa bleaching inatosha.
 
onana na dentist, mwambia unataka kufanya teeth whitening by zoom.
ukishafanyiwa iyo kitu, mtu akikucheki anaweza dhani una milk teeth.
hiyo ni treatment ni kiboko, kama si ya njano sana basi ukifanyiwa bleaching inatosha.
poa mkuu
 
onana na dentist, mwambia unataka kufanya teeth whitening by zoom.
ukishafanyiwa iyo kitu, mtu akikucheki anaweza dhani una milk teeth.
hiyo ni treatment ni kiboko, kama si ya njano sana basi ukifanyiwa bleaching inatosha.
Je kama yamekuwa ya brown (meno yaliooza- kama wengi wanavyotamka) Je kuna uwezekano wa kuyabadilisha na kuwa milk- teeth?
 
Je kama yamekuwa ya brown (meno yaliooza- kama wengi wanavyotamka) Je kuna uwezekano wa kuyabadilisha na kuwa milk- teeth?

inawezekana, kuna njia mbalimbali kutegemeana na hali ya meno.
unaweza kufanya external bleaching,au internal bleaching.
internal bleaching ni nzuri kwa meno kwa hayo meno unayozungumzia kwasababu ina-brightens teeth from the inside out, wakati external bleaching ina-brightens teeth from the inside out.

vilevile dentist anaweza aka-add some coating layer, ili kuficha rangi ya njano/brown.

kumbuka kuwa hizi sio permanent solutions, kwamfano hiyo njia ya ku-add coating layer,baada ya mda hiyo layer inalika(arond 15yrs), bleaching method inategemea na wewe unavyotunza meno yako kama ni mvutaji sigara baada few months weupe unapotea.
teeth zooming,20 years guarantee.
 
inawezekana, kuna njia mbalimbali kutegemeana na hali ya meno.
unaweza kufanya external bleaching,au internal bleaching.
internal bleaching ni nzuri kwa meno kwa hayo meno unayozungumzia kwasababu ina-brightens teeth from the inside out, wakati external bleaching ina-brightens teeth from the inside out...
apo sijakuelewa...
 
kuna watu wanasema chumvini kuna kemikali zinazong'arisha meno. (N:B zamia chumvini et yowa own rizk)
 
Ubarikiwe sana uliyeuliza swali na wachangiaji wengine, kumbe mambo haya yanawezekana. je Agakhan hospital yupo dentist mzuri wa kufanya hii huduma yakupendezesha watu au anaweza kupatikana kwingine.

kama yupo na anakubali card za strategy ili tuendelee kufurahia dunia. Is how much by cash for bleaching, teethwhitening, scaling etc. Huduma hii inachukua muda gani kwanin wengine miezi yakwenda milimani kula ndizi na nyama choma tukiwa na babu na bibi zetu vijijini imekaribia
 
mie navyowajua hawa wataaluma wa meno...kila kitu kwao kinawezekana hata kibogoyo wa kuzaliwa anakuwa na meno yoooote 32...ila sasaaaa...pale kunako swala zima la malipo ..duuu...hawa hawaoni aibu kumwambia mtu 6 figures mpaka 7 figures za tshs....hawa jamaa ni noma aisee kwa bei
 
ila mkuu mbona unataka ku-ondoa hizo grilles zako mzee...wenzako huko mbele wanalipia kuweka hizo rangi kwa vito mbalimbali...wewe mzee ni naturally gifted...ahahaha..lil-wizzy akikusikia unataka kutoa grilles anaweza kulia kwa hasira...you are blessed mannnn
 
ila mkuu mbona unataka ku-ondoa hizo grilles zako mzee...wenzako huko mbele wanalipia kuweka hizo rangi kwa vito mbalimbali...wewe mzee ni naturally gifted...ahahaha..lil-wizzy akikusikia unataka kutoa grilles anaweza kulia kwa hasira...you are blessed mannnn
teh teh teh..mamsapu kakomaa....kama vipi hakuna 'denda'
 
Yote hayo ya nini bana sawa na ukiwa na mvi unaanza kupaka kantar ikisha nywele zinakuwa na rangi ya kutu ,utableach mpaka lini ilihali unakaa usa river au marangu the teh
 
Nenda Muhimbili IPPM clinic (fast track) jengo lipo opposite na Maternity Clinic Chumba namba 73...Muulizie Dr Nyerere au Dr Gombo utapata tiba ya tatizo lako kwa kutumia strategy card yako..............wataka umissTz nini? All the best
 
Back
Top Bottom